Mbatia: Hisia za Wanasiasa kuhusu Uchaguzi Mkuu haziwezi kuelezeka kwa maneno

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,498
9,279
Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia, ameshauri kufanyika kwa mazungumzo ili kupata mwafaka wa kitaifa utakaoliwezesha taifa kwenda mbele baada ya kuwapo kasoro mbalimbali katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 28, mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mbatia aliwataka viongozi wote wa kidini kutumia ndimi zao vizuri, kukubaliana kwamba masilahi ya Tanzania kwanza, mambo mengine baadaye na kamwe wasikubali kukichoma moto kichaka kilichowahifadhi.

Mbatia alisema kuwa hisia za wanasiasa kuhusu Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu haziwezi kuelezwa kwa maneno, bali watu wote wenye upendo na Tanzania wanaweza kuziona hisia hizo.

Hata hivyo alisema kuwa pamoja na watu mbalimbali kuwa na hisia hasi zinazokinzana na utu, maadili ya Kitanzania pamoja na tunu zilizoelezwa kupitia Wimbo wa Taifa za umoja na amani, zinaweza kuchoma kichaka ambacho wamejihifadhi ambacho ni Tanzania.

“Maneno hayatoshelezi kuelezea hisia, labda kwa kupitia nafsi. Hisia zetu kwa ujumla kuhusu mchakato wa tukio lililoitwa Uchaguzi Mkuu wa 2020, haziwezi kuwakilishwa kwa maneno, lakini wote wenye nia nzuri na mama yetu Tanzania kwa kupitia nafasi zao wanaweza kusikia au kuelewa hisia za wengi kwa muda huu.

“Licha ya kwamba kwa miaka 59, hatujaweza kumtumia vizuri mama Tanzania ili tuweze kujipatia mahitaji msingi kwa wote na kwa furaha ya kweli, sasa tuko kwenye kumwangamiza,” alisema Mbatia.

Alisema kuwa kwa miaka 28 chama chake kimekuwa kikiimba wimbo wa kupata Tume Huru ya Uchaguzi na kwamba sasa gharama zake zimekuwa kubwa.

“Maneno yetu sasa yanasikika dunia nzima, kwani dunia nzima imeshuhudia vitendo vinavyokiuka makubaliano yetu ya kitaifa ya miaka 28 iliyopita, kwamba maendeleo endelevu yanatokana na demokrasia ya vyama vingi vya siasa.

“Kama taifa tumekiuka hata makubaliano ya kitaifa, kwa mfano kufunga baadhi ya mitandao ya kijamii,” alisema Mbatia.

Aliongeza kuwa endapo Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere angekuwapo leo, angewaeleza kuwa hii si Tanzania na demokrasia aliyowaachia na angewataka kujikusanya waanze upya.

“Hii siyo kwa wanasaiasa peke yao, ni la Watanzania wote, hatuwezi kuangalia tu wakati mama anaamka na huzuni na kulala na hasira,” alisema Mbatia.
 
Aha hawaaminiki, Mbatia pole sana, wote tunajua mgombea Urais wako alishinda kiti cha Urais. Na wewe pia ulishinda ubunge Vunjo, hata hahaha unasema wamekupora?

Maendeleo ya kisasa Tanzania.
 
kwani TAIFA LIMESIMAMA....? WE JAMES USALITI UNAKUTAFUNA kila kukicha tunawasikia MUAFAKA WA KITAIFA huwa siwaelewi kwani ninini shidaa............? kabla ya uchaguzxi uliwapa mgobgo wenzako wa upinzani ukijua labda utaambulia kitu, hukujua wenzako walikuwa wanataka kukutumia kama ngazi , TULIA ..........!!!
 
Inasemekana Ngiri (warthogs) ni moja ya wanyama wasahaulifu duniani kuliko viumbe vyote alivyo viumba Mungu.

Ngiri anaweza kuwa akifukuzwa na Simba na katika kimbia yake akikutana na majani mazuri ya kula atasimama na kuanza kula, then ataanza kujiuliza "hivi nilikuwa nafukuzwa na Simba Jana au Leo?".....ghafla Simba anatokea na kumrarua tayari Kwa kitoweo !!

James Mbatia kaamua kujitoa ufahamu na anadhani watanzania ni wasahaulifu kama Ngiri wakati yeye ni zaidi ya Ngiri.....
 
Uchaguzi ulikuwa huru na haki
kama mmeshindwa si Basi, au uchaguzi kuwa huru ni upinzani kushinda?
Sasa wewe Mbatia chama chako kimechoka!

Mgombea wako alikuwa mchovu!
pesa hakuna, hata mawakala hukuweka!
Hii story ya uchaguzi ulivurugika hausaidii sasa
...jipangeni, muda unayoyoma
 
Anasema kuhusu zile nafasi 40 za majimbo alizoahidiwa?

Ninacho msifia Mh.Mbatia ni mahili sana kuji-pretend, hata ukimwangalia body language yake anapo jaribu ku-address certain burning issues kuhusu Taifa letu usanii wake unaji-reveal dhahili - kumbuka kisanga cha juzi juzi hapa alipo sema alifukuzana na majambazi: mara majambazi walinifukuza wakani - overtake, baadaye na Mimi nikawa-overtake nikala kona, nikapigia Simu Police Patrol Mkoa mzima wa Kilimanjaro, Mara majambazi yalipo nikaribia yaligwaya maana yalijua na mimi nilikuwa na chuma ndani(mguu wa kuku) yaani ukusikiliza adithi nzima ilikuwa totally incoherent i.e burudani tosha!!!

