Wanasiasa na Lugha ya Vita: Hekima ya kupunguza sababu ya kuingia vitani na Malawi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanasiasa na Lugha ya Vita: Hekima ya kupunguza sababu ya kuingia vitani na Malawi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Aug 8, 2012.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Aug 8, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  Daraja ya Kagera (Kyaka) lililobomolewa na Idi Amin na vikosi vyake pamoja na majengo yaliyobomolewa nakubakia majeraha ya vita.


  • Wanasiasa wanaotoa lugha ya vita hawana hekima na ni hatari
  • Wengine wanatafuta ujiko wa kisiasa
  • Tusizungumzie vita kama hatuko tayari kupigana
  • Vita si lelemama

  Na. M. M. Mwanakijiji

  Sikutegemea kama Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ulinzi, Usalama na Mambo ya Nje Bw. Lowassa kutoa kauli ambayo ikiunganishwa na ile ya Sitta na ya Membe inazidi kuchochea hali ya kutotafuta suluhu. Wote hawa watatu bila ya shaka wanasema kutokana na nafasi zao lakini pia yawezekana wanasema kwa sababu wote watatu wanatajwa vile vile kama wagombea watarajiwa wa urais mwaka 2015. Hata hivyo nazipima kauli hizi kwa jambo la kwanza na si kwa hilo la pili.

  Vita si jambo dogo na si jambo la mzaha kama watu wengine wanavyochukulia. Nimeona tangu Wamalawi walipozungumza suala la kudai "ziwa zima" la Nyassa kuwa ni lao baadhi ya watu wetu mwitikio wao wa kwanza umekuwa ni "tupeleke majeshi" au "tupeleke vijana wetu" na sasa leo Lowassa ananukuliwa na vyombo vya habari mbalimbali kuwa JWTZ liko tayari kwenda vitani na Malawi kuhusu suala hili. Hili ni jambo la kusikitisha na kushangaza.

  Kufikiria vita siyo jambo dogo na wala si jambo la kutafuta ujiko au siasa. Ni sawa na kuamua kushika bunduki na kumuelekezea mtu. Polisi huwa wanaambiwa kuwa usielekeze Bunduki kama hauko tayari kuitumia. Wale ambao wanabeba silaha (nao ni raia) wanajua kabisa kuwa hutoi silaha kibindoni kama hauko tayari ku-pull the trigger. Maana ya yote haya ni kuwa kutoa silaha na kuishika mkononi siyo suala la ubishoo, urembo au kujionesha kuwa unaweza.

  Tusipokemea hili la wanasiasa mwisho tutaona watu wanaanza mazoezi ya kutuonesha vifaa vya kivita ili kuwapiga mkwara wa Malawi. Na kweli wapo ambao wanatamani kuona "vijana wetu" wanaanza kuelekea mpakani au kwenye ukingo wa Ziwa Nyassa ili kutuma ujumbe kuwa tuko tayari. Sasa hili ni zuri na linasisimua akili na hisia za "kizalendo". Lakini tusije kuwa ni mambo ya Wag the Dog ambapo ili kushinda uchaguzi timu ya wanamkakati wa kampeni waliamua kutengeneza 'vita isiyokuwepo' ili kupoteza mawazo ya wapiga kura.

  Ninachoogopa zaidi ni kuwa wakati watawala wetu tumewabana kuhusu uongovi wao mbovu, sera zao zilizoshindwa na ukosefu wa maono usiokoma suala la mgogoro wa Ziwa Nyassa limewapa 'gia' ya kutokea na sasa hata watu waliokaa kimya wakati wananchi wetu wanauawa nakudhalilishwa na vyombo vya usalama wanasimama pasi ya kuomba radhi na kutaka tusimame nyuma yao. Nimeshangaa kuona Lowassa leo ameweza kukutana na vyombo vya usalama na kupewa taarifa zinazohusu vita lakini huyu huyu hajakutana na vyombo hivi wakati maisha ya wananchi wetu yanahatarishwa na vyombo hivi. Alikuwa wapi kwenye matukio ya Arusha, Mbeya (Tukuyu), Tarime na Songea? Kote huku hakuonesha kujali sana lakini leo ameibuka na kuonesha kuwa ana uwezo wa kufuatilia vyombo vya usalama?

