Wanaume kutokusaidia kupika

Wanaume kutokusaidia kupika

Parata

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2011
Posts
3,090
Reaction score
693
Katika ndoa wote tunajua kuwa ni kusaidiana yaani katika kazi na majukumu mengine,sasa kuna wanaume kwenye ndoa zao wanakua kama mke wake ni housegirl wake,kupika kila siku yeye,kufua,kudeki.kidume akija yeye ni kula tu na kujimwayamwaya kitandani,kiukweli hali hii si nzuri.
 
Malezi,mazoea na mfumo dume ndio chanzo.
Na nyie wanaume mnachangia saa wanaume wenzenu wawe hivyo kwa kuogopa mtawaona wanatawaliwa na wake zao. Kwenye vikao vya kaunta hamuishi kusema namna gani mwanaume anatakiwa kuonyesha Uanaume kwa kuwa mkorofi kwa mkewe. Wengie wanadhani kuoa = housegirl anaetimiza majukumu ya kitandani na kuchangia uchumi.

Wasaidieni wake zenu bana ili waweze kuwahudumia vizuri faragha!!
 
Katika ndoa wote tunajua kuwa ni kusaidiana yaani katika kazi na majukumu mengine,sasa kuna wanaume kwenye ndoa zao wanakua kama mke wake ni housegirl wake,kupika kila siku yeye,kufua,kudeki.kidume akija yeye ni kula tu na kujimwayamwaya kitandani,kiukweli hali hii si nzuri.

Wengine hatuna matatizo na kupika. Tunapika kila mara.
 
Wacha niseme am lucky,wangu mie ananisaidia kila kazi bila hata ya kumuomba....nfkiri inategemea na malezi....
 
Ujifunze na mengine basi kufua,kudeki 😉😉😉

Mbona nnajua mengi tu. Sifuliwi nguo na mtu. Na huwa sideki kwa kutumia ile mitambara. Nina hardwood floors na kapeti. Natumia mop na vacuum cleaner.

Sijui kumtumikisha mtu.
 
Mwanaume umleavyo ndivyo akuavyo😕
 
Ujifunze na mengine basi kufua,kudeki 😉😉😉

pants1.jpg
 
Mbona nnajua mengi tu. Sifuliwi nguo na mtu. Na huwa sideki kwa kutumia ile mitambara. Nina hardwood floors na kapeti. Natumia mop na vacuum cleaner.

Sijui kumtumikisha mtu.

Nicee🙂🙂🙂🙂

Hukuniambia ilikuaje siku ile ya kitu nyama ya mbuzi
 
Nicee🙂🙂🙂🙂

Hukuniambia ilikuaje siku ile ya kitu nyama ya mbuzi

Ilikuwa baab kubwa. Na hivi Seahawaks walishinda kwa kishindo....

Wenye kupenda Heineken walizishushia, wenye kupenda Mad Dog 20/20 nazo zilikuwepo. Ilikuwa bomba sana

MD_2020.jpg
 
Ilikuwa baab kubwa. Na hivi Seahawaks walishinda kwa kishindo....

Wenye kupenda Heineken walizishushia, wenye kupenda Mad Dog 20/20 nazo zilikuwepo. Ilikuwa bomba sana
ww ni mdau wa NFL...???
 
Back
Top Bottom