Wanaovaa nguo za nje kuzomewa

Wanaovaa nguo za nje kuzomewa

Hao wanaozomea watalipwa na nani?

Kama hawatalipwa waatafanya kazi zao nyingine saangapi
Je huyo waziri atakua miongoni mwa wanaozomea?

Hii nchi inatia huruma jamani,eti huyo ni mtu aliyetakiwa atoe kauli kwa niaba ya serikali

Je ashatoa ufumbuzi wa suala la sukari?
 
Na nukuu, au kwa sabab wanasiasa ni ma-failure!!!!
Hence proved!
 
Natumai ubunifu huu uliotukuka wa Tanzania ya Viwanda hautaishia katika nguo tu. Itabidi iendelezwa kwa watakaotumia magari ya nje nao wazomewe, simu za kutoka nje nao wazomewe, na watakaotumia kompiyuta nao wazomewe, Watakaotumia vitabu vya kutoka nje chuo kikuu nao tuwazomee tu!
 
Jamani jamani jamani! ya sukari hadi kwenye nguo? kama tumeondoa ratiba ya chai na uji sasa tutaanza kutembea uchi! siku zinakuja!
 
Waziri wa Viwanda na Biashara Ndugu Charles Mwijage amesema kwamba kuanzia mwakani watu wote wanaovaa nguo za nje watazomewa ili kulinda viwanda vya nguo vya ndani.

Nafikiri kuzomewa ni kosa kisheria kwani nakumbuka kwenye uchaguzi mwaka jana kuna wanachama na wafuasi wa chama kimoja cha siasa walikuwa wakizomewa, wazomeaji walikamatwa na polisi.
 
Kuna wakati napata shida na kauli za viongozi wetu haswa wa awamu hii.Kana kwamba bado wapo kwenye kampeni na wanaowaambia watoto wadogo. IT IS NOT FAIR
 
Kama kweli hii ni kauli ya waziri, safari ya Tanzania ni ndefu.
 
Hawa Wa waheshimiwa naona wanaleta utani tumekosa sukari lakin tunakula miwa au tunakunywa soda kama mbadala je tukikosa nguo nin mbadala wake
 
Siamini kwamba upuuzi huu unaweza kutoka mdomoni mwa mtu mwenye kichwa chake!😵
 
Hakuna kituhapo wazir Wa KILIMO ulishasikia anasema chochote kuhusu KILIMO cha pamba?hayo ni maigizo kama mengine
Watu hukimbilia vya nje kwa kufatana na ubora wake, hivi vya ndani ili vitufae na tuachane na vya nje ni wao na viwanda vyao kuhakikisha ubora usiopingika na ikiwezekana wafikie viwango vile vya nje au zaidi, hapo wala hakutakuwa na haja ya kumzomea mtu, automatically watu tutajikuta tukivaa vya ndani na kuachana na vile vya nje! Nchi ina mikakati ya kuelekea kwenye mapinduzi ya viwanda, ngoja tuendelee kuomba yawe wanayoyakusudia.
 
Waziri wa Viwanda na Biashara Ndugu Charles Mwijage amesema kwamba kuanzia mwakani watu wote wanaovaa nguo za nje watazomewa ili kulinda viwanda vya nguo vya ndani.
e868fffc4dbdded809429a88d172c340.jpg
 
Safi kabsa ubarikiwe kwa kuwa na mawazo pevu ,huyo wazir bora angesema anaanza na kandambili lakini nguo Lol !!!!
Anayenikera mimi ni Waziri wa Afya, kwa nini naye hatangazi tumzomee kila atakayeenda kutibiwa nje ili kukuza hospitali za ndani?
 
Hv kuna kiwanda chochote cha nguo za kiume hapa nyumbani?
 
Back
Top Bottom