Wanaovujisha taarifa na nyaraka muhimu za serikali, hii imekaaje?

Wee unadhani TISS wanafanya kazi na ccm tu????

Waliotoa hizo secret Info we unadhani ni raia wa kawaida????

Usalama wanafanya hivyo kwa maslai mapama ya nchi.... Huo ndio uzalendo nchi ikija kutaifishwa kwa madeni ya kizembe nani atakae laumiwa?? Serikali, jeshi la polisi, jwtz au usalama nani atakae laumiwa???
Boss umeongea point ya maana sana ambayo wengi hawaifikiri hii

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tundu Lissu wa Chadema amethibitisha kwamba anazo taarifa na nyaraka mbalimbali ambazo amepewa na baadhi ya watu wanaoaminika kwamba ni watumishi wa serikali.

Tundu Lissu amepewa nyaraka hizi na watu hawa kwa minajili ya kuzitumia kwa manufaa yake yaani kupalilia safari yake kisiasa na kujipatia umaarufu.

Ni hivi majuzi tu raisi wa Marekani Donald Trump alichukua hatua ya kurekebisha hilo ambapo baadhi ya wasaidizi wake wametuhumiwa kuvujisha taarifa mbalimbali kutoka ndani ya White House kwa waandishi wa habari na wapinzani wake.

Taarifa nyingi za serikali zina utaratibu wake wa kuzihifadhi na hupewa jina maalum la "top secret" au "classified information" kuzuia uwezekano wa kudukuliwa au kuibiwa,

Je, sheria inasemaje juu ya hili la kuvujisha taarifa na nyaraka za serikali kwa watumishi wa umma?

Je, yapi majukumu ya mdhibiti mkuu wa nyaraka za serikali na msemaji wa serikali au maofisa habari "information officers" kwamba labda kuna mahali wanapwaya?

Karibu tujadili bila kuingiza siasa.

Tunapojadili tuzingatia umuhimu wa kuhifadhi nyaraka na taarifa za serikali na wajibu wa maofisa habari na mdhibiti mkuu wa taarifa na nyaraka za serikali.
....hupewa jina maalum la "top secret" au "classified information" kuzuia uwezekano wa kudukuliwa au kuibiwa.Hivi tangazo la kukamata mali ya mdaiwa nalo linaangukia katika top secret?
Hili wala wasihangaike na Lissu au mtu mwingine yoyote.Tujirekebishe katika kuangalia mambo ya mikataba.Tunapigwa kila kukicha!!
 
Mimi naamini katika whistle Blowing ni mtu binafsi anatoka na anajilipua kutoa kila kitu.

Lakini hii naona ni kama vile "indirect whistle blowing" ambapo badi aletoa hizo nyaraka kwa Tundu Lissu hawezi kuitwa "Whistle Blower".

"Indirect Whistle blowing" inasimama kabisa kuwa "challenged legally" kwa sababu imetumia mtu wa kati.

Labda uniambie hii indirect whistle blowing inaruhusiwa kisheria.
Kumbuka LS hanaga kawaida ya kukurupuka maana kwa wanavyomwinda usiku na mchana anagekuwaga anakurupuka zamani sana wangeshamtia ndani na akapigwa mvua kadhaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Suala hapa ni kwamba ndege imezuiliwa mpaka serikali itakapolipa deni kwa hao wanaoidai sawa?

Kwa maana kwamba kama ipo pesa nusu imelipwa na bado serikali inajitahidi kulimaliza hilo suala halafu anatokea mtu anaingilia mchakati huo na kuweka kwenye public domain wewe unaona hiyo ni sawa?

Kumbuka haya majadiliano na namna ya kulipana yanafanyika nje ya nchi na siyo hapahapa Tanzania.
Aisee unaonekana unaijua sana serikali
Madaraja yetu yanapanda lini?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mmepewa dhamana na wananchi msimamie rasilimali zao, hatujawauzia nchi. Hivyo mnapofanya maamuzi msifanye mkadhani hiyo ni mali binafsi, yaani tumekupa tu dhamana halafu unataka kutuficha hadi sisi kwa vitu vinavyotuathiri moja kwa moja huu ni uhujumu. Wengine wangekuita mpumbavu kabisa.
 
Ni wazo zuri lakini kwa mwenye akili pia ataona
si vyema kiongozi mmoja kuwa na mamlaka makubwa kiasi cha kuitia nchi katika hatihati na madeni makubwa kiasi hiki kuna haja ya mabadiliko ili kuwe na usawa
Mbali na hapo haya yataendelea na serikali mpaka itashindwa kuendesha miradi yake

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kweli viongozi wetu hawafanyi jambo jema katika haya yanayoendelea,lakini yule anayevujisha siri inabidi atizame anayempa taarifa kama anaweza kuitoa katika njia nzuri,na sio mtu anatumia njia hiyo kwa manufaa yake.Na kinachoonekana mtu anatumia minajili yake kisiasa.
 
