Wanaume kama Mabinti | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanaume kama Mabinti

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Regia Mtema, Feb 23, 2010.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #1
  Feb 23, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Jana nilikuwa napita karibu na bar fulani,nikasikia wimbo wa Jide wa Wanaume kama mabinti ukanikumbusha mbali.Nikatafakari sana na baadaye nikaja kugundua kuwa Lady Jaydee ameimba kitu cha ukweli mtupu.Mapenzi ya siku hizi yameshuka sana,si wanaume si wanawake hatuoi wala kuolewa bila kuweka vigezo kwa yule unayetaka kuwa naye.Wanaume wa siku hizi utasikia mimi mchumba wangu au mke wangu lazima awe na kazi,elimu kuanzia kidato cha sita na kuendelea na vigezo vingien ,wengine wanaangalia hata uwezo wa wazazi wako.Jamni haya mambo yametokea wapi?Mbona hayakuwepo zamani na wazazi au babu zetu walifaidi maisha ya ndoa tena kuliko sasa kila kukicha watu wanalia ooh ndoa,imenichosha n.kZaidi ya hayo ndoa nyingi siku hizi zinavunjika uklinganisha na miaka ya zamani.Hivi ninyi wanawake na wanaume mnaoweka vigezo je mnaoa ama kuolewa na vigezo au mtu?je vigezo hivi tunavyoweka vinongeza nini katika maisha ya ndoa?na je vingekuwa na maana mbona ndoa za siku hizi nyingi zao hazina mvuto?kila siku kufumaniana,kama sio laivu basi kwenye simu n.k.Jamani hebu tuache mapenzi yachukue mkondo wake,tusiilazimishe mioyo yetu ijifunze kupenda kwasababu tu ya kuangalia vigezo,tukumbuke mioyo huwa haijifunzi badala yake ina penda yenyewe kwa kuamua yenyewe.
   
 2. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #2
  Feb 23, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  umenena mkuu .......................

  siku hizi kuna "deals" hakuna mapenzi. unakuta mtu anajiuliza kama hakuna mapenzi, kwa nini uoe mtu mzigo, akutegemee kwa kila kitu na atake uwatunze na wazazi wake na mahari ulishatoa, usomeshe ndugu zake etc. ndo maana wanaume wa siku hizoi wanasisitiza mke aliyeenda shule japo kidogo na mwenye kazi ili asimlemee sana kwani suala la mapenzi linaelekea kusahaulika........................

  hebu fikiria uoe mke darasa la saba, alikuwa akikuamkia shikamoo kabla, ulipomuoa anajiona sawa na wewe, anataka nawe umpelekee maji bafuni, ukibisha jamii nakuona umepitwa na wakati!!!!! sasa si bora uchukue libishi na huku ukijua ni libishi na wala hujihangaishi kuliomba likuwekee maji bafuni, unabeba mwenyewe mpaka Mungu akujaalie kujenga nyumba yenye shower ndani, hata ukichekwa, umesevu mizigo, hata mkiachana likadai mali pari-pasu na lenyewe lilichangia......................
   
 3. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #3
  Feb 23, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Do you think kwa hali hii utafaidi mapenzi ya kutoka moyoni?
   
 4. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #4
  Feb 23, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  hakuna kitu mzee, hayo ya kutoka moyoni itabidi tu tukubali matokeo,.............tuyasahau kabisa, lbda uokote Mungu akikujaalia emtu exceptional .............though its very rare!!!!!!!!!!!!!!!
   
 5. Mtoto wa Kishua

  Mtoto wa Kishua JF-Expert Member

  #5
  Feb 23, 2010
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 827
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 45
  Ndio yale yale , Mzee ana fariki watoto wana teseka sababu Mzee kaoa mke darasa la saba au asiye na kazi sababu ya mapenzi toka moyoni.
  Dunia ya sasa ni muhimu kuangalia future ya fammilia, mambo ya kuoa demu asiye na mchago wowote zaidi ya kukupa undoa na kuku pikia vizuri yame pitwa na wakati, sasa himu umuhimu ni jinzi ya kuendesha fammilia na mna ya kuhakikisha mchango wa kiuchumi unaletwa na wote baba na mama, ili mmoja akipotea mwingine ana weza kuendeleza hali nzuri ya maisha na fammilia haita tetereka , haya yatapatikanaje kamaunaokota kitu eti umekipenda na ni just mama wa nyumbani ?
   
 6. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #6
  Feb 23, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  tatizo mnajidai kuwa mnaweza kumpangia Mungu ratiba ya kazi zake za kila siku, ndio maana hamuwezi ku-enjoy ndoa milele................
   
