Wanasheria tusaidieni hili la bodi ya mikopo

StingRay

JF-Expert Member
Jun 28, 2014
493
1,000
Kumekuwa na ubabe mkubwa mkubwa sana unaofanywa na serikali kupitia Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu kuhusu kulipa madeni ya mikopo ya 'tuition fees' na kufikia hata hatua ya kutu-brand majina ya "wadaiwa sugu" mara "defaulters" nakiwango cha kulipa kikiwa kikubwa sana. Mfano mtu alikuwa anadaiwa Tshs. 3,000,000/= nakufikia kudaiwa 7,000,000/=. Huyu mtu hakuwahi kukataa wala kugoma kulipa na taarifa zilikwishafika Bodi ili akatwe lakini ni uzembe wao wamekaa muda wote bila kukata halafu leo unamwadhibu mtu kwa kitu kisichokuwa na mkataba maalumu wa namna ya kukata mkopo. Inaumiza sana hii. Lakuni pia maagizo yanataka sheria ipitishwe ili makato yawe 15% badala ya 8% ilitokuwa ikitumika mpaka leo.

Naomba Sana wanasheria mtusaidie maana tunanyongwa na serikali yetu jamani.
 
yusuphfrancis

JF-Expert Member
Oct 26, 2016
431
500

Mliichaguwa wenyewe! Chaguo lenu milele, acha muisome number eeh! Ccm mbele kwa mbele
 
iparamasa

JF-Expert Member
Nov 14, 2013
13,443
2,000
mbali na hilo,asilimia 65 ya wanaoitwa wadaiwa sugu walishalipa,

na wengi wao hawana mikataba halali ya kukopa/kukopeshwa,watu wakiingia mahakamani wanawakaanga vizuri tu
 
Dumelang

JF-Expert Member
Aug 11, 2011
3,011
2,000
Mimi hili naona tukomae twende mahakamani, maana tulishaingia mkataba wakukatwa 8% leo wanataka kwenda kinyume na mikataba tuliosaini. Usishangae siku wakaja na riba hata kama zamani hatukusaini wala kuingia mikataba ya riba

Nadhani ni wakati wa wana sheria wa nchii kuzitendea haki taaluma zao.
 
Monsgnor

JF-Expert Member
Mar 26, 2012
538
1,000
Hapa ndipo napo mkumbuka Mchungaji Christopher Mtikila(RIP)....kesi kama hizi alikua ananunua halafu anazimiliki hapa lazima iwe tatu bila
 
jaji mfawidhi

JF-Expert Member
Feb 20, 2016
8,922
2,000
Mketa mada upo sahihi ila nakujibu kwa kifupi.

Ulikopa na sio ruzuku,lipa,mbona Benki ukikopa anawafuata kulipa na si wao kukukumbusha.

Pili,fomu mkopo ipo wazi,hamna mkopo usio na riba labda wa benki ya kiislamu.

Tatu,waambie na wadogo zako,kadri unavyochekewa kulipa deni linapanda.

Mwisho Lowassa alisema atawafutia deni mkakataa,sasa lipeni,
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom