Uchaguzi 2020 Wanaovaa nguo za CCM kwenye mkutano wa Kampeni kwanini baada ya mkutano huzivua kabla ya kurejea makwao?

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
762
6,980
Mikutano mingi ya Chama cha Mapinduzi inapomalizika eneo la tukio watu wenye uniform za chama upotea au kuzibadilisha na hivyo kutoonekana wakiwa wamezivaa kurejea makwao.

Miaka ya nyuma mtaani watu walikua wanaona fahari kuzivaa kuanzia bodaboda, mama ntilie, wajumbe na watu wengine. Ilikuwa sawa na mchuano wa Simba na yanga panapotoa droo ambapo kila mmoja uvaa jezi kwenda nayo hata bar au maskani.

Ni kweli kwamba Hawa wanaovaa hizi nguo wanavaa kwakuzipenda au wanavalishwa? Kama wanavalishwa kwanini wanaowavalisha wasiwape masharti ya kwenda nazo nyumbani bila kuzivua?

Hata bodaboda wenye bendera au hata kofia mtaani ambao ni wana CCM wanakosekana? Afadhali vyama vingine ambavyo wapenzi wao watasema wanawindwa na dola, CCM kwanini mmekosa imani na nguo zenu?

Mtu kama anaogopa kuvaa jezi mtaani kwake unamtenganishaje na msaliti? LIPO TATIZO SEHEMU, TULIKOSEA
 
Wakati wa kwenda

JamiiForums-1617535992.jpg
 
Mwaka huu ccm wamekosa mpaka mawakala baadhi ya maeneo ndio ujue sasa kwamba hawana Chao
Juzi nilishangaa nikuzungumza na rafiki yangu mmoja wa siku nyingi sana ambaye ni kiongozi wa CCM ndani ya mkoa (simtaji Ila akisoma hii atanikumbuka) na namnukuu,
"Hata sie wenyewe kuipigia kura ccm sasa ni ujinga maana haipo tena sasa kuna kitu kingine kinaitwa magu, tutawapa kura wale wabunge wetu bora lakini vibaraka wake tunatosa. CCM haitakufa kwa kukosa utawala 2020 bali itatupa nafasi ya kuwafagia hawa washamba"
Sasa kuna kitu hapo kimebaki hapo?
 
Mimi pia nilikutana na kiongozi mmoja wa CHADEMA ambaye tulikuwa wote mahali nikamuuliza kwa mshangao je, na wewe uko huku? Akanijibu kuwa anaganga njaa kwenye opportunities na kwamba wapo wengi huko...akasema hawezi kumpa kura kibaraka na mpenda ushoga..tehteh
 