  Kama nilivyosema hapo juu vita si lelemama kama baadhi ya watu wanafikiria. Najua wapo ambao wanafikiria kuwa vita dhidi ya Uganda ilikuwa ni uamuzi wa haraka na papara. Wengi (labda vijana zaidi) wanakumbuka tu maneno ya "nia tunayo na sababu tunayo" lakini ni wachache (hata wazee yumkini) wanaokumbuka kuwa kabla ya kufikia maneno hayo Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere alielezea juhudi mbalimbali za kutatua mgogoro wetu na Uganda licha ya "chokochoko" zilizoanza miaka karibu mitano nyuma. Kwa Tanzania kwenda vitani ilikuwa ni uamuzi wa mwisho pale ambapo njia zote za amani na kidiplomasia ziliposhindwa.

  Leo viongozi wetu tena wakubwa na wenye dhamana nzito zaidi wanazungumza kana kwamba tumeshindwa kabisa kutafuta njia za amani na za demokrasia na sasa wanataka kuifanya Malawi kama wanavyofanyia wananchi wetu. Wananchi wakiandamana wanapigwa virungu na kuuawa na wakigoma wananyamazishwa kwa ghafla. Na hata mazungumzo wanataka yawe kwa masharti yao. Matokeo yake wamejenga fikra wanaweza kum-bully mtu yeyote, vyovyote, na kwa lolote kiasi kwamba wanataka kuanza kuibully Malawi. Hili linafanywa kwa sababu moja tu kuwa Tanzania ni kubwa kuliko Malawi na inawezekana ina uwezo mkubwa wa kuishinda Malawi.

  Wanaozungumza hivi wanafikiria vita inapigwana na wingi wa watu tu na vitu. Vita ni mikakati na mbinu lakini vile vile vita ni kujitoa muhanga. Tunapozungumzia lugha ya vita sijui kama tunafikiria viongozi wetu wanaweza kuhamasisha taifa kama ilivyokuwa miaka ya 1970 ambapo watu walichangia kuku, mbuzi na ng'ombe. Wangapi kati yetu leo watakuwa tayari kutoa magari na mabasi yao kwenda vitani? Wangapi wataamua kwa hiari yao kwenda kupigana chini ya viongozi hawa hawa? Itakuwaje kama watu wakiwa vitani kashfa kubwa ya ufisadi nyumbani inanguruma tena (mafisadi kwa asili hawabadiliki).

  Tunapozungumzia vita tunazungumzia maisha ya watu kuuawa. Watu wasifikiri kuwa tukienda vitani na Malawi au nchi nyingine yoyote jirani basi tutakuwa kama tunamsukuma mlevi. Ni wangapi wanafikiria kulipuliwa kwa miji yetu inayozunguka ziwa Nyassa? Mbamba Bay, Kyela, Tukuyu, Rungwe, Mbeya, hata Songea? Kweli kina Lowassa wanapozungumza lugha ya vita wanafikiria kabisa kuwa tumesahau jinsi Amin alivyolipua Mwanza? au ndio viongozi wetu hata historia tena wamesahau? Au watu wamesahau jinsi tulivyolazimika kuchimba mahandaki na kufanya mazoezi ya kujihami hadi kuwa na kuku ndani kwa ajili ya kukimbia nao kwenye mahandaki? Au watu wameshasahau jinsi Idi Amin alivyoweza kuua mamia ya watu wetu pale vikosi vyake vilipovuka Mutukula na kuingia Kagera?

  Ninachosema ni kuwa ipo haja ya haraka ya viongozi wetu kuonesha hekima ya kukwepa lugha ya vita. Si kwa sababu hatuna uwezo wa kupigana na Malawi (naamini tunao tena mkubwa na naamini tunaweza kushinda) lakini bado hatujawa na sababu ya kufanya hivyo. Watu kudai "ziwa zima" wakati sisi tumejenga bandari na watu wetu wanavua na kuishi kwenye ziwa hilo na tuna meli miaka nenda rudi na Wamalawi hawajarusha hata baruti ni jambo la kutufanya tufikiri. Kama kweli Wamalawi wangekuwa wanataka vita au ugomvi mbona wao sababu "wanayo" kuwa tumeingilia Ziwa lao na tunafanya vitu kinyume cha sheria?

