Wanaovaa nguo za nje kuzomewa

Wanaovaa nguo za nje kuzomewa

Hawa jamaa siku hizi wanachekesha sana. Huku kuna aliyesema askari watoe matairi wakauze na huyu anasema watu wazomewe. Siasa bwana!
 
Hii ina tofauti gani na ile ya kustopisha sukari ya nje ili kulinda sukari ya ndani? Hii ndio mikakati yenyewe ya kufufua viwanda?
 
ye mwenyewe amevaa nguo za wapi,rais wake,waziri mkuu wote wanavaa nguo za wapi naogopa kusema zaidi kwani sina uhakika kama ametoa hiyo kauli
 
Kama leo masikini tumekosa sukari kwa maamzi yao yasiyohusisha utafiti basi tujiandae kutembea uchi kama si kuvaa majani.

Suruali za vitenge watavaa wenye pesa sisi wa nguo za buku buku tununue nguo hizo sasa kwani hilo ni tangazo la kututayarisha.

Wao wanajiandaa kutucheka kwa kuwa wanajuwa nguo zetu zitakuwa na vilaka vyakutosha.

Kiukweli bado hatuna viwanda vya kutuvalisha watanzania wote labda kama anatengeneza fursa kwa muuza nguo na fundi chereani wachukue pesa yote ya mwananchi namaanisha manunuzi na kuweka viraka itakuwa ghali sana kama ilivyotokea kwenye sukari
 
Viwanda gani vya kulinda?? Au mwakani vitakuwa vimeshajengwa na kuanza uzalishaji?
 
Tatizo siasa zetu cheap sana ishu ni kwamba hvyo viwanda vitengeneze nguo bora na za kisasa watu watanunua ila huwez kutaka sympathy ktk dunia ya ushindani
 
Wakimaliza hapo wahamie kwenye magari. Watu wote wanunue magari yetu ya Nyumbu.
 
upload_2016-6-6_11-57-29.png
 
Hii "hapa kazi tu" yaweza wehusha baadhi ya makada na memba wa kabineti. Sijui wanaelewa maana yake? Tusijekuta hatimaye tunaongozwa kwa komedi waheshimiwa wakishindana kumzidi kasi ya "vilio" mwenye "msiba".
 
Ili kutatua tatizo la ukosefu wa ajira ni muhimu sana tuwe na viwanda vya nguo. Kiwanda chochote cha nguo lazima kiwe na wafanyakazi wengi.

Have we lost all sense of self worth? Haiingi kabisa akilini kwetu kwamba tunaweza kuwa na viwanda vitakavyotengeneza nguo nzuri? Na hatuongelei mitindo (design) za ndani bali nguo za kutengeneza vitambaa hapa kwetu na kushona mashati, suruali na nguo za wanawake nchini kwetu.

Ningependa sana nivae nguo za vitambaa vilivyotengenezwa Tanzania na kushonwa na mafundi nguo wa Tanzania. Nashindwa tu kuzipata.

Tubadilike. Tujue kwamba ni sahihi waziri apange mikakati ya kuwepo viwanda vya nguo na kulinda soko lake.
 
Duh! Waziri mzigo mwingine huyu ambaye hakustahili kuwa hata Mbunge wachilia mbali kuwa Waziri.

Waziri wa Viwanda na Biashara Ndugu Charles Mwijage amesema kwamba kuanzia mwakani watu wote wanaovaa nguo za nje watazomewa ili kulinda viwanda vya nguo vya ndani
 
kwa hivo tutadunda mitaani na nguo za ndani tu? Uchizi kweli.
 
Sukari Hali Ndio hii, mnataka mrejeshe kaniki? Nchi ya viwanda haiwezi kujengwa kwa mwaka mmoja. Musikurupuke
 
Rubbish! Hii serikali imetufanya sote tuna akili finyu. Waambieni wanenu na wake zenu acheni kuingilia maisha ya watu ! Mara tuchomoe matairi ya gari mara sukari ikikamatwa itagawiwa bure! Magu's government give us a break for crying out loud!
 
Back
Top Bottom