Wanaume Bwana... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanaume Bwana...

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by MziziMkavu, Aug 19, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Aug 19, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Wanawake hao walikutana kiwandani na kuwa marafiki kabla ya kugundua kuwa wameolewa na mume mmoja Tuesday, August 18, 2009 3:01 PM
  Wanawake wawili wa nchini China ambao waligeuka kuwa marafiki baada ya kuanza kazi kwenye kiwanda kimoja, walipigwa na butwaa kugundua kuwa wote wawili walikuwa wameolewa kwa mume mmoja na wote wamezaa naye mtoto mmoja. Bwana Cui Bin, 42, mkazi wa Zhengzhou, amehukumiwa kwenda jela miezi mitatu kwa kufunga ndoa na wanawake wawili bila wanawake hao kujua, limeripoti gazeti la Dahe Daily.

  Bin alimuoa kwanza Zhang Dandan na kufanikiwa kupata mtoto wa kike lakini Bin alikuwa na hamu sana ya kupata mtoto wa kiume.

  "Nilitaka siku zote niwe na mtoto wa kiume, lakini kutokana na sheria za China zinazoitaka kila familia kuwa na mtoto mmoja tu ilinibidi nitafute mwanamke mwingine wa siri" alikiri Bin.

  Baada ya kuona amepata mtoto wa kike kwa mke wake wa kwanza, Bin aliamua kumuoa mwanamke mwingine aliyeitwa Wang Na na kufanikiwa kuzaa naye mtoto wa kiume.

  Bin aliugawanya muda wake kwa wake zake wote wawili huku akitumia sababu mbali mbali wakati alipokuwa akitoka kwa mke mmoja kwenda kwa mwingine.

  Wakati huo huo Zhang na Wang walikutana kazini na kugeuka kuwa marafiki kutokana na kupenda kuimba miziki ya Karaoke, hawakuwahi hata siku moja kufikiria kwamba walikuwa wameolewa na mume mmoja.

  Wang alikuwa akijua kuwa mume wa rafiki yake alikuwa anafanya kazi za ujenzi mji mwingine.

  Zhang naye kwa upande wake alikuwa akijua kuwa Wang alikuwa ameolewa hivi karibuni lakini hakuwahi kumtembelea nyumbani kwake.

  Ukweli wa mambo uliibuka wakati Wang alipoanza kuhisi mume wake ana kimada nje baada ya kumsikia mumewe akiongea na mwanamke mwingine kwenye simu.

  Wang alichukua simu ya mumewe na kuipiga namba ya mwisho kupigwa na ndipo alipopigwa na butwaa akibaki haamini kuwa alikuwa akiongea na mke mwenza.

  "Nilipiga namba ya mwisho kwenye simu yake na mwanamke alinijibu kwa kusema kuwa yeye ni mke wa Bin, kwakuwa tulikuwa tukijuana kwa sauti, moja kwa moja tulijuana" alisema Wang.

  Bwana Bin anaendelea kutumikia kifungo chake cha miezi mitatu. http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsId=2846694&&Cat=7
   
 2. B

  Boney E.M. JF-Expert Member

  #2
  Aug 19, 2009
  Joined: Jan 22, 2007
  Messages: 425
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Na wao watakosa matunzo kutoka kwa mzee....
   
Loading...