  Wamalawi walipozungumza kwa lugha ya Vita mara moja walitambua kuwa hakuna sababu ya ku-escalate tension kwenye eneo hilo hasa kwa vile tayari tumeshawahi kuwa na tension sana. Ndio maana Waziri wa Mambo ya Nje aliamua kupunguza makali ya lugha ya vita. NI wakati kwa viongozi wa TAnzania nao kupunguza ukali usio wa lazima na kuchochea lugha ya vita. Na sisi wananchi tusiuziwe kirahisi vita kwani ina gharama kuliko watu tunavyoweza kufikiria. Ikumbukwe vita ya Uganda iliigharimu Tanzania kuliko watu wengi wanavyojua na imeacha mojawapo ya majeraha makubwa katika mwelekeo wa uchumi wetu ambayo hadi leo tunasikia maumivu yake. Sijui kama tunataka vita nyingine hasa kwa sababu ambazo ni za kidiplomasia na kisiasa.

  Hekima itusukume kufikiria mara mbili. Tutoe nafasi kwa diplomasia na mazungumzo ya amani na nina uhakika wa Malawi kama ni watu wa amani watanyosha mkono wa amani. Njia mojawapo kama tukitaka na sisi kutumia mbinu za diplomasia ni hilo nililosema kwenye mada nyingine badala ya kupeleka vifaru na askari wetu karibu na Ziwa Nyassa na sisi tuanze utafiti kwenye eneo tunaloamini ni letu na kuwaacha Wamalawi wafanye kwenye eneo lao. Kama wanafanya hivyo kwenye sehemu ya eneo letu basi tuna sababu ya kuhakikisha hizo 'incursions' hazitokei na hapo ikibidana kuweka boti zenye silaha kuhakikisha hayo hayatokei.

  Endapo juhudi hizi za kuonesha sisi ni watu wa amani hazitapokelewa na kama juhudi za kidiplomasia zitashindwa na Wamalawi watapuuzia kabisa madai yetu na kuanza kutenda kanakwamba hatuna la kusema basi ni wakati huo Watanzania waandaliwe kwa kitu ambacho kinaweza kutokea - vita. Na hili lisizungumzwe na kila "dick, tom and harry" kwa sababu wanavaa suti za vyeo mbalimbali. Mtu pekee wa kuweza kulizungumzia hili kama uwezekano ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  Endapo tutaacha wanasiasa ambao wanatafuta ujiko kwenye macho ya wananchi walizungumzia na kututia hamasa wakati wao wenyewe hawatoenda vitani na yawezekana hawana mtoto au ndugu hata mmoja JWTZ basi tutajikuta tunapelekwa vitani kisiasa na siyo kwa sababu tunatishiwa au tunajihami. Ni matumaini yangu viongozi wa upinzani (CHADEMA) hawatoingia mtego huu wa kuzungumza lugha ya vita. Hili waachiwe CCM na mashabiki wake mpaka pale ambapo juhudi zao za kisiasa zitakpokuwa zimeshindwa basi waseme tunaenda vitani na hapo viongozi wa upinzani watolee maoni na msimamo wao. Wapinzani wasizungumze lugha ya vita bali ya amani.

  Ndio maana kwa upande wangu ninaangalia sana watu wanaotaka kuwa ma-amiri jeshi wakuu, tusipoweza kuwaangalia wanavyoweza kutumia hekima watu hawa watakuja kutupeleka vitani na tukajikuta tunapigana na tukiulizwa tunapigania nini hatujui kumbe watu walitukaniana mama zao na taifa likaingizwa vitani. Na matumaini yangu JWTZ halitaingia kwenye hili suala la kisiasa na kidiplomasia. Tunataka JWTZ letu litakapozungumza iwe ni baada ya tangazo rasmi la vita nje ya hapo JWTZ iwaache wanasiasa wafanya mambo yao.