Ni kweli viongozi wetu hawafanyi jambo jema katika haya yanayoendelea,lakini yule anayevujisha siri inabidi atizame anayempa taarifa kama anaweza kuitoa katika njia nzuri,na sio mtu anatumia njia hiyo kwa manufaa yake.Na kinachoonekana mtu anatumia minajili yake kisiasa.

Mkuu, umeandika jambo la maana sana hapa na inabidi wale wanabodi wanaoenda nje ya mada wakusome vizuri.

Katika mada yangu nimegusia hilo la huyu kibaraka wa wazungu Tundu Lissu kutaka kutumia nyaraka na taarifa za siri alizopewa na baadhi ya watumishi wa serikali kutaka kujipatia umaarufu.

Pili, nimeuliza kwamba sheria inasemaje kwa watumishi wa serikali wanaovujisha nyaraka na siri za serikali kwamba imekaaje.

Na kwamba kuna madhara gani kwa upande wa serikali na watu kama Tundu Lissu na wapembe wake.

Nilitegemea kuwepo na mtiririko wa nguvu kutoka kwa wanabodi ambao wanaweza kutupatia mwanga juu ya hili na badala yake naona ni watu kama 10 hivi ambao wanaonyesha wananielewa ukiwamo wewe.

Wengine ama wanakwenda nje ya mada kwa kukosa hoja au wanaamua kuandka tu sentensi mbili tatu kupoteza muda.

Twende kazi jamani hili suala ni as it stands liko "very, very serious" na huko kwenye "corridors of power" kuna mshikemshike na watu wanapigana vikumbo..
 
Safi sana wewe mtu uliyewafahamisha hawa wezi,vilaza na mabashite wa ccm kua uzalendo ni kuvujisha tena si kuvujisha tu pumba za ccm,ila yale ya kuiponya nchi.Mungu akubariki na kukulinda na wakwenu wote ccm isiwakusudie uovu, wowote,Amen.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Deni la serikali sio siri, kila mtanzania anapaswa kulijua, kwa sababu kila mwananchi anawajibika kulilipa. Serikali inaweza kuzuia kusema kile tunachodaiwa kwa muda fulani, lakini wale wanaotudai hawawezi kufanya siri kile wanachokidai.

Shughuli ya mnada nao siyo siri, bombardia yetu ilikuwa iko mbioni kupigwa mnada huko Canada.

Pasipo Tundu Lissu hayo yote tusingeyajua. Lissu amesema ndio tukayajua, na sasa serikali na makada wa kijani wako busy kukiri kimtindo kile alichokisema Lissu kuwa ni ukweli.
 
Morali wa kufanya kazi vizuri na kuficha siri za serikali vitatoka wapi kama kuna uhakiki usioisha unaosababisha waajiriwa wengi kukosa stahiki zao na kama hakuna nyongeza za mishahara? Morali itatoka wapi kama mtu hajui atatumbuliwa lini na vipi? Mpaka madiwani wanawafukuza wakurugenzi, madaktari wanawekwa ndani na wakuu wa wilaya n.k. Kwenye hali kama hiyo nani atakuwa mtiifu kwa serikali?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mnazungumzia sana siri za serikali kuvuja akapewa Tundu Lissu. Kwani barua iliyoandikwa kuvunja mkataba husika ilikuwa siri? Au ukweli kwamba kulikuwa na kesi kuhusu madai ya hiyo kampuni si ulikuwa unajulikana? Siri ambazo hazitakiwi zivujishwe ni zile ambazo zikitolewa, usalama wa nchi unaweza kuwa mashakani. Kama kuna kiongozi ameharibu kazi, yeye atataka nyaraka za ushahidi wa uharibifu wake ziwe siri kwa ajili ya kumlinda yeye. Lakini hiyo siyo siri inayohusu usalama wa nchi bali ni usalama wa huyo kiongozi. Kwa hiyo, kabla ya kuendelea kujadili habari ya Lissu kupewa siri za nchi hebu tujiulize: Je, nyaraka za uvunjaji wa mkataba zinakuwaje ni siri za kuhatarisha usalama wa taifa?Je, ukweli kwamba hukumu.ilitolewa na nchi yetu ikadaiwa $ mil 25 ni siri inayoweza kuhatarisha usalama wa taifa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wee unadhani TISS wanafanya kazi na ccm tu????

Waliotoa hizo secret Info we unadhani ni raia wa kawaida????

Usalama wanafanya hivyo kwa maslai mapama ya nchi.... Huo ndio uzalendo nchi ikija kutaifishwa kwa madeni ya kizembe nani atakae laumiwa?? Serikali, jeshi la polisi, jwtz au usalama nani atakae laumiwa???
mbona umetoa Avatar picha yako Mkuu
 
Back
Top Bottom