LWITIKO LWITIKO
JF-Expert Member
- Jan 27, 2013
- 209
- 118
Kitanda hakizai haram ww hiyo ni fam yake lazima aheshimiwe tu.
siku ya leo nmealikwa kwenda kutatua ugomvi wa watu wapendanao sasa kwa kweli naona kama vile shida tu
jamaa rafiki yangu anamwanamke ambaye ndio mke mtarajiwa amejifungua mtoto wa kike cha kushangaza hajashirikishwa kuita jina la mtoto kashaangaa anapigiwa na shemeji yake kuwa mtoto tumemuita fulani sasa jamaa anajiuliza mbona mimi sijashirikishwa na mimba tumelea mwanzo mwisho jana kampigia mwanamke na kumwambia tuachane na wakati huo wiki ijao tunaenda kutoa poza kaniambia rafiki yangu nikamwambia apotezee tu jamaa hataki
hivi utaratibu wa kuita jina ukoje kwa mtoto
Hii kali kweli, kibongo bongo kitendo tu cha kumpa mimba binti yangu bila kumuoa kwangu mimi ni tusi sembuse kumtafuta ashiriki kutoa jina?
Kama ni jina la sifa may it will be ok, but to me hata kama alikuwa malkia au mfalme mwanangu ni lazima awe na jina lake pekee ambalo sisi wazazi tutaridhia. Wanangu wa kiume niliwachagulia majina na wa kike mama yao. Of course tunakuwa na options za majina, tunayajadili na kupatikana moja au mawili. Mfano kila mtoto wangu ana majina mawili mawili. Mfano John Bosco, Erick Xavery, Mary Rose, Mary Theresia, Mary Blessings, etc.Vp kama yana bahati! Hutaki abebe bahati zote.. Japo sikubaliani na urithishwaji wa majina ya babu/bibi/ndugu
utaratibu hauko hvyo mkuu. Baba wa mtoto anatakiwa ndiyo ampe jina au atoe idhin kwa mkewe au ndg yeyote atoe jina..... Hayo unayosema ww ni miongon mwa wanaume wachache wanaoburuzwa na wakwe zao ndio wanaweza kufanyiwa kama mawazo yako yanavyowaza, unaonesha kuwa ww hata dem akija kwako na ukamgonga leo halafu kesho akakwambia nina ujauzito wako na ww ukakubali
mkuu hii inanipa shaka kuna binti nimezaa nae ila japo hatuja owana plan nikwamba tutafunga ndoa.tatizo ni hilo jina nilimchagulia mwanangu jina la kislam na tukakubaliana tatizo yeye kamuita mtoto jina tofauti kabisa namuuliza lina maana gani anasema la mcheza mpira na kila nikimuomba cheti cha kuzaliwa mtoto lazima ugovi...smtime nahisi na pigwa mchangame najua kwa mila za kiafrika kama hujatoa mahari na hujaoa unakuwa huna mamlaka juu ya mtoto. Sasa jamaa yako hata posa hajapeleka anataka aanzishe vurugu. Halafu hapo anaoa mke au anaoa mtoto? Kama anaoa mke haina shida jina la mtoto atalibadilisha mbele ya safari!
Kama ni jina la sifa may it will be ok, but to me hata kama alikuwa malkia au mfalme mwanangu ni lazima awe na jina lake pekee ambalo sisi wazazi tutaridhia. Wanangu wa kiume niliwachagulia majina na wa kike mama yao. Of course tunakuwa na options za majina, tunayajadili na kupatikana moja au mawili. Mfano kila mtoto wangu ana majina mawili mawili. Mfano John Bosco, Erick Xavery, Mary Rose, Mary Theresia, Mary Blessings, etc.
Unajua kwenye mahusiano kuna pressure. Za chini kwa chini sasa linapotokea jambo dogo ndio watu hupata sababu ya kuonyeshana misuli au kutapika nyongo zaosiku ya leo nmealikwa kwenda kutatua ugomvi wa watu wapendanao sasa kwa kweli naona kama vile shida tu
jamaa rafiki yangu anamwanamke ambaye ndio mke mtarajiwa amejifungua mtoto wa kike cha kushangaza hajashirikishwa kuita jina la mtoto kashaangaa anapigiwa na shemeji yake kuwa mtoto tumemuita fulani sasa jamaa anajiuliza mbona mimi sijashirikishwa na mimba tumelea mwanzo mwisho jana kampigia mwanamke na kumwambia tuachane na wakati huo wiki ijao tunaenda kutoa poza kaniambia rafiki yangu nikamwambia apotezee tu jamaa hataki
hivi utaratibu wa kuita jina ukoje kwa mtoto
Kama alikuwa bado hajamuoa huyo mwanamke, hana haki ya kutoa jina ashirikishwe kutoa jina yeye kama nani?
huyo jamaa yako ni mtoto na hajakua......
na wala hakua na nia ya kuoa
Ameshiriki vipi kulea mimba
wakati binti bado anaishi na wazazi? Hata kishika uchumba (posa)
hajatoa? Ningekuwa mzazi wa huyo binti ningemweka lock-up huyo dogo kwa
kumlaghai binti yangu.
Hujanielewa kabisa mkuu
wangu, kwanza sina demu na kwa umri huu sina sababu ya kuwa naye na
kuzaa haramu nje. Lingine nimesema majina tunakubaliana mimi na mke
wangu, hakuna ndugu, wala mzazi aliyetusaidia kuzaa watoto na zaidi wa
kiume huwa nawachagulia majina options nyingi na mwishowe tunachagua
mawili na wa kike mke wangu anachagua options na tunakaa tunakubaliana
majina matatu official kwa ubatizo na cheti cha mtoto. Si eti kwamba eti
nachaguliwa ukweni, hakuna kitu kama hicho. Huyu jamaa mleta mada
inaonekana huwa hawako karibu na huyo aliyezaa naye!!! Ni matatizo ya
kuzaa watoto kabla ya ndoa!!! Mke kwa wazazi, kijana kwa wazazi!!! Sasa
hapo si unategemea kuchaguliwa jina tu na wajomba na maanti. Chunga
kuzaa kabla ya ndoa.
tulia wewe nyinyi ndio mnaokuja kuwa wazee nuks.kama jamaa alikuwa anatoa fedha ya matumizi huko ndio kulea mimba afterall jamaa hana haja ya kupanic coz mtoto kama ni wakwake atakuja tu siku hizi hakuna kugombania watoto.
ndugu yangu siyo kila mtu anapenda kuzaa nje ya ndoa na si vyema kumuita mtoto wa nje haram please.usiongee kwa kuwa hayajakukuta.