Wanasiasa acheni ushamba wa kuchoma moto mali za familia kwa kisingizio cha "hasira" za kufelishwa Uchaguzi!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,937
141,911
Mambo yaliyosikika kutokea Meatu mkoani Simiyu na Liwale na maeneo mengine ya Mikoa ya Kusini yanasikitisha sana.

Ninaandika haya baada ya kushuhudia wananchi wa Lindi wakikitaja chama kimoja cha Upinzani kinachoongozwa na Profesa anayeheshimika duniani kwamba kinahusika na hii " choma choma" ya nyumba na magari viongozi wa CCM na Serikali.

Huu siyo utamaduni wa kitanzania, kama unaamini Umefelishwa kwenye Ubunge au udiwani isivyo halali nenda Mahakamani ukadai haki yako badala ya kujigeuza jambazi wa kuchoma mali za washindi.

Wanasiasa hasa wa kusini acheni " Ushamba" jifunzeni kwa wenzenu wa kaskazini wanaofanya siasa za kistaarabu.

Maendeleo hayana vyama!
 
Hivi kwa nini UVCCM nao wasireact. Kwa kuchoma nyumba za wagombea ili tuelewane Ikiwezekana hata kwa kutumia polisi wajue kuwa tumeshika mpini.

Japo tuoneshane makali!

#LoserLissu.

#PoleniUpinzani
 
Wewe binafsi umekuwa ukishadadia uonevu wa makusudi kwa wenye mitazamo tofauti na nyie,halafu sasa,una kuja na maswali kwanini tumefika huku..Rudi nyuma na tafakari yote ambayo umekuwa ukishadadia.
Unadhani hao uvccm ni " wanyonge" bwashee!
 
Back
Top Bottom