Wanasiasa na mtaala wa elimu

Wanasiasa na mtaala wa elimu

Civilian Coin

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2012
Posts
2,305
Reaction score
4,401
Wanasiasa wa Tanzania wamekuwa ndio chanzo cha kushuka kwa elimu ya Tanzania, matokeo mabovu ya darasa la saba, kidato channe na kile cha sita chanzo ni wanasiasa. Na kumbuka Mh. Joseph Mungai alipokuwa waziri wa elimu alibadilisha kabisa mtaala wa elimu kwa kuunganisha baadhi ya masomo na kuwa somo moja kwa shule za msingi na zile za sekondari, hivyo hivyo na kuondoa masomo ya biashara kwa shule za sekondari. Hali hii iliwachanganya walimu na wadau wa elimu, naye Mh. Magreth Sitta alipo teuliwa kuwa waziri wa elimu akarejesha mtaala wa zamani na kuvunja utaratibu wa Mh. Mungai, kama vile haitoshi Profesa Jumanne Maghembe naye alipoteuliwa kuwa waziri wa elimu yeye hakubadilisha bali akaboresha kwa kupunguza baadhi ya mada na kuongeza mada zingine ambazo hazikuwepo kabisa. Pamoja na yote wanafunzi na walimu wanashindwa washike lipi na wafuate lipi? Kinachofuata ni kuporomoka kwa taaluma ya elimu na kuweka visingizio walimu hawatoshi.

Kubadilishwa kwa mitaala mara kwa mara ni chanzo cha kushuka kwa kiwango cha taaaluma na ufaulu kwa wanafunzi kudorora kutokana na walimu kutokuwa na uelewa wa kutosha kuhusu mitaala mipya.
Kitendo cha serikali kubadili mitaala mara kwa mara kina shusha elimu, mtaala unabadilishwa bila hata mwalimu kupewa semina, kuna walimu wengine ni wazamani, tangu walipo jifunza mbinu za ufundishaji wakiwa chuoni hawaja wahi kupata semina.

Baada ya kubadilishwa kwa mitaala mipya, walimu wanaletewa wa fundishe bila semina na mbinu na elimu ya ufundishaji, matokeo yake wanashindwa kumudu masomo, hivyo kuwaathiri wanafunzi. Kubadilishwa huku kwa mitaala kunawafanya wanafunzi wasielewe somo kutokana na kutokuwepo kwa msimamo thabiti, hali inayo wapa wakati mgumu wanafunzi kuelewa somo.

Ni muda muafaka sasa kwa serikali yetu kuangalia upya jinsi ya kuboresha mitindo ya mitaala hiyo ya elimu maana ina wachanganya wanafunzi na walimu.

Mitaala imegeuzwa kuwa biashara binafsi za watu, kwasababu kila waziri anapoingia madarakani anakuja na mbinu zake mpya, anabadilisha mitaala iliyopo na kuweka ya kwake, mawaziri na wizira ya elimu wamegeuka wafanyabiashara wa elimu. Mitaala inapoandaliwa iwe ni ya kudumu siyo ya muda mfupi, kama ina mapungufu ifanyiwe maboresho siyo kubadilishwa, na vilevile uandaaji wa mitaala ushirikishe walimu, wazazi na wadu wa elimu kwani wao ndio walio karibu na mazingira yanayowazunguka wanafunzi wa kitanzania.
 
AFADHALI UMELIONA HILO ILA SWALA ZIMA LA MASLAHI YA WALIMU PIA LINACHANGIA> ONA SASA MATOKEO YA DARASA LA SABA WANAPATA KIGUGUMIZI KUYATOA. EBU WALIMU KAZENI HAPOHAPO HADI SERIKALI ITAKAPOWATAMBUA UMUHIMU WENU KWA JAMII. MISHAHARA MIZURI WANAPEANA WAO MWALIMU AMEACHWA KAMA YATIMA KAZENI UZI MPAKA KIELEWEKE. SERIKALI IRUDI KUWAPIGIA MAGOTI. KAMA HAWATAKI MWAKA 2o13 WAFERI WOTE. HAKUNA HAJA YA KUGOMA KWA SASA TUWAKAMATE KATIKA MATOKEO. WAKOME KURINGA. WATANGAZE YALIVYO WASICHAKACHUE NA BADO WATAWATAMBUA WALIMU NI AKINA NANI?
 
Unapokuwa na kiongozi dhaifu wa taifa kama kikwete yanayotokea sio bahati mbaya yanapaswa kutokea.

Alisema akawambia wafanyakazi nitawapiga, kumbuka walimu ni sehemu kubwa ya hao wafanyazi nani anakubali dharau kama hizi?

Akawatisha walimu anadhani taaluma ni siasa za maji taka kama afanyavo kijana wake nape kuropoka na kupayuka ovyo

Kubadili mitaala ni sababu kubwa ya kuyumba na kushuka kwa elimu, lakini maslahi duni kwa walimu ni sbabu kubwa zaid.

Endapo KIKWETE ataendelea na ujasiri wa kijinga kuwakandamiza walimu hakika hatutakuwa na la kujivunia zaid taifa la wajinga. madhara ya ubabe na mslahi duni ni zaidi ya madhara ya kubadilisha mitaala
 
Ujinga wa CCM ni pale wanapopima ubora wa elimu kwa idadi... Viongozi vilaza tulio nao wanatugharimu kweli kweli. Wanaona fahari sana kusema wameandikisha wanafunzi kadhaa wa ngazi flani ya elimu... Habari ya ni kwa kiasi gani elimu watakayoipata hao walioandikishwa itawawezesha kukabiliana na changamoto za maisha za sasa sio ishu kabisa... Hawa vilaza wanatucost. Russel aliwahi kusema "The trouble of the world is that the stupid are so confident while the intelligent are full of doubt". Vilaza hawa wanajiamini sana na ndio watawala wakati wenye akili wamejaa hofu na mawazo yao yamefunikwa kabisa. Tukiendelea kutawaliwa na hawa vilaza, tutakuwa tunaendelea kudumbukia shimoni kwa maelfu!
 
Tuacheni itikadi za kisiasa hapa!
Hili ni suala linalogusa moja kwa moja mustakabali wa maendeleo ya taifa letu. Mfumo wetu wa elimu haujabadilishwa, ni ule ule tuliochukua kutoka kwa mkoloni! Tukiendelea nao tutakuwa taifa tegemezi daima!
Suala la kuwa na mfumo mpya wa elimu linatakiwa lichukuliwe kwa umakini na liwe na mchakato mrefu kama tunavyotaka katiba mpya.
Umefika wakati wa kuamka na kuanza kulipigia kelele hili tatizo, watoto/wadogo zetu wanaweza wakajikuta ni wataalamu wa kuchati kwenye facebook na kutembelea mitandao mbalimbali wakati hawana uwezo wa kubuni hata kitu kimoja (sijatoka nje ya pointi, namaanisha mfumo wa sasa unapelekwa kimazoea kiasi kwamba watoto wana uwezo hata wa kuotea maswali wanayoulizwa kwenye mitihani kwani walimu wao nao wamepoteza ubunifu wa kutunga maswali; hii inafanya watoto wazingatie mambo mengine yasiyo na maana kwa maisha yao)
Huwezi ukamlazimisha mwalimu atunge maswali mapya wakati mitaala ni ile ile tokea zamani. Na hapa sio suala la kubadilisha mada (topics) katika masomo, ni kubadilisha mfumo mzima ili baadae tuwe na wataalamu wetu wa kuzitumia rasilimali tulizonazo!
 
Back
Top Bottom