 7. Bazazi

  Bazazi JF-Expert Member

  #7
  Feb 23, 2010
  Joined: Aug 18, 2008
  Messages: 2,160
  Likes Received: 915
  Trophy Points: 280
  Swali kuntu, swali lililokwenda shule; haya wadau changieni hoja
   
 8. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #8
  Feb 23, 2010
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,581
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 145
  .........Sasa kama hamtaki kuoa mke wa darasa la saba, ataolewa na nani?

  Mbona zamani kuna wanaume wenye elimu zao walioa wanawake wa darasa la saba na kuwaendeleza kielimu. Mapenzi hayachagui usomi, na hayo ndio mapenzi ya kweli..........ukioa mwanamke darasa la saba halafu ukimsomesha kwani kuna ubaya? Baadaye si atakuja kusaidia watoto wenu kama mwanaume haupo!!
   
 9. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #9
  Feb 23, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 37,735
  Likes Received: 9,245
  Trophy Points: 280
  Wanawake wanalilia usawa sana, wakipewa usawa wenyewe huu wanalalamika.
   
 10. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #10
  Feb 24, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Sidhani kama usawa wanaoulilia wanawake ni huu.
   
 11. Noname

  Noname JF-Expert Member

  #11
  Feb 24, 2010
  Joined: Feb 8, 2010
  Messages: 1,269
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  kwani akiwa kasoma darasa la saba ndio hayuko sawa na wewe or you should treat her like shit? then u expect to have a happy life :rolleyes: Thanks GOD i wasnt born in that time where I have to carry heavy things ... yani nyie mliwanyanyasa sana wanawake...
   
 12. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #12
  Feb 24, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 14,794
  Likes Received: 1,431
  Trophy Points: 280
  hahahahaaaa! unenena mkuu! anibebee maji kwani alinikuta sina mikono? anifulie kwani alikuta navaa nguo chafu? anipikie kwani alikuta nakula unga au mchele kama panya?
  Alaaaaa!!
   
 13. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #13
  Feb 24, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 14,794
  Likes Received: 1,431
  Trophy Points: 280
  weeee!! nani anabeba? house girl sio? au unaishi dawasco, maji hayakatiki? huendi sokoni? hutoi vitu kwenye gari kama unalo? Mimba je? sio kitu kizito, au jamaa ndo anabeba
   
 14. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #14
  Feb 24, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Unayafanya haya ua unajishaua tu?
   
 15. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #15
  Feb 24, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 14,794
  Likes Received: 1,431
  Trophy Points: 280
  Umekosea kidogo, uliza utafanya?
   
 16. Noname

  Noname JF-Expert Member

  #16
  Feb 24, 2010
  Joined: Feb 8, 2010
  Messages: 1,269
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  maji hayakatiki... tunaenda wote store.. he is the one who push the trolly.. sitoe kitu kwenye gari.. my husband is a gentleman he dont allow me to do that...

  mimba ntabeba mie but thats something else... sio ndoo ya maji:rolleyes:
   
 17. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #17
  Feb 24, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Ok,je utayafanya hayo uliyoyasema Mkuu?
   
 18. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #18
  Feb 24, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,845
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 0
  mwanamme anataka kulishwa, kuvishwa na pia kutumikiwa kama mkewe ni mama wa nyumbani hana kazi vile!

  kweli dunia ya mwisho hii, mwanamme ndo anapiganiwa na sio kinyume chake! agggr

  maji nitamuwekea bafuni kwa mapenzi tu sio kuwa ni wajibu wangu............nafikiri nae hatojali maana alijua anaoa akina wale "wabishi"
   
 19. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #19
  Feb 24, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 368
  Trophy Points: 180
  Hivi unaoa Mwenzi ama MJENZI?

  Kama unaoa mwenzi hata akiwa Darasa la Saba mtayafanya sawa na yule wa Chuo kikuu! Ni mipango na kupendana kati yenu wawili! Sawa atakupeleka maji bafuni lakini nawe si unakatia hiyo michongoma kwenye fence? Na mkiwa na upendo hata kazi kati yenu zinajibalance hakuna kutegeana!

  Ila kama nia yako ni mjenzi ndo hapo utaishia kupiga percentage ya mshara wake inatumika kiasi gani! Na katu hutojua kupendwa toka moyoni na hakika you die lonely!
   
 20. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #20
  Feb 24, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 14,794
  Likes Received: 1,431
  Trophy Points: 280
  Nitafanya, tena the lions share.
   
Thread Status:
Not open for further replies.
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...