Wanaume kupika na kupakua ni ushamba jamani??

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,720
21,779
Embu tuabarishane jamani

nimeenda kwa shoga yangu nikiwa na rafiki yangu mmoja
aakashangaa gafula binti yuko sebulen akasiki sauti
shemeji umekuja karibu yakhe...leo nimeingia mwenyewe
kwenye mtalimbo!!!watu wakacheka wenye kuhisi mtalimbo mwingine
gafra tukaingia tukakuta mwanaume anausukuma ugali kana ana akili nzuri jamani kuna watu wana bahati nyie..kurudi sebulen mwana ume yule akatenga chakula amemaliza tukaagana njian best anauliza hivi rafiki yako kalipata wapi lile shamba wallahi....
Nikasema kweli wengine tunawatafuta wengine wanaikimbia

nkasea jamani labda sijui kwangu nikaona normal...ila mwanaume kupika ushamba???
 
Msiposaidiwa shida, mkisaidiwa shida na mnatuona washamba na labda tumeshalambishwa limbwata! sijui tukimbilie kambi gani! Labda njemba hapendi ugali unaopikwa na mkewe.....just thinking aloud :)
 
Ni kweli kabisa

kuna watu awajui mapenzi ni kushhirikiana lakini wengine wanaamini ushirikiano vitandani tu..hapa ndipo kosa kubwa!!!!
Tusaidiane kila department jamani sio cfo,ceo wewe cio wengine no..wote tuwe kitu kimja na i can imagine jamani mwanamke wa aina hiyo anavyofurah moyon mwake...hapo utakuta ata limbwata ajawekewewa akiwekewa???
Braaaa braaaaaa
 
INATEGEMEA,mwanamme anaweza kupika kutokana na sababu zifuatazo;
1.Mkewe anaumwa
2.Kazi ni nyingi sana hivyo inabidi mme asaidie,
3.Mwanamke hana ujuzi sana wa mapishi,hivyo mwanamme atajifanya kumsaidia,lakini lengo
ni kumuelekeza anataka chakula kipikweje.
4.Wapo wanaume wanaopenda mambo ya kike,kike,kike,kike, kila shughuli waifanyao
akina mama nao wanatamani, si ajabu ukakuta kavaa khanga ya mkewe kutwa nzima
5. Wapo wanaume wenye huruma ya hali ya juu,hivyo wanasaidia tu
6. Upendo nao ukizidi sana sana sana ndio hivyo tena
7. Limbwata likikolea sawasawa atapika,atafua nguo,ataosha vyombo,hata gesti atakusindikiza
(naomba usiniulize limbwata ninini hata mimi huwa nalisikia tu)
 
TALL
naomba usiniulize limbwata ninini hata mimi huwa nalisikia tu)

KWA MALEZO YAKO NA MTITIRIKO

WE USHALINYWA TUPE TU LADHA YAKE ZAIDI KUNA MENGINE UMEFICHA NJE YA HAPO JUU.............ILA ALIKUTESA
 
Kama mwanamke anahitaji "ukombozi" basi adui wa huo ukombozi ni wanawake haohao
 
kupika inategemea, lakini kama kuna wageni sio ustaarabu dume likaingia jikoni na kuandaa chakula cha wote
 
hakuna tatizo kumsaidia mamaa mambo ya jikoni....tunachoogopa ni maneno yenu kina mama..hamkawii kutuona mume ***** kisa tu tumewasaidieni kupika...
 
wakuu suala la kupika kwa wanaume ni zaidi ya mapenzi au kuwa mume *****; wanaume naturally ni wapishi wazuri sana na ndio maana hoteli nyingi chefs wengi ni wanaume.

kupika ni art kama vile sanaa nyingine na kusema kweli kipaji kile hakiigiki,

wanaume wengi waliolelewa vizuri hujua kupika na huweza kupika, pia wanaume waliowahi kuishi mabachelor au colleges mara nyingi wamekua wanapika

Now back to family issues
Mwanaume anayepika mara nyingi huwa na kipaji au uwezo wa kuwa karibu pia hata na watoto na mamaa. zaidi ya hayo, mwanaume anayepika is naturally romantic, more helpful, loved by kids na pia inaonyesha ana muda wa kufanya mazuri kwa mke na watoto

Moreover, kupika tu ni fun kinoma

TO ANSWER THE QUESTION, MWANAUME KUPIKA SIO USHAMBA
 
Tena kumheshimu sana BJ. Haya Hongera kwa ushindi mkubwa wa jana. Naona SAF aliamua kumpumzisha star wenu jana.

