umenena mkuu MMJ tatizo wanasiasa wetu penye janga ndio wanataka watoke kisiasa,wanakua wanaongea wasichokiamini.
Nakiri suluhu ya kidiplomasia ndio bora.
Lakini MM unafahamu ya kuwa Malawi wamegawa vitalu kwa ajili ya utafiti wa gesi na mafuta ziwani upande wa Tanzania? In fact ni ziwa lote upande wa TZ. I agree, sometimes you must be very bold to halt the situation while pursuing diplomatic agenda.
Mwanakijiji ni mnafiki sana, kumradhi kama nitakuwa sijaeleweka ila nitasherehesha.
Mkjj ni mtu aliejenga chuki na Lowasa tokea alipotaka kumuhoji na kumwambia amuache anakula, akaanza kuleta vihadithi vya sungura, mara ndege inayoruka na wananchi waloduwaaa na mengi mengine ya kipropaganda, lengo kumchafua lowassa aonekane hafai ktk jamii.
daima mwanakijiji amekua akiotea na kusubiri nn Lowasa kasema au kafanya aje na spinning zake. mwana kijiji acha chuki binafsi na jadili mambo kwa upana wake.
tuje kwenye suali ambalo liko mbele yetu kama wana taifa hili, serikali kwa kupitia waziri wetu wa mambo ya nje ameeleza msimamo wa taifa letu, Samuel Sitta ameeleza, na tuko wazi kabisa njia ambayo taifa hili itafuata ni kutafuta utatuzi wa taifa hili kwa njia ya amani na kidiplomasia. na kabla ya Lowassa watu wakaanza kuja juu, ooh serikali dhaifu, kwa nn tusitoe kauli na kuandaa jeshi? na hao unaojidai kuwatetea au niseme njia yako ya kutaka kutugawa kwenye jambo la nchi kivyama nnakusudia CHADEMA wabunge wao ndio walikuwa wakali sana kuwa tuandae sasa mapambano.
cha msingi serikali yetu iko makini, na alichozungumza Lowasaa hajazungumza kama Lowasaa amezungumza kama Mwenyekiti kwenye kamati ya Ulinzi na Usalama, ulitaka azungumzie nn kuhusu usalama wa nchi ? yy ameeleza jinsi gani kuwa usalama wa nchi yetu upo, na jinsi gani jeshi letu lilivyo tayari kama litalazimishwa kwenda vitani(jua hii si option ya taifa). sasa kosa lake ni lipi ? angenyamaza ungesema, akisema unasema ww kweli mnafiki na mtu mbaya sana kwa taifa letu.
mm nnaona ww ni hatari zaidi kwa taifa letu kuliko hata malawi. acha kaka hizo
Umesema vyema sana nakubaliana na wewe asilimia mia. Lakini nikusahihishe kidogo tu kuwa Tanzania haina uwezo wa kuipiga Malawi nina huakika na hilo.
Pili ikitokea vita nina tamani sana Tanzania ishindwe (mimi ni mtanzania ninaipenda sana nchi yangu Tanzania.). Hii inchi ya mafisadi ikipigwa then naamini kabisa itakuwa nchi ya watanzania baada ya Vita.
Wacha upuuzi wewe! vita sio kitu kizuri hata kidogo, wala sio kitu cha kushabikia........ ianaelekea hujaonja radha ya vita...............Mzee/kijana acha hiyo mambo! Acha zipigwe,zirindimeeee. Soma historia vizuri, hakuna nchi imesonga mbele bila damu kumwagika. Acha woga. akiingia sebuleni, ataingia bedroom. Amka!
Kwa maana hiyo tunaomba vita hiyo na itokee ili sisi sote tuungane na Malawi kuipindua serikali ya ccm madarakai, tukifa watu kama laki hivi waliobaki wataishi maisha mapya ya raha, wakubwa na wadogo tutaheshimiana.Mmj that's very nice analysis. Jamani point hapa ni tabia ya serikali kutuhamisha mawazo na kubadili dira na kuacha mambo muhimu bila kujadiliwa/kufanyiwa kazi. Tumeshtuka. Ya madaktari yako wapi? Walimu? Achilia mbali mauaji ya raia wasiokuwa na hatia. Hakuna hata siku moja waziri hata rais kutangaza vita dhidi ya zuluma mbalimbali hapa nchini,au ujinga n.k mimi naona adui mkubwa yupo ndani ya nchi na sio nje ya nchi.na adui huyu ni CCM