Mpaka LEO najiuliza hivi mwandisi mwenzetu huyu ni kitu gani kulimsukuma ku-behave the way he did kwa kuwaletea Watanzania wenzake Mickey Mouse stories and for what if I may ask?

Sina nia ya kumsema vibaya Mh.Mbatia lakini yeye kama msomi anapashwa kuwa highly principled jinsi anavyo ji-conduct kwenye masuala ya kisiasa, hasiwe unpredictable kama shock wave za Tsunami.
 
Mbatia amechoka kupewa ahadi hewa,hapo anauma na kupuliza,

inaonyesha hata akipiga simu inapokelewa na mpambe;badala ya Bosi jiwe kama ilivyokuwa kabla

katikati ya maneno yake kuna tafsiri anapeleka ujumbe kwa mtu mkubwa, anataka akumbukwe kwa wadhifa kama Mrema,Mzee wa Parole
 
Mbatia amechoka kupewa ahadi hewa,hapo anauma na kupuliza,

inaonyesha hata akipiga simu inapokelewa na mpambe;badala ya Bosi jiwe kama ilivyokuwa kabla

katikati ya maneno yake kuna tafsiri anapeleka ujumbe kwa mtu mkubwa, anataka akumbukwe kwa wadhifa kama Mrema,Mzee wa Parole
 
Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia, ameshauri kufanyika kwa mazungumzo ili kupata mwafaka wa kitaifa utakaoliwezesha taifa kwenda mbele baada ya kuwapo kasoro mbalimbali katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 28, mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mbatia aliwataka viongozi wote wa kidini kutumia ndimi zao vizuri, kukubaliana kwamba masilahi ya Tanzania kwanza, mambo mengine baadaye na kamwe wasikubali kukichoma moto kichaka kilichowahifadhi.

Mbatia alisema kuwa hisia za wanasiasa kuhusu Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu haziwezi kuelezwa kwa maneno, bali watu wote wenye upendo na Tanzania wanaweza kuziona hisia hizo.

Hata hivyo alisema kuwa pamoja na watu mbalimbali kuwa na hisia hasi zinazokinzana na utu, maadili ya Kitanzania pamoja na tunu zilizoelezwa kupitia Wimbo wa Taifa za umoja na amani, zinaweza kuchoma kichaka ambacho wamejihifadhi ambacho ni Tanzania.

“Maneno hayatoshelezi kuelezea hisia, labda kwa kupitia nafsi. Hisia zetu kwa ujumla kuhusu mchakato wa tukio lililoitwa Uchaguzi Mkuu wa 2020, haziwezi kuwakilishwa kwa maneno, lakini wote wenye nia nzuri na mama yetu Tanzania kwa kupitia nafasi zao wanaweza kusikia au kuelewa hisia za wengi kwa muda huu.

“Licha ya kwamba kwa miaka 59, hatujaweza kumtumia vizuri mama Tanzania ili tuweze kujipatia mahitaji msingi kwa wote na kwa furaha ya kweli, sasa tuko kwenye kumwangamiza,” alisema Mbatia.

Alisema kuwa kwa miaka 28 chama chake kimekuwa kikiimba wimbo wa kupata Tume Huru ya Uchaguzi na kwamba sasa gharama zake zimekuwa kubwa.

“Maneno yetu sasa yanasikika dunia nzima, kwani dunia nzima imeshuhudia vitendo vinavyokiuka makubaliano yetu ya kitaifa ya miaka 28 iliyopita, kwamba maendeleo endelevu yanatokana na demokrasia ya vyama vingi vya siasa.

“Kama taifa tumekiuka hata makubaliano ya kitaifa, kwa mfano kufunga baadhi ya mitandao ya kijamii,” alisema Mbatia.

Aliongeza kuwa endapo Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere angekuwapo leo, angewaeleza kuwa hii si Tanzania na demokrasia aliyowaachia na angewataka kujikusanya waanze upya.

“Hii siyo kwa wanasaiasa peke yao, ni la Watanzania wote, hatuwezi kuangalia tu wakati mama anaamka na huzuni na kulala na hasira,” alisema Mbatia.
Wewe Mbatia na Lipumba hamna akili nzuri, bora Mbowe hajielewi, nini kiliwafanya msusie Bunge la katiba, tume huru ilipatikana, tatizo serikali tatu tu, vyote mkitaka kwa pamoja, wakati safari ni hatua, mngepata vichache vingine baadae.
Sasa ona mnavyo pambana na NEC, halafu mnakumbuka tume huru ambayo ilipita kwenye katiba mpya, ni wajinga na kufuata mkumbo!
 
Kitu kingine ambacho kitatuchewesha sana upinzani ni USHABIKI MAANDAZI , tuna jaribu kuona upinzani mwingine wowote kinyume na muono wa Chadema sio upinzani.

Hii ni vita ya kisiasa, kama tunaweza kuona upinzani ndani ya CCM ni faida kwetu, inakuwaje tunashindwa kuangalia upinzani Njee ya CCM ni bora zaidi na wakuuamini kuliko upinzani wa ndani ya CCM?

Bila kuchukua kila silaha inayo weza kumuumiza kisiasa CCM ni faida kwetu tutache lewa sana ? Siasa ni uwanja mpana sana wa mapigano , kuna beki, viungo, washambuliaji na waamuzi. Yote ni neema kwetu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom