Wanaume Andikeni "Wosia" mapema

Wanaume Andikeni "Wosia" mapema

Jenerali Ambamba

JF-Expert Member
Joined
Sep 8, 2014
Posts
3,344
Reaction score
2,537
Kuna Kisa kimoja nataka niwashirikishe.

Mkabala na Nyumba niliyohamia hivi karibuni baba mwenye nyumba alifariki dunia, baba huyu aliacha mke na watoto kadhaa, aliacha na mali zikiwemo Nyumba, sasa huyu baba ni mjita na mke wake ni mkerewe, Mama huyu baada ya mume kufariki ndugu walikuja na kugawa urithi kwa "watoto", wa marehemu, mama yao akapewa chumba kimoja tu, na watoto wakapewa chumba kimoja kimoja katika nyumba hyo, Nyumba ina vyumba 6, kila mtoto alipewa chumba kimoja na mama yao akapewa chumba kimoja, sasa watoto wamishaoa, na kuolewa lakini vyumba vyao wamepangisha wapangaji, na pesa zinazopatikana kwa kupangisha mama yao anawatumia huko walipo, Sasa unakuta kwa mfano nyumba au choo/bafu linahitaji ukarabati, pesa za kufanyia ukarabati hakuna, mama yao anaishi maisha ya shida, na anasema kuwa hizo ndo mila za wajita!! ebo.


Hivi kuna aja gani ya kugawa urithi kwa watoto wakati mzazi mmoja bado yu hai?

Vijana ambao hadi tunaoa bado tunang'ang'ania urithi wa wazazi wetu ni sahihi?

Kwa nini wanaume hata wanawake tusiandae wosia mapema hata wa mdomo tu?
 
Habar za mirathi hizi jaman ni pasua kichwa
 
Swala la urithi ni kweli arithi baba au mama je ni vyema baba arithi mali ya mkewe alefu atumie kwa wanawake wengine au mama alithi mali ya mmewe atumie kwa wanaume wengine watoto warithi mali ya MZAZI wao MZAZI atunzwe na watoto wake kosa hapo watoto hawatunzi MZAZI wao wapumbavu
 
Swala la urithi ni kweli arithi baba au mama je ni vyema baba arithi mali ya mkewe alefu atumie kwa wanawake wengine au mama alithi mali ya mmewe atumie kwa wanaume wengine watoto warithi mali ya MZAZI wao MZAZI atunzwe na watoto wake kosa hapo watoto hawatunzi MZAZI wao wapumbavu

yeah! this is right , mambo ya mila kwa kweli yatupiliwe mbali, na watoto lazima tuwe na akili ya kujitambua basi, unadhani usipomtunza mzazi wako nani akusaidie kumtunza?
 
Mwanamke akijua umeacha wosia WA kummilikisha Mali zote, ataingia tamaa ya kukutanguliza mbele za haki.

Labda kama sio mmachame, na sasa imeenea kwa makabila mengi .
Nikifa mke wangu achukue vitu vya jikoni vyote na vya chumbani kwetu.

ha ha ha ha mimi sitaki hizi shida mume wangu anijengee nyumba kwa jina langu ndugue wakija kuchukua mali za jina lake nipambane mpaka kufa
 
Mwanamke akijua umeacha wosia WA kummilikisha Mali zote, ataingia tamaa ya kukutanguliza mbele za haki.

Labda kama sio mmachame, na sasa imeenea kwa makabila mengi .
Nikifa mke wangu achukue vitu vya jikoni vyote na vya chumbani kwetu.

Inabidi tukiwa tunaandaa wosia tuwashirikishe kaka zetu wakubwa au baba wadogo, hawa wanawake hawatabiriki kabisa.
 
Nitalifikiria hilo. ila kwa haka kachaga kangu kakigundua nimesha sign wosia si katanichinja tu!!!!!!??

wosia sijauandika na kanavoninyemelea usipime!!!
Ukiwa na macho mawili usivae miwani.
 
ha ha ha ha mimi sitaki hizi shida mume wangu anijengee nyumba kwa jina langu ndugue wakija kuchukua mali za jina lake nipambane mpaka kufa

Jipange mnapokua hai kutegemea milasi ni kudumaza akili na kutafuta migogoro isio na sababu.

Watu wanatimba mahakamani kupapalikia milasi ata kaburi wanasahau kulimia loh! Binadamu sisi mungu atusaidie!.
 
Lakini kuna wanawake wanateseka sana baada ya waume zao kufa, kuna cases nyingi sana,ni tofauti na mwanamke aliyetangulia, mume hapati shida sana...halafu ndo ukute mwanamke ni mlokole au asiyependa makuu mbona atahangaika sana?
 
Wosia andika kwa wanao sawa ila mama akipata tatizo ni jukumu lao watoto kumtake care......
 
Ila ukifa ujue ushamaliza kazi yako hapa dunian na kimsingi huwezi tengenezea mtu yeyote maisha hapa dunian ili eti ukifa asiteseke.....Hakuna jema hata moja achia watoto urithi wa mali ukifa tu wanauza mali zote nadhan mifano ipo kibao....Wachia urithi mke wako baada ya wewe kufa atakutana na Manuu hapa nitamchanganya tutakula mali zako zote nkishamailiza namtema.....So take it easy na we ukifa umekufa tu kwan yanaoendelea mara baada ya vifo laiti marehemu wangepata wasaa wakufufuka walau dk 1 waone mali walizoacha zinavyotobolewa angekufa kwa mara ingine.
 
Mali arithi baba au mama na itakapotolea baba au mama anataka kuoa au kuolewa tena basi mali hizo zigawanywe kwa watoto kwanza ndiyo mambo mengine yaendelee
 
Naomba kuuliza, kwani mme au mke akifariki pasipokuwa na wosia, ni nani anayestahili kurithi mali? Kwani hakuna sheria ya mirathi inayo-define warithi wa mali?
 
Minadhani kuanzia mwanzo wakununua Mali Kama unae Mtoto bora umuandikie mapema...
 
Back
Top Bottom