Wanasiasa wa Tanzania yetu wanatufundisha nini....?

comson

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
288
41
Ni kawaida kwa mtoto kujifunza kutoka kwa mkubwa wake (imitation) au kwa kuiga kutoka kwa yule ampendaye (modelling)...

Hv kwa hawa wanasiasa wetu tunajifunza nini...! Kwa mfano: Inashangaza kwa nchi kama tz kujadili na kuunda tume ya kujadili kurudishwa kwa chura wa kiwira... wakati nchi iko kwenye giza....

Mwanasiasa anashindwa kujibu hoja na kubaki bungeni anachekacheka tu bila ya sababu na hoja ajaitolea majibu ya kuridhisha..; ref: bajeti ya wizara ya katiba na sheria... LISSU V/S waziri wa sheria...yaani kajibu nothing kwa lissu na ana wasiwasi.....
 
Tatizo la viongozi wetu, hawaangalii uzito wa hoja, wao wanachoangalia ninani katoa hoja.
Hivyo basi hoja inaweza ikawa ya muhimu na maana kwa taifa lakini ikabezwa kwa sababu tu imetolewa na upinzani.
 
Wanatufundisha kuwa siasa si ngumu. Hazihitaj akili. Ukichoka unalala.
 
Liwasira na Komba wanataka kuleta hoja binafsi ya kuwepo na Sleeping allowance.
 
Kwamba usiogope kuiba kwani wakishtuka inaundwa tume kwanza. Ikishaleta ripoti hadi bunge likae, liijadili na mwisho unaambiwa "Jivue Gamba". Unaachia ngazi Unaenda kula vyako tratiiiibu.
 
Back
Top Bottom