Wanaume, huu si uungwana hata kidogo

Wanaume, huu si uungwana hata kidogo

Khantwe

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2012
Posts
59,468
Reaction score
119,632
Habari za asubuhi.

Naomba niende moja kwa moja kwenye lengo langu.

Kuna baadhi ya wanaume wana tabia ambayo mimi binafsi sipendezwi nayo kwa hakika. Mwanaume anakuwa anathamini watoto kuliko mke wake aliyemzalia hao watoto. Sisemi msiwapende watoto wenu ila mjitahidi kubalansi.

Utaona mtu yuko bize na watoto tu, weekend anachukua watoto anawatoa out,kama ni zawadi wanapata watoto tu.

Hata akiweka picha facebook ni kuweka watoto mwanzo mwisho, huoni hata siku moja kaweka picha ya mkewe au walau aweke wanae pamoja na mama yao. Niliwahi kuona mtu ameweka picha facebook eti 'bon voyage my daughter' nikajiuliza hivi huyu mtoto wa mwaka mmoja anasafiri hadi
Mwanza peke yake? Hata ukiangalia kwenye visimu vyao vya tochi huoni picha ya mkewe hata moja.

Hivi kuna sababu zozote za msingi zinazowafanya muwe hivyo? Huyo mwanamke ndiye aliyewaweka tumboni miezi tisa hao watoto unaojivunia, akaenda leba na hatimaye na wewe ukapata cha kujisifia mbele ya wanaume wenzio.

Hivi bado hamjui kuwa kuna wanawake wanatoa mimba? Au hamjui kuwa kuna watu walichezea ujana wao hadi leo hawana uwezo wa kushika mimba? (siwazungumzii wale wenye matatizo ya uzazi yaliyotokea kwa bahati mbaya)

Sasa kinachokufanya usimthamini huyu mwanamke ni nini?

Huyo ndo mkeo...ulimchagua kati ya maelfu uliowaona...na hayo matunda unayoringia umeyapata kupitia yeye. Mthamini mkeo.

Be proud of her.
Ni hayo tu
NB:
Sisemi muweke picha zao ziwe profile picture.....ile kuonekana mnajali uwepo wao japo mara mojamoja inapendeza
 
Haya MTETEZI wa HAKI za WAKE....Ngoja waje wataalam watueleweshe🙂
 
Kwikwikwiiii...!! Mke ni mke na watoto ni watoto!! Nikuweke kwenye social networks kwani sikupendi?? Vidume wana tabia ukimsifia sifia sana mkeo wanaanza kufatilia na kumtongoza kwa nguvu zote ili wajue tu unachokipenda mule!!

Ili kuepusha hayo sijiweki wala sikuweki kwenye social networks ili tubaki salama daima wacha watoto wajidai!!
 
watakumwagia tindikali mke mwenza.. Ntuzu njoo utoe maelezo hapa
 
Last edited by a moderator:
Kwikwikwiiii...!! Mke ni mke na watoto ni watoto!! Nikuweke kwenye social networks kwani sikupendi?? Vidume wana tabia ukimsifia sifia sana mkeo wanaanza kufatilia na kumtongoza kwa nguvu zote ili wajue tu unachokipenda mule!!

Ili kuepusha hayo sijiweki wala sikuweki kwenye social networks ili tubaki salama daima wacha watoto wajidai!!

Huko ni kutojiamini.....mbona na yeye ana account fb na instagram na anaweka picha? Watongozaji huko hawamuoni? Kwanza wanaanzaje kumtafuta....ina maana unapoweka picha yake unaweka na namba ya simu?
 
Back
Top Bottom