DOKEZO BBT LIFE (Chini ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi) imefeli, acheni kuwatumia vijana kwa maslahi yenu

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Nikiwa mmoja ya vijana walio katika program ya BBT LIFE iliyo chini ya wizara ya Mifugo na uvuvi napenda kusema haya nikiwa na uchungu wenye kuumiza, Vijana wenu mnawatumia kisiasa.

Kwanini nasema hivi?

Mnachokisema kwenye majukwaa na kinachotendeka huku ni tofauti, mfano mdogo alinukuliwa N/W wakati hua David Silinde akisema Kila kijana atapata faida ya Tsh 10M, vyombo vya habari vikaandika viongozi mkapata sifa nasisi huku mkatupa matumaini, vijana wengi mtaani wakaanza kutamani sana kushiriki ila sasa kumbe zilikua siasa.

Mh! Waziri Ulega akisimama kwenye majukwaa anasema vijana watapatiwa maeneo kwenye ranch za taifa, well sasa jiulize huko ranch za taifa hayo maeneo tunaenda kuyafanyia nini bila capital, hata ingekua tunaenda kulima tungehitaji pembejeo na mbolea.

Kwenye maonyesho ya Nane nane mmechagua vijana mkawapanga vya kuongea mbele ya Mh! Rais na watanzania kwa ujumla vitu vya uongo ili muonekane mnafanya kazi nzuri mzidi kupata maendeleo wakati hawa vijana huku ambao kutwa ni kuchunga ng'ombe na elimu zao wakiendelea kua masikini zaidi.

Mkasema kwenye maonyesho ya Nanenane kua BBT LIFE hadi sasa imetengeneza faida ya Tsh 74M, hii hesabu ya kinafiki sana, watu wakasifia bila kujua hiyo pesa ikigawanywa kwa Jumla ya vijana 240 kwa Muda wa zaidi mwaka utajua ni sifa pekee ndio wanazohitaji bila kutuangalia sisi ambao familia zetu zimejawa na matumaini makubwa kupitia speech zenu za uongo.

Viongozi mbalimbali wanatutembelea wakiwa na Camera zao wanaongea Speech za uongo ili kuwadanganya watanzania.

Kuna mengi sana ya kuongea ila naomba Viongozi mkijifikiria nyinyi basi tufikirieni na sisi, tumesoma sana, nina degree lakini nimekubali kujitoa kushiriki nikiamini itanitoa kwenye umasikini wa familia yangu.

Ikiwa mnaamini kuwa kila mnachokisema kwa watanzania ni kweli, Tusainisheni mkabata ambao unaeleza ni kipi tutafaidika nacho.

Waziri wa kilimo Mh! Husseni Bashe nampongeza sana, katimiza ahadi yake ila Mh! Ulega BBT LIFE inaelekea kutupoteza zaidi. Tunaenda mwaka wa pili sasa bila matumaini.

Wana JF tunaomba mtupazie sauti tunapotezwa kwa umasikini wetu
 
Mkuu

,Mkuu,pole sana.
Najua lazima hata kupata hiyo fursa kuna chochote kitu ulitoa pamoja na kuonesha kadi ya Uvccm.

Sasa swali langu kwako ni kwamba hayo hukuyatarajia?

Kule elimuni kila vijana wanaambiwa jitoleeni ili mpate ajira,una wafahamu wangapi waliopata ajira kwa kujitolea?
Pole sana,hujachelewa sepa kachukue bodaboda yako uendelee kushika fedha yako ijapo kidogo lkn ina uafadhari mkubwa.
 
Tafuta gape katika yote uliyoyaeleza litumie vizuri hapo ndo pakutokea..... (Lazima Kuna gape mahali)

Note: Sijakushauri uibe.

Kila la kheri.
 
Hizi project wali lenga kupiga pesa tu ata ile BBT ya BASHE ime feail vibaya sana vijana wana ondoka kuke shambani hawaoni future zaid ya wauza sura kuwatumia ..soon ata baki bashe na matrekta yake
 
Back
Top Bottom