  Siasa na Diplomasia vikishindwa tujiandae kwa ushindi wa Kivita. Hapo ndio tutoe silaha zetu kibindoni na kuzielekeza kwani tutakuwa tayari kuzitumia.

  MMM
   
 2. mndwadage

  mndwadage JF-Expert Member

  #2
  Aug 8, 2012
  Joined: Jul 15, 2012
  Messages: 345
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  umenena mkuu MMJ tatizo wanasiasa wetu penye janga ndio wanataka watoke kisiasa,wanakua wanaongea wasichokiamini.
   
 3. M

  Masauni JF-Expert Member

  #3
  Aug 8, 2012
  Joined: Aug 15, 2010
  Messages: 378
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Umesema vyema sana nakubaliana na wewe asilimia mia. Lakini nikusahihishe kidogo tu kuwa Tanzania haina uwezo wa kuipiga Malawi nina huakika na hilo.
  Pili ikitokea vita nina tamani sana Tanzania ishindwe (mimi ni mtanzania ninaipenda sana nchi yangu Tanzania.). Hii inchi ya mafisadi ikipigwa then naamini kabisa itakuwa nchi ya watanzania baada ya Vita.
   
 4. Acha Uvivu

  Acha Uvivu JF-Expert Member

  #4
  Aug 8, 2012
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 528
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  M. M. M nakujua na nakukubali kwa maono yako hasa kupitia makala zako zilizojaa hekima. Lakini ni wanasiasa wepi watakuwa na japo akili ya kutambua hoja hii nzito ya kufikiri kwanza kabla ya kuchukua maamuzi ya kivita? Na tena ukijua kuwa mvutano huu hata mwezi haujaisha tokea kuibuka na tayari wameropoka. Sitta, Membe na Lowassa ni viongozi wa serikali lakini kimkakati utajua kila mmoja amesema kuhusu suala hili kwa malengo mahususi, Kisiasa. Tusubiri tuone.
   
 5. M

  Magesi JF-Expert Member

  #5
  Aug 8, 2012
  Joined: Jul 10, 2012
  Messages: 2,590
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Fisadi amepata pakutokea anaropoka 2 anfikiria vita ni sawa na ufisad wanaoufanya
   
 6. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #6
  Aug 8, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Kipimo cha watu tulionao
   
 7. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #7
  Aug 8, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,197
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Mwanakijiji viongozi wetu ni malimbukeni vita ya kagera mpaka Leo hatuja recover wanataka nyingine kwasababu wanapakukimbilia wengine wanaumwa wanataka wakifa kwa magonjwa Yao isingiziwe walikuwa mstari wa mbele kwenye vita ili historia Yao iwe safi
   
 8. Mkuu wa chuo

  Mkuu wa chuo JF-Expert Member

  #8
  Aug 8, 2012
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,253
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  duh! Kama ndio hivyo kwanini tusiwaachie tu hilo ziwa mambo yaishe kwasababu mbona maliasili ziko nyingi tu huku Tanzania
   
 9. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #9
  Aug 8, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,273
  Trophy Points: 280
  Mimi tangu waanze kauli zao za kishetani nimekataa kabisa kuingizwa mkenge katika hili, Kikwete amekwenda Uganda kwenye mkutano wa Amani ya maziwa makuu, huku nyumbani vibaraka wake wanahubiri vita!! my self am out of this na niko tayari kuishi uhamishoni kuliko kuifia nchi inayotuuwa huku tukiwa hai.

  Anayetaka kuninyooshea kidole mimi siyo Mzalendo na anaipe kwanza tafsiri isiyo na shaka ni nini maana ya neno uzalendo.
   
 10. Sir R

  Sir R JF-Expert Member

  #10
  Aug 8, 2012
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 2,177
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Nchi iko katika mgawanyiko mkubwa.

  JK anawalinda mafisadi sijui vita wanayotangaza watapataje support ya wananchi.

  Kuna watu watawasaidia wamalawi.
   
