Pakome
JF-Expert Member
- Dec 8, 2024
- 1,541
- 916
Ifike mahali kelele za kila siku ziishe
Too much is harmful
Wanasiasa tambueni kuwa Wananchi wanafuata maelekezo yenu
Mkisema nchi itulie basi itatulia
Mkisema iwake basi itawaka
Ninyi ndio wenye uamuzi wa mwisho kabla ya matokeo
Twendeni Mataifa makubwa tuone namna yametulia na yanafanya kazi bila kelele
Twendeni China tuone utulivu
Twendeni Japan tuone utulivu
Twendeni Ujerumani tuone utulivu
Wananchi wametulia wanafanya kazi hawana kelele
Tupatwe na wivu mkubwa wa kutulia kama wao
Kila siku kelele za huyu kafanya hivi yule kafanya vile zinaharibu nchi
Dunia itasonga mbele sisi tutachelewa mwisho tutaonekana wajinga kwasababu wenzetu watafanikiwa sisi tutabaki na kelele za kisiasa zisizokwisha
Kaeni mezani fanyieni kazi yote yanayopigiwa kelele
Uzuri ni kuwa yote hayo ni mambo ya kuzungumzika wala sio ya kushikiana visu na mawe
Visu na mawe yalikuwa maisha ya zamani karne ya kwanza
Karne hii tuliyopo sio ya kushambuliana kama fisi kana kwamba sisi ni wanyama
Wanasiasa kaeni chini myamalize kwasababu ninyi ndio wenye uamuzi wa mwisho na Wananchi tunafuata maagizo yenu
Mkieleza Wananchi mambo mema basi watafanya lakini pia mkiwaeleza mabaya watafanya pia