Wanaume huwa hawaonji mara moja……………………..!

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,806
15,379
slide-214-378x335.jpg

Ni kama "Unga" ukimbwia, utabwia tena..........................

Watafiti na wataalamu wengi wa masuala ya uhusiano wanakiri sasa kwamba, mwanaume akishatoka nje mara moja kwenye uhusiano wake, atatoka tena na tena. Kwa hiyo kama mwanamke amemfumania mpenzi wake au mumewe, basi ajue kwamba upo uwezekano mkubwa sana wa bwana huyo kumsaliti tena. Kutoka mara moja na kuacha siyo kawaida ya wanaume, labda tu kama atajifunza soma kubwa sana baada ya kutoka mara moja.

Lakini mbaya zaidi, inaelezwa kwamba, akihama uhusiano, yaani kama ametoka kwenye uhusiano na kuanzisha mwingine, uwezekano wa kutoka tena nje, unakuwa mkubwa zaidi. Wakati mwingine ni vigumu kuamini hivyo, lakini ndivyo ilivyo. Tumezoea kwamba, mtu akiungua mara moja, huogopa kucheza na moto, lakini kwenye suala la kutoka nje, kuna ukweli kwamba, kwa kadiri anavyotoka nje, ndivyo mwanaume anavyotaka kutoka tena na tena.

Kwa nini mwanaume anapotoka nje, inakuwa kama vile ni lazima arudie tena jambo hilo?

Mwanaume hatoki nje kwa sababu hampendi mkewe, hapana. Mwanaume hutoka nje kwa sababu ya tamaa ya mwili. Kwa hiyo, kama ameoa na akashindwa kuheshimu ndoa yake kwa kuongozwa na tamaa, ni wazi kwamba, hatakuwa na uwezo mkubwa wa kudhibiti miito ya kimwili. Udhaifu huo utamfanya kutamani vingi na kutenda. Kama mwanaume ana uwezo wa kudhibiti mihemko yake na kuheshimu uhusiano wake na mkewe, ni vigumu kwake kutoka nje. Kama uwezo huo hana, atatoka na akishatoka mara moja, ataamini kwamba hana uwezo wa kudhibiti, hivyo kutoka mara ya pili na ya tatu na nne litakuwa ni jambo la kawaida kwake.

Kuna kutoka nje ambako kunatokana na mwanaume mwenyeqwe kuwa na matatizo ya kisaikolojia. Anatoka nje katika kujaribu kuukabili udhaifu wake. Kwa hiyo akitoka anabaini kwamba, udhaifu bado upo. Anaamini kwamba, mwanamke aliyetoka naye, hajaweza kumsaidia kupata anachokikosa, hivyo hutafuta mwingine. Hata hivyo inategemea ni sababu ipi inayomfanya mwanaume kutoka nje ya ndoa yake. Kama ni sababu ambayo inahusiana na uhusiano na mwenzake kuwa na matatizo, bado kuna uwezekano akatoka tena nje. Hii ni kwa sababu, kila uhusiano una matatizo yake, ambayo dawa yake ni kujadili na kupata ufumbuzi, siyo kutoka nje.

Mtu akigeuza kutoka nje kuwa ni dawa, atatoka kila uhusiano atakaoingia kwa sababu, atakuta matatizo kwenye kila uhusiano. Hakuna uhusiano wa kimalaika kumbuka………………………
 
kazi tunayo....lakini hii picha mkuu mhh...sidhani kama ni sawa sana kuiweka hapa...
 
kazi tunayo....lakini hii picha mkuu mhh...sidhani kama ni sawa sana kuiweka hapa...
Haya mkuu, nimekusikia na nimebadilisha hiyo picha, nadhani hii niliyoweka sasa ni nzuri zaidi.................................
 
Ni kama "Unga" ukimbwia, utabwia tena..........................

Mwanaume hatoki nje kwa sababu hampendi mkewe, hapana. Mwanaume hutoka nje kwa sababu ya tamaa ya mwili. Kwa hiyo, kama ameoa na akashindwa kuheshimu ndoa yake kwa kuongozwa na tamaa, ni wazi kwamba, hatakuwa na uwezo mkubwa wa kudhibiti miito ya kimwili. Udhaifu huo utamfanya kutamani vingi na kutenda. Kama mwanaume ana uwezo wa kudhibiti mihemko yake na kuheshimu uhusiano wake na mkewe, ni vigumu kwake kutoka nje. Kama uwezo huo hana, atatoka na akishatoka mara moja, ataamini kwamba hana uwezo wa kudhibiti, hivyo kutoka mara ya pili na ya tatu na nne litakuwa ni jambo la kawaida kwake.

Mtu akigeuza kutoka nje kuwa ni dawa, atatoka kila uhusiano atakaoingia kwa sababu, atakuta matatizo kwenye kila uhusiano. Hakuna uhusiano wa kimalaika kumbuka………………………

Hapo kwenye bold kuna kweli, tamaa ya mwili huchangia kwa kiasi kikubwa! Lakini tukumbuke pia si wanaume tu wanaotoka nje, wapo wanawake pia ambao kimsingi wao hutoka nje kwa tamaa ya vitu!!!

Mtu yoyote akianza kutoka nje, huwa haachi kirahisi, ni sawa na kula nyama ya mtu au kumtafuna mkuu wa meza, ukionja huwezi kuacha kamwe!!!
 
kwa nini watu wanaoa/kuolewa wakati wanajua kabisa hawapo tayari kiji-commit kwa partners wao??sielewagi mwenzenu..
kama tamaa wote tunazo,vishawishi pia vipo..lakini are we trying our best kweli??
 
Napale mkeo anatembea na your best friend hapo imekaaje ?

Sent from my BlackBerry 9360 using JamiiForums
 
dah!! mkuu Mtambuzi kamwaga mchele kwa kuku mitetea.. ..leta na upande wa pili basi mkuu:loco:
 
Last edited by a moderator:
Hivi kuna mwanaume anayeweza kukaa kwenye ndoa yake kwa kipindi chote cha uhai wake bila kumchit mke wake hata siku moja??siamini kama wapo!!
Mie sijawahi kum-cheat mama Ngina, lakini naogopa nikisema kwa sauti hapa kina dada wakware humu wakisikia watanitega ili kunitia ibilisi nifanye kweli, ili wapate la kusema..................

young-aa-couple.jpg
 
hongera sana!! mama Ngina must be very proud of you aisee uwe unawapa wanaume tuisheni humu wajue jinsi ya kukabiliana na hiyo changamoto.
 
11 Reactions
Reply
Back
Top Bottom