Wanaume kwa hili, laana itatumaliza

LEVEL

Senior Member
Joined
Jul 4, 2013
Posts
195
Reaction score
51
Kuna wanaume wanaooa kabla hawajajipanga kimaisha hivyo hushirikiana vizuri na wake zao katika kutafuta maisha, ila pindi tu mambo yanapokua mazuri ghafla wanaume hawa hubadilika na kuacha ustaarabu waliokua nao enzi zile hawana kitu na huanza mateso kwa wake zao waliosaidiana kutafta maisha na kuwaona wake zao hawafai wakati wao ndo walio wadumaza watoto wa watu kwa matatizo ya kutokuwa na uwezo wa kuwapatia matunzo yanayostahili.

Watoto wa watu wanavumilia mlo moja kula ugali kila siku kusuka mara mbili kwa mwaka leo ukifanikiwa unamwona hafai! Tuacheni hizo laana aisee, baki na mkeo kwani wewe ndo ulomfanya mtoto wa watu awe hivyo alivyo.
 
Mkuu nakupa big up sana....umerusha jiwe kwenye nyumba ya vioo
yaani sio muda utasikia yowe kali sana.

wadada fanyieni kazi alichokisema jamaaa na wadau tujirekebishe
juu ya hii tabia kwani mdau kasonya kuwa hii laana (curse) itatumaliza.
 
unamwamchia mali zote.....wanazingua sana bana....kila kitu unampa na mtaji kabisa asiwe na kisingizio.....
 
Wanaume wana laana nyingi sana kwa wanawake wao wanavowatelekeza bila sababu simply wamepata walicho kipata
 
Wamekusikia...Wamekuelewa wanaume wenye tabia hizo,ushauri wako unagusa sana.
 
Na wanamama wanaobadilika pindi waume wakiyumba, wao inakuwaje? Au better them, than us?
 
Vere true, yani ule msemo wa maskini akipata Nadhani huwa unawahusu wao...
Mara chache sana mwanaume apate abaki na ustaarabu wake
 
hapo umeongea ukweli ila umeongea upande mmoja tu....!!!
vp upande wa hao wanawake hakuna laana yao..!!!
 

Nimeshindwa kusoma. Kweli Mh. Mungai na Shukuru wametuharibia bongo za watoto wetu!!!
 
Wengi wenye tabia hiyo hufa vifo vibaya sana wakiwa lonely and as losers. Fuatilia utaona!
 
Hautakiwi kumtelekeza ila kuwa very strictly, maana Kumwendekeza mwanamke ni sawa na kucheza na nyani shambani, jibu lake unalijua...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…