Wanasheria CHADEMA: Mbowe hatakwenda polisi

Kisheria mtu anaenda polisi baada ya kukamatwa au anaandikiwa summons sio kupitia vyombo vya habari. Hiyo summons ingepelekwa makao makuu ya Chadema. Mbona Siro hafanyi hivyo? Ni tuhuma ya madawa kweli au Siro anatumika kisiasa kumnyanyasa tu Mbowe? Mbona wale 64 ambao hawajaenda hawafuatiliwi anafuatiliwa tu Mbowe?
 
WANASHERIA CHADEMA: MBOWE HATAKWENDA POLISI

WANASHERIA wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wamesema wamemshauri Mwenyekiti wao wa Taifa, Freeman Mbowe, asiende kuripoti polisi leo.

Akizungumza jana Mwanasheria wa CHADEMA, John Mallya, alisema Mbowe hatakwenda kuripoti polisi leo kwa sababu amefungua kesi ya kikatiba Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam na inaanza kusikilizwa Februari 21 mwaka huu.

“Mbowe haendi polisi, tumemshauri asiende kwa sababu kesi yake inaanza kusikilizwa Jumanne (kesho).

“Kama wanamhitaji, waje keshokutwa (kesho) Mahakama Kuu, watampata hapo,”alisema Mallya.

Kwa upande wake, Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, Tundu Lissu, alisema yuko Mwanza na hajawasiliana na Mbowe.

“Hapa niko Mwanza sijawasiliana na mwenyekiti, lakini kama nikiwasiliana naye, nitamshauri asiende huko polisi.

“Kwa hiyo, naweza kusema kilichofanywa na Kamishna Sirro si wito wa kipolisi bali ni siasa kama ambavyo alifanya Makonda kwa kutangaza majina ya watu hadharani.

“Wito wa polisi huwa ni wa kimaandishi, hawajamwandikia barua, hawajampigia simu.

“Hawa maafande wana namba zetu za simu sisi kama mawakili wa chama, kama wanamhitaji Mbowe kwanini wasitupigie simu mpaka watangaze kwenye vyombo vya habari,”alihoji Lissu.

Alipoulizwa kama Mbowe atakamatwa wakati wowote kuanzia sasa, Lissu alisema watalazimika kulishtaki mahakamani Jeshi la Polisi kwa kitendo hicho.

“Hatuwezi kukubali utaratibu huu, waache kufanya siasa, wakimhitaji mwenyekiti wetu wamwandikie barua,”alisema Lissu ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki.
naona jeshi la polisi limeamua kujidhalilisha lenyewe makusudically kabisa.
 
Eti polisi wangewapigia mawakili wa CHAMA.Hivi LISSU anajua sheria huyu? Hilo kosa alilofanya mbowe la madawa ya kulevya ni la kichama hadi chama kihusishwe na mawakili wa chama wahusishwe? KOSA LA KIBINAFSI WANAGEUZA LA KICHAMA.huyu ndio LISU MGOMBEA URAISI WA TLS!!!!!!!!!!! asiyejua kipi cha kichama na kipi cha kibinafsi

Sijui kwa nini hutaki kuelewa kuwa mbali na hayo wanapashwa kumpa spika taarifa ya kuhitajika kwa Mbowe Polisi, maana mbali ya kuwa M/Kiti wa CHADEMA ni mbunge na ni mkuu wa kambi rasmi ya upinzani bungeni. Pili ingekuwa ushahidi wanao bila shaka agekuwa ameisha kuwa arrested na kufikishwa mahakamani, kumbuka kuwa hakuna utaratibu wa kisheria wa kumuita mtuhumiwa kwa kutumia Luninga, magazeti au redio badala ya barua ya wito!!!!!!!!
 
upumbavu mwingine ndio huu wa kusema kosa la Mbowe kwani huyo mwizi wa vyeti ana ushahidi dhidi ya Mbowe?
Mbowe hana kosa mpaka mahakama itakapohamua vinginevyo.....kwani askofu Gwajima alikuwa na kosa gani na alitajwa na huo huo kilaza aliyeiba vyeti?
 
Kosa alilofanya MBOWE la madawa ya kulevya sio la kibunge na halina uhusiano na maswala ya ubunge wala na Ndugai
 
Mbowe aende basi polisi chap chap akathibitishwe kama anahusika au hahusiki kama alivyofanya Gwajima
 
upumbavu mwingine ndio huu wa kusema kosa la Mbowe kwani huyo mwizi wa vyeti ana ushahidi dhidi ya Mbowe?
Mbowe hana kosa mpaka mahakama itakapohamua vinginevyo.....kwani askofu Gwajima alikuwa na kosa gani na alitajwa na huo huo kilaza aliyeiba vyeti?
angiza unachotaka na kuja kulipa mkuu...
 
Kosa alilofanya MBOWE la madawa ya kulevya sio la kibunge na halina uhusiano na maswala ya ubunge wala na Ndugai
Nani kadhibitisha kosa hilo wakati hajafikishwa mahakamani na kuhukumiwa? wewe ulisoma sharia za wapi?????
 
njia ni nyingi za kufika taarifa kama namba yake kazima, mawakili wapo au watume barua ya wito ataipta. usiruhusu mihemuko ya watala itawale akili yako....
Kama kiongozi wa kitaifa, na hauna hata likizo kwa nini uzime simu, watu wanaweza kukutafuta uwasaidie hata baadhi ya mambo. Mfani kwa nini ujifiche, badala ya kukaa nyumbani au kuendelea na shughuli zako kana kwamba hakuna kilichotokea ili kama ukikamatwa kimakosa basi watu wakuone unavyoonewa.
 