Acha tu, mana ukimkebehi msaada unasitishwa!..Nikipata wa namna hiyo nitafurahi hata kama majukumu ya ndani nayamiliki vzr.
Oh! thanx,yani ilibidi star Rooney apumue asijeruhiwe zaidi mana bado kuna mechi ngumu zinakuja!..Nilisikitika mlivyodroo, ilikuwa mshinde eniwei ndo kandanda!..
 
Kabisa BJ..halafu wengine husahau kwamba huo ni msaada tu na kudhani ni wajibu wa mwenzie na hapo ndipo njemba husimamisha msaada wake. Ahsante sana BJ tumepoteza opportunity nzuri sana jana ya kukaa bega kwa bega na miamba wawili wa soka UK. Jamaa baada ya kujifunga goli tu basi nikahisi Rooney asingecheza maana sasa hivi huja kuokoa jahazi kuanzia dkk ya 55 na kuendelea kama bado ni 0-0. Mchapo wa J`mosi nausubiri kwa hamu kuu I hope itakuwa mechi nzuri sana na siyo midebwedo kama ile ya MANU na L`pool. Matokeo ambayo mimi niyafurahia zaidi ni 0-0 ili kuisaidia timu yangu :) si unajua tena mvuta kamba....... Haya J`pili njema...usipotee kiasi hicho jamani hasa kule kwenye soka. Tangu utoke likizo umeadimika kama shilingi ya Kenya ;)
 
Mama mia mie nimeshapika sana tu lkn tulipokuwa mimi na yeye na mtoto wetu akiwa na mwezi mmoja mpaka sita beki 3 wetu alikula kona mapema kukimbia kazi, ilikuwa nikitoka job, nakuta nguo za mtoto, nepi nafua nazianika nje, kid akiamka ntamsaidia kumbembeleza kwa kweli hiyo kitu imenitengenezea uaminifu na upendo mkubwa sana na ukaribu wa hali ya juu, tunaishi km marafiki hakuna ubaba flani hivi wa kizamani, kweli very enjoyable.
 
BAK, kuna njemba nyingine kwenye mambo ya maakuli ni balaa..unatamani kila siku akaangize, ha ha ha
Inshalaah,jmosi tushinde kama Ze Blue hawatatuzibia!..Siku hizi kila mshabiki anaombea timu pinzani ifungwe,lol!..Na nyie kazeni kamba ila manu taifa kubwa!....sipotei tena pal, si unaelewa mikiki ya maisha na kujipanga ukizingatia 2010 ina mambo mengi!..j2 njema too!!
 
endelea kuwa na upendo huo kaka wa kumsaidia mkeo,wewe ni mfano wa mwanaume bora.
 
BAK, kuna njemba nyingine kwenye mambo ya maakuli ni balaa..unatamani kila siku akaangize, ha ha ha
Inshalaah,jmosi tushinde kama Ze Blue hawatatuzibia!..Siku hizi kila mshabiki anaombea timu pinzani ifungwe,lol!..Na nyie kazeni kamba ila manu taifa kubwa!....sipotei tena pal, si unaelewa mikiki ya maisha na kujipanga ukizingatia 2010 ina mambo mengi!..j2 njema too!!

Ni kweli kabisa BJ kuna njembas nyingine zinajua kukaangiza vibaya sana. Niliwahi kualikwa kwa Wabongo (mke na mume) basi Baba mwenye nyumba ndiyo alikaangiza siku hiyo...we acha tu maana msosi ulikuwa bab kubwa! Sawa jipange vyema BJ ni kweli 2010 ina mambo mengi sana. Kila la heri. Jumamosi sitaki nyie mshinde wala Chelsea washindi na sare iwe ya 0-0 si unajua mshindi mwaka huu anaweza kuwa kwa tofauti ya magoli tu? Haya kwaheri.
 
Mie pia nina rafiki yangu ameolewa, mara kadhaa nikienda kwao kwa dinner unakuta mume yupo jikoni tena amepachika kwa juu na ile nguo special ya kupikia na msosi mtamu..of course wanasaidiana na majukumu mengine,raha sana maisha yale kama heshima haipotei!..mwingine hata kutoa chombo mezani hatoi acha kuosha,huh!.
Asante, tutazidi habarishana via sport page yetu kuhusu huo mpambano ujao!..Naona umekamia sana 0-0,na iwe ila mie nataka ushindi tuongeze magoli na points ha ha...bye 4 now!
 
Back
Top Bottom