Wanaume kupigana kisa mapenzi ni ushamba

Wanaume kupigana kisa mapenzi ni ushamba

The redemeer

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2025
Posts
4,780
Reaction score
8,155
Kama ulikua hujui kuwa wanaume KUPIGANIA mwanamke huo ni USHAMBA wacha nikufahamishe;-
Wanaume wengi huishia pabaya kisa wanawake,
Na hasa wale wanaume ambao humpenda demu,
Kiasi ambacho anafika kupigana na wanaume wenzie kisa demu,
Labda nikwambie tu kwamba katika dunia hii,
Hakuna kitu cha kipumbavu kama mwanaume kupigana na mwanaume mwenzie kisa mwanamke,
Hiki ni kitendo cha kijinga sana na kilishapitwa na wakati,
Kwani mwanaume kamili hawezi kupigana na mwanaume mwenzie kisa demu,
Huenda usinielewe leo lakini ipo siku utakuja kunielewa,
Kwani ni kweli kusalitiwa kunauma tena sana,
Lakini mwenye kosa kwenye hilo ni mwanamke wako siyo mwanaume,
Kwasababu yeye ndie anaetakiwa kujitunza na kujiheshimu,
Mwanaume hana kosa kwasababu mwanaume kutongoza ndiyo asili yake,
Na mwanamke kutongozwa ndiyo asili yake,
Ila kukubali au kukataa ndiyo maamuzi yake,
Kwahiyo kama mwanamke anajitambua yupo na mtu,
Lazima atakataa ili kumpa heshima mumewe au mwanaume wake,
Lakini mwanamke asie jitambua ndiyo atakubali na kuliwaliwa hovyo nje,
Licha ya kuwa anajua kuwa ana mwanaume wake,
Yeye ndiye mwenye kosa na siyo mwanaume,
Kwahiyo unachotakiwa kufanya dili na mwanamke,
Usidili na mwanaume mwenzako hilo ni kosa kubwa sana kwasababu,
Mungu alishasema tuishi nao kwa akili hawa viumbe,
Najinsi ya kuishi na mwanamke aliekuacha kwa akili ni kufanya uwamuzi mmoja tu,
Nao siyo mwengine ni uwamuzi wa kumuacha basi,
Hapo ndiyo utakua umetimiza uanaume wako,
Na utakua umetimiza agizo la mungu la kuishi nae kwa akili,
Yani usimtukane wala kumpiga utakuja kupata kesi bure ya mauaji,
Mwanaume anaejitambua hapigi mwanamke wala kumtukana,
Bali mwanaume kamili hufanya maamuzi ya kiume,
Na maamuzi ya kiume hapa ni kumuacha basi,
Hiyo ndiyo dawa sahihi ya mwanamke msaliti,
Nasiyo kupigana na mwanaume mwenzio,
Au kumpiga mwanamke huo ni upumbavu,
Na ukifanya hivyo yaani amekusaliti ukaamua kumuacha,
Bila kumpiga popote na bila kumtukana na bila,
Kugombana na yule mwanaume aliefanya nae uchafu wa kukusaliti,
Nakuhakikishia huyo mwanamke baada ya wewe kumuacha,
Lazima ataachwa na yule mwanaume aliekusaliti nae,
Haki ya mungu nakuhakikishia penzi lao haliwezi kudumu lazima wataachana tu,
Unajua kwanini ni lazima hao watu wataachana,
Ni kwasababu mwanaume kutwa atakua anajiuliza kuwa,
Kama huyu mwanamke amemuacha bwana wake au mume wake amekuja kwangu,
Ni lazima na mimi ataniacha tu akipata mwanaume mwengine,
Kwasababu kuwa nae yeye haimaanishi kuwa hatotongozwa tena,
Kwahiyo hili swali wanaume waliopora wanawake za watu,
Huwa wanajiuliza sana tena waliopora wanawake za watu,
Halafu mwanaume mwenye huyo mwanamke,
Akaamua kumuacha mwanamke wake kimya kimya bila kumpiga mwanamke wala kumtukana,
Na bila kugombana na mwanaume mwenzake au kupigana nae,
Ndiyo kabisaaaaa ndiyo maana nimekwambia,
Katika maisha yako mwanaume usipigane na mwanaume mwenzio kisa demu,
Ukifanya hivyo utamfanya huyo aonekane wathamani sana,
Hivyo hawata achana hao watu ila ukiachana nae kwa amani lazima wataachana,
Kwanza kwa kipindi watakacho kuwa pamoja,
Muda mwingi sana watakua wanakuzumzia,
Na hiyo hali ndiyo itakayo kuwa inamtesa sana mwanaume,
Kumnyima raha kabisa kabisa mwanaume,
Mwisho wa siku lazima wataacha tu huo ndiyo ukweli,
Yani hata wewe hapo msomaji wangu ukimpora mwanamke wa mtu,
Huwezi kumuoa yani lazima mutaachana,
Tena kama ni mke wa mtu ndiyo kabisaaaaa.
ACHENI USHAMBA PIGANIA MAISHA NA .......

Makala hii imeletwa kwenu na Dhulkad Madara kutoka Morogoro
 
Back
Top Bottom