 11. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #11
  Aug 8, 2012
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Hawana uwezo mkubwa wa kukaa kwenye meza yamajadiliano, kwa mfano wameshindwa kujadiliana na madaktari, waalimu, wazee wa community, wanafunzi kuhusu madai yao ya msingi na aghalabu wamekuwa wakikimbilia FFU kutuliza.

  Lakini above all in times of war people make money, isije kuwa wanaombea vita ili wafaidi kwenye expenditure ya dharura wakati wa vita.
   
 12. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #12
  Aug 8, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  kweli kabisa Watanzania wanafikiria vita in terms of nostalgia ya vita ya Idi Amin.. na wengine wanataka tu na sisi "tuheshimiwe"...
   
 13. N

  Ndyali JF-Expert Member

  #13
  Aug 8, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 1,222
  Likes Received: 148
  Trophy Points: 160
  Kama ugonvi huu unasababishwa na fununu za kuwepo kwa mafuta naomba watanzania wenzangu tuwaachie wamalawi wayachimbe maana ni wananchi wa Malawi wtafaidika. Lakini tukichimba mafuta hayo kwa kivuri cha watanzania atafaidika Lowasa na Rizwan, huku wakiwaacha watoto wetu wakikalia matofali/mawe madarasani. Misaada pekee tunayopata kwa hawa jamaa ni Tshirts za njano/kijani wakati wa chaguzi. Wenzetu wa Malawi hutuzia bidhaa mbalimbali kwa bei nafuu sana kama enzi za wakoloni wa kizungu, kuliko mkoloni mweusi ccm .
   
 14. S

  Sheba JF-Expert Member

  #14
  Aug 8, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 210
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Mwanakijiji

  Umenena sahihi kabisa, sina la kuongeza na nakupongeza kwa busara hii kubwa. Wakati mwingine unatoa busara sana, sijui wakati mwingine unaamuaga tu kuyumbisha watu? Ujumbe wako wa leo ningependa ufikiewengi zaidi. Umeongea kama stateman. Udumu​
   
 15. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #15
  Aug 8, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280

  huwezi kujua how correct uko kwenye hili. Msidhani wao watapigana hivyo vita shauri lenu!
   
 16. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #16
  Aug 8, 2012
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Hawatapigana asilani na madhara ya vita socially ( majeruhi na vifo) financially kwa wananchi haitawagusa kamwe, bali wataisikia redioni tu
   
 17. s

  sirghanam JF-Expert Member

  #17
  Aug 8, 2012
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 289
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Tulimshinda amini inayesadikika alikuwa na vifaa bora vya kivita kuliko sisi kwa kitu kimoja kikubwa.. Amini alitumia jeshi lake kupigana na Watanzania wote. Nyerere aliwatayarisha Watanzania wote, na wote walikuwa sehemu ya ile vita.. Hakika Tanzania ikiingia vitani kipindi hiki nchi ilivyokosa umoja itakuwa ngumu sana. HAWA VIONGOZI SINA UHAKIKA KAMA WANALIONA HILI
   
 18. Bob

  Bob JF-Expert Member

  #18
  Aug 8, 2012
  Joined: Sep 10, 2007
  Messages: 277
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Nakiri suluhu ya kidiplomasia ndio bora.
  Lakini MM unafahamu ya kuwa Malawi wamegawa vitalu kwa ajili ya utafiti wa gesi na mafuta ziwani upande wa Tanzania? In fact ni ziwa lote upande wa TZ. I agree, sometimes you must be very bold to halt the situation while pursuing diplomatic agenda.
   
 19. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #19
  Aug 8, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,273
  Trophy Points: 280
  Na wewe huwe na busara, huwezi kuquote uzi mzima halafu unareply mistari miwili hujui unawapa shida wanaotumia simu unnecessary? kwa nini usimmention Mzee Mwanakijiji??
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 20. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #20
  Aug 8, 2012
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Na hayo mafuta na gesi tunayodhani tunailinda haitatusaidia tukikomboa eneo hilo, kwani tayari wenyewe wanaopiga kelele leo hii wana geological surveys za ziwa lote ili kujua swaiba gani apewe
   
Loading...