Sijui kwa nini hutaki kuelewa kuwa mbali na hayo wanapashwa kumpa spika taarifa ya kuhitajika kwa Mbowe Polisi, maana mbali ya kuwa M/Kiti wa CHADEMA ni mbunge na ni mkuu wa kambi rasmi ya upinzani bungeni. Pili ingekuwa ushahidi wanao bila shaka agekuwa ameisha kuwa arrested na kufikishwa mahakamani, kumbuka kuwa hakuna utaratibu wa kisheria wa kumuita mtuhumiwa kwa kutumia Luninga, magazeti au redio badala ya barua ya wito!!!!!!!!
mkuu kunywa soda nakuja kulipa, vichwa vingine vinaelewa ila vinajidai havielewi.... usije ukakuta unabishana na mwenye PHD yake (pure head damage)
 
Kama kiongozi wa kitaifa, na hauna hata likizo kwa nini uzime simu, watu wanaweza kukutafuta uwasaidie hata baadhi ya mambo. Mfani kwa nini ujifiche, badala ya kukaa nyumbani au kuendelea na shughuli zako kana kwamba hakuna kilichotokea ili kama ukikamatwa kimakosa basi watu wakuone unavyoonewa.
mkuu nazania hakuna kitu kizuri kama ukijua sheria na taratibu zake, na hakuna kitu kibaya kama kujua sheria harafu unajitoa ufahamu eti huzijui..
 
lisu:watampigiaje simu wakati simu kazima?
Je wameshindwa kumwandikia barua? Mara kaandikiwa barua ya kuitwa polisi na kaenda?Iweje hii ya kutumia vyombo vya habari kuliko barua au cm?
Mbona list ya awamu ya tatu hawakuitaja kama mbili za awali?
Wanajua matope yao walioyafanya lkn wanajitoa akili.....
Kosa alilofanya MBOWE la madawa ya kulevya sio la kibunge na halina uhusiano na maswala ya ubunge wala na Ndugai
Kosa hajafanya Mbowe bali inasemekana Bills kuna biashara ya unga,yaani watu wakienda disko wanafanya na mengineyo.....
Je kwann wasianze na meneja kwanza kisha mmliki ndo afuate?
 
Je wameshindwa kumwandikia barua? Mara kaandikiwa barua ya kuitwa polisi na kaenda?Iweje hii ya kutumia vyombo vya habari kuliko barua au cm?
Mbona list ya awamu ya tatu hawakuitaja kama mbili za awali?
Wanajua matope yao walioyafanya lkn wanajitoa akili.....

Kosa hajafanya Mbowe bali inasemekana Bills kuna biashara ya unga,yaani watu wakienda disko wanafanya na mengineyo.....
Je kwann wasianze na meneja kwanza kisha mmliki ndo afuate?
Kuonyesha kwamba anapinga madawa ya kulevya nadhani angehairisha hata vikao vya bunge na kukimbia Polisi ili asaidie kizazi kinachopotea maana yawezekana miongoni mwa waathirika ni wafuasi wake.

mkuu tusitetee na ujinga. Sheria zimewekwa kwa faida ya wananchi sio kama vigezo vya kukwepakwepa maana haiendi kufungwa, bali ni interview na ikiwezekana anapimwa kidogo ili kuwaaminisha wafuasi wake nyie kwamba yuko safi na kama akikikutwa na madawa, nashauri mtafute intependent au source nyingine ambayo mnaiamini ithibitishe kisha ikiwezekana afungwe ili kusafisha taswira ya chama pendwa.

maoni yako please
 
WANASHERIA CHADEMA: MBOWE HATAKWENDA POLISI

WANASHERIA wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wamesema wamemshauri Mwenyekiti wao wa Taifa, Freeman Mbowe, asiende kuripoti polisi leo.

Akizungumza jana Mwanasheria wa CHADEMA, John Mallya, alisema Mbowe hatakwenda kuripoti polisi leo kwa sababu amefungua kesi ya kikatiba Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam na inaanza kusikilizwa Februari 21 mwaka huu.

“Mbowe haendi polisi, tumemshauri asiende kwa sababu kesi yake inaanza kusikilizwa Jumanne (kesho).

“Kama wanamhitaji, waje keshokutwa (kesho) Mahakama Kuu, watampata hapo,”alisema Mallya.

Kwa upande wake, Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, Tundu Lissu, alisema yuko Mwanza na hajawasiliana na Mbowe.

“Hapa niko Mwanza sijawasiliana na mwenyekiti, lakini kama nikiwasiliana naye, nitamshauri asiende huko polisi.

“Kwa hiyo, naweza kusema kilichofanywa na Kamishna Sirro si wito wa kipolisi bali ni siasa kama ambavyo alifanya Makonda kwa kutangaza majina ya watu hadharani.

“Wito wa polisi huwa ni wa kimaandishi, hawajamwandikia barua, hawajampigia simu.

“Hawa maafande wana namba zetu za simu sisi kama mawakili wa chama, kama wanamhitaji Mbowe kwanini wasitupigie simu mpaka watangaze kwenye vyombo vya habari,”alihoji Lissu.

Alipoulizwa kama Mbowe atakamatwa wakati wowote kuanzia sasa, Lissu alisema watalazimika kulishtaki mahakamani Jeshi la Polisi kwa kitendo hicho.

“Hatuwezi kukubali utaratibu huu, waache kufanya siasa, wakimhitaji mwenyekiti wetu wamwandikie barua,”alisema Lissu ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki.
Yule vuvuzela wao lizaboni anasema wameshamkamata
 
Back
Top Bottom