Wanaume kupika na kupakua ni ushamba jamani??

Ni kweli kabisa, hata mimi baba yangu mzazi alipokuwa hai (kwa sasa ni marehemu) siku moja moja alikuwa anaandaa bonge la msosi halafu tunakula pamoja katika familia. Kweli inapendeza sana. Pia hata mimi mwenyewe mtoto wa kiume kuna wakati wazazi wakitingwa sana na kazi na pengine wakati fulani wanakuwa wamechoka, basi hata mimi naingia jikoni naandaa msosi wa nguvu.

Ila si vema sana mwanamke kukaa sebuleni na mashosti zako halafu mwanaume akawa jikoni anapika. Kwa hapa italeta picha ambayo si nzuri kwa hao mashosti zako ambao mkishaagana tu wanabadilika kuwa Radio Umbea. Ila kama mwanamke ni mgonjwa sana na huna uwezo wa kukaa jikoni kwa wakati huo itakuwa sawa maana hata hao mashosti watakuwa wanaiona hali yako.

Halafu kwenye nyumba za kupanga ambako mara nyingi mnakaa uani kupika mfano familia 5 au zaidi, hata 2 si vema kwa mwanaume kukaa na wanawake kupika. Kwa hapo kama mwanamke hajiwezi ni mgonjwa sana, basi mwanaume afanye utaratibu wa kuiomba familia mojawapo za wapangaji hao kumsaidia kupika.

GM7 kumbe bado wakaa na wazazi eeeh next karibu kwangu tuaidiane kupika
 
Aisee nimependa hiyo kumbe tuko wengi ambao baba zetu walikuwa wanatupikia, Manake kwa marafiki zangu nilikuwa sioni hiyo halafu nilikuwa naona aibu nikija na rafiki home afu tunakuta baba ndo anapika!!!!
Tena kuna wakati mimi mtoto wa kiume rafiki zangu walikuwa wananitembelea nyumbani halafu bahati nzuri/mbaya wananikuta niko jikoni. Nilikuwa sioni cha ajabu nawakaribisha sebuleni halafu nawaambia niko studio naandaa songi.
 
wakuu suala la kupika kwa wanaume ni zaidi ya mapenzi au kuwa mume *****; wanaume naturally ni wapishi wazuri sana na ndio maana hoteli nyingi chefs wengi ni wanaume.

kupika ni art kama vile sanaa nyingine na kusema kweli kipaji kile hakiigiki,

wanaume wengi waliolelewa vizuri hujua kupika na huweza kupika, pia wanaume waliowahi kuishi mabachelor au colleges mara nyingi wamekua wanapika

Now back to family issues
Mwanaume anayepika mara nyingi huwa na kipaji au uwezo wa kuwa karibu pia hata na watoto na mamaa. zaidi ya hayo, mwanaume anayepika is naturally romantic, more helpful, loved by kids na pia inaonyesha ana muda wa kufanya mazuri kwa mke na watoto

Moreover, kupika tu ni fun kinoma

TO ANSWER THE QUESTION, MWANAUME KUPIKA SIO USHAMBA

Du! Wacha nikachukue kozi ya upishi!:rolleyes:
 
Kapewa "shuntama" huyo! Mwanaume marufuku kupika mkeo akiwepo!!!!
Halafu nyie ndo tunawaqkutaga pale Leaders club asubuhi mnachoma "ngumi" mimoshi kila mahali....lakini mkifika kwenu mnajifanya wa miaka ileeee!

Kidume lazima uchome nyama home, misamaki ichomwe,,,,,,,,watu walio kwenye nyumba yako wajue kuwa, hivyo vitu sio vinapatikana bar tu!
 
GM7 kumbe bado wakaa na wazazi eeeh next karibu kwangu tuaidiane kupika
Kwa sasa bado namtunza mama (baba ni marehemu). Nitashukuru kama tukikaa pamoja milele na kusaidiana kupika. Teh teh teh teh teh teh
 
mweh Baba_Enock una ukoloni wewe .. sidhani kama mamsap anasaidiwa hata kutandika kitanda :)
Kama sio hiyo blue, ungejibu tuhuma kwenye red. mnataka msaidiwe kila kitu wakati mwingine. mtasaidiwa hadi nanihii, shauri yenu.
 
Napenda kupika ila kila nikipika nakosolowa sijui kupika,kitu ninachoweza kupika labda chai na tambi.Kuna siku wife alichelewa kazini nikajitosa jikoni nakwambia wali ulikuwa kama ugali mpaka watoto wakasusa ikabidi nikawachukulie nyama choma wasilale na njaa.

Siku hizi mara nyingi nikiwahi nyumbani nakuwa na wife jikoni namsaidia kukata nyanya,vitunguu na nk,natumaini muda si mrefu nitafuzu kozi ya upishi chini ya uangalizi wa karibu wa wife.
 
Kapewa "shuntama" huyo! Mwanaume marufuku kupika mkeo akiwepo!!!!
Sawa kabisa kiongozi. Unatumia kinywaji gani vile?

mweh Baba_Enock una ukoloni wewe .. sidhani kama mamsap anasaidiwa hata kutandika kitanda :)
Nilitaka nikujibu kwa hasira hapa. Lakini kuna kiongozi kamaliza kila kitu. Msome hapo chini.

Kama sio hiyo blue, ungejibu tuhuma kwenye red. mnataka msaidiwe kila kitu wakati mwingine. mtasaidiwa hadi nanihii, shauri yenu.
 
Napenda kupika ila kila nikipika nakosolowa sijui kupika,kitu ninachoweza kupika labda chai na tambi.Kuna siku wife alichelewa kazini nikajitosa jikoni nakwambia wali ulikuwa kama ugali mpaka watoto wakasusa ikabidi nikawachukulie nyama choma wasilale na njaa.

Siku hizi mara nyingi nikiwahi nyumbani nakuwa na wife jikoni namsaidia kukata nyanya,vitunguu na nk,natumaini muda si mrefu nitafuzu kozi ya upishi chini ya uangalizi wa karibu wa wife.
Mkubwa, as time goes, you will be too involved with life, hutaweza kuka kaa jikoni kila saa.

Ushauri wa bure, kama umeoa juzi juzi............tengeneza utaratibu wa kudumu, ambao ni sustainable, usifanye vitu ambavyo in 4 years down the line hutaweza kuvifanya. Usikae kae jikoni kila wakati, tafuta unachoweza, na uwe unawapikia wafurahi.

Unachofanya sasa hivi, ni kumrithisha mkeo, lakini watoto watajuaje hiki chakula amepika baba?
 
Tena kuna wakati mimi mtoto wa kiume rafiki zangu walikuwa wananitembelea nyumbani halafu bahati nzuri/mbaya wananikuta niko jikoni. Nilikuwa sioni cha ajabu nawakaribisha sebuleni halafu nawaambia niko studio naandaa songi.

Mwanangu hilo songi la kihindi.
 
Ni kweli kabisa

kuna watu awajui mapenzi ni kushhirikiana lakini wengine wanaamini ushirikiano vitandani tu..hapa ndipo kosa kubwa!!!!
Tusaidiane kila department jamani sio cfo,ceo wewe cio wengine no..wote tuwe kitu kimja na i can imagine jamani mwanamke wa aina hiyo anavyofurah moyon mwake...hapo utakuta ata limbwata ajawekewewa akiwekewa???
Braaaa braaaaaa
Ni vizuri kushirikiana na kusaidiana, lakini kuna division of labour ya asili. Mwanaume atapasua kuni, ataua nyoka akiingia ndani n.k. Kama ni kupika iwe hakuna budi labda mama ana dharura sio amekaa sebuleni na wewe dume nzima unasokota ugali.

Limbwata hilooo:D
 
Mkubwa, as time goes, you will be too involved with life, hutaweza kuka kaa jikoni kila saa.

Ushauri wa bure, kama umeoa juzi juzi............tengeneza utaratibu wa kudumu, ambao ni sustainable, usifanye vitu ambavyo in 4 years down the line hutaweza kuvifanya. Usikae kae jikoni kila wakati, tafuta unachoweza, na uwe unawapikia wafurahi.

Unachofanya sasa hivi, ni kumrithisha mkeo, lakini watoto watajuaje hiki chakula amepika baba?

Ni jambo la hatari hilo. Hata hivyo nadhani tunaweza kuwa tunaishi maisha toafuti. Mfano, nyumbani kuna wife, msichana wa kazi, ndugu mmoja au wawili wa kike. Kwa nini mimi niingie jikoni kupika, na hasa hasa chakula cha kawaida kama ugali? Nitafanya kitu kingine ili hiyo timu ya wapishi wazuri wa wali na ugali wapate kitu cha kupika. Ila kama kuna kitu special mfano salad, au mchuzi fulani naweza kujitosa. Hata hivyo pamoja na kupenda kumsaidia wife, kama tunaishi uswahili siwezi hata siku moja kukanyaga jikoni. Kama mama anaumwa nitatumia jiko la mchina chumbani na siyo kwenda kwenye kijiwe cha umbeya ati nataka kupika. Naomba mnisamehe, ila ndo ukweli wangu!!

tatizo lao mkuu, usipokuwa makini, mdeko unageuka regulation.
I tell you me.

Hili ni jambo la muhimu sana. Kama inawezakana ni vizuri kuwa na mgawanyo wa kazi unaoeleweka badala ya kuishi kwa mipango ya kudandia dandia. Kama wote mnapika basi ieleweke na ikibidi muwe na ratiba kabisa ili nani ajue yuko zamu. Na kama mwenye zamu akikwama basi anaomba msaada badala ya kuwa na kitu kisichoeleweka ambacho kinaweza kumpa mmoja wenu nafasi ya kumchezea mwenzake (to take advantage).
 
Ni vizuri kushirikiana na kusaidiana, lakini kuna division of labour ya asili. Mwanaume atapasua kuni, ataua nyoka akiingia ndani n.k. Kama ni kupika iwe hakuna budi labda mama ana dharura sio amekaa sebuleni na wewe dume nzima unasokota ugali.

Limbwata hilooo:D
Mchili bana!!
Sasa hapa mjini wewe unapasua kuni saa ngapi?, unakaa kwenye shimo mpaka nyoka aingie ndani?
nini kitakuwa substitute ya zile natural devision of labour ambazo kwa kijijini, zinakuja kutokana na mazingira?
kuna vitu vingine, we do for the family............not for gender.
 
Binafsi nikiwa nyumbani kwangu(hasa wakati wa weekend) huwa kuna wakati napika(mimi ni mpishi mzuri sana) na mama watoto hufurahi sana anapokula chakula nilichokiandaa mimi,hata mtoto wangu hufurahi sana anapokula chakula nilichokiandaa na hupenda kila wakati niwe naandaa(napika chakula)..so sioni tatizo lolote la mwanaume kupika chakula...Kwa wanandoa(au wapenzi) wenye mapenzi ya kweli kusaidiana kupika si kitu cha ajabu na wala si limbwata...ni zaidi ya mapenzi....Kama kweli unampenda utamlinda(na kumpikia mara moja moja)...hahaaaaaa
 
Kakangu kule juu......

tehe tehe lakini ASENI WENGA amefulia mkuu
samahani kama nimekukwaza.
 
Back
Top Bottom