Wanasiasa Na Wanarakati Wa Tanzania Pasua Kichwa, Wengine Wanahoji Vitu Vya Msingi Pale Tu Wanapokosa Fursa, Wengine Vitu Vya Hovyo Hovyo Tu

TataMadiba

JF-Expert Member
Feb 7, 2014
9,866
5,742
Tangu Serikali ya awamu ya Tano chini ya Uongozi wa Rais John Pombe Magufuli nimekuwa nikufuatilia kauli za Wanasiasa na wanaharakati wanaojaribu kuukosoa uongzi wa JPM , hakika hio nchi ina watu pasua kichwa sana.
Watu ambao ukosoajo wao ulitegemewa kuwa changamoto kwa Serikali katika kuyashughulikia matatizo ya wananchi, wamekuwa na ukosoaji wa hovyo kabisa.

Kuna wengine walijaribu kuhoji mambo ambayo ukiwasikiliza kwa makini unaona kama wana hoja lakini kumbe ni kwa sababu tu wamekosa fursa za kupiga maana mambo kama hayo hayo yalitokea wakati wakiwa kwenye nafasi za kuyahoji lakini wakayanyamazia kwa sababu tu nao walikuwa sehemu ya ubadhilifu huo, mbaya kabisa wanayoyahoji hivi sasa hawana chembe yoyote ya ushahidi juu ya wanachokihoji.
Lililo nisikitisha ni hili la kuhoji baadhi ya Watanzania kuteuliwa kwenye nafasi mbalimbali za uongozi. Hivi kiwa Mkuu wa Wilaya au Katibu tawala sifa zake lazima uwe na jinsia ya kiume, mzee, au msomi wa taaluma fulani? Basi Watanzania tulifanywa mazoba , ukosoaji wa kipumbavu kiasi hiki tutapoteza muda mwingi sana kuupigia makofi na kushangilia kijinga kijinga tu.

Kama hivi ndivyo tunavyopaswa kuikosoa Serikali kwa lengo la kuifanya iwe kwenye mstari na kuwatumikia wananchi wake hakika safari bado ni ndefu.
Eti "Kama Wachumba wenu ndiyo wanateuliwa kuwa Wakuu wa Wilaya?" Na watu wanapiga Makofi paa, paa, paaa.

Jamani hatuko serious. Hivi huyo anayewateuwa hao Watanzania ni kweli anaweza kumteua mtu ambaye hana uwezo? Wangapi waliteuliwa kwa matumaini makubwa lakini wamelitumbukiza taifa letu kwenye wimbi la Ufisadi, ruswa, wizi, uzembe n.k? Wanasiasa wetu, wanaharakati wetu na Wasomi wetu ni kweli mna akili na mawazo yanayofanana? Hatuwezi kuwatofautisha kweli kwa kauli zenu angalau tukasema huyu ni msomi, huyu ni mwanasiasa tu na yule siyo kosa lake ni mwanaharakati?
 
Nakumbuka JPM aliwaita wastaafu wakampa ushauri,moja ya majibu yake ni kuwa aachwe atawale halafu atakuja kuhukumia baadae!Akatolea mfano kuwa hata Obama kamuacha Trump atawale anavyotaka!
Daah,wazee wakainamisha tu vichwa kwa aibu!Hii nchi sio kampuni yako mpaka watu wasikuseme wanapoona mambo hayaendi vizuri,yaani uachwe tu!!!!!
 
Tangu Serikali ya awamu ya Tano chini ya Uongozi wa Rais John Pombe Magufuli nimekuwa nikufuatilia kauli za Wanasiasa na wanaharakati wanaojaribu kuukosoa uongzi wa JPM , hakika hio nchi ina watu pasua kichwa sana.
Watu ambao ukosoajo wao ulitegemewa kuwa changamoto kwa Serikali katika kuyashughulikia matatizo ya wananchi, wamekuwa na ukosoaji wa hovyo kabisa.

Kuna wengine walijaribu kuhoji mambo ambayo ukiwasikiliza kwa makini unaona kama wana hoja lakini kumbe ni kwa sababu tu wamekosa fursa za kupiga maana mambo kama hayo hayo yalitokea wakati wakiwa kwenye nafasi za kuyahoji lakini wakayanyamazia kwa sababu tu nao walikuwa sehemu ya ubadhilifu huo, mbaya kabisa wanayoyahoji hivi sasa hawana chembe yoyote ya ushahidi juu ya wanachokihoji.
Lililo nisikitisha ni hili la kuhoji baadhi ya Watanzania kuteuliwa kwenye nafasi mbalimbali za uongozi. Hivi kiwa Mkuu wa Wilaya au Katibu tawala sifa zake lazima uwe na jinsia ya kiume, mzee, au msomi wa taaluma fulani? Basi Watanzania tulifanywa mazoba , ukosoaji wa kipumbavu kiasi hiki tutapoteza muda mwingi sana kuupigia makofi na kushangilia kijinga kijinga tu.

Kama hivi ndivyo tunavyopaswa kuikosoa Serikali kwa lengo la kuifanya iwe kwenye mstari na kuwatumikia wananchi wake hakika safari bado ni ndefu.
Eti "Kama Wachumba wenu ndiyo wanateuliwa kuwa Wakuu wa Wilaya?" Na watu wanapiga Makofi paa, paa, paaa.

Jamani hatuko serious. Hivi huyo anayewateuwa hao Watanzania ni kweli anaweza kumteua mtu ambaye hana uwezo? Wangapi waliteuliwa kwa matumaini makubwa lakini wamelitumbukiza taifa letu kwenye wimbi la Ufisadi, ruswa, wizi, uzembe n.k? Wanasiasa wetu, wanaharakati wetu na Wasomi wetu ni kweli mna akili na mawazo yanayofanana? Hatuwezi kuwatofautisha kweli kwa kauli zenu angalau tukasema huyu ni msomi, huyu ni mwanasiasa tu na yule siyo kosa lake ni mwanaharakati?
Ni kweli kabisa ulilosema - Nilimsikia Generali Ulimwengu akisema hayo nikamshangaa sana mtu na heshima zake anaongea mambo ya vijiweni kwenye kadamnasi kubwa hivyo. Ili kusudi apigiwe makofi iweje? Ni aibu!
 
Back
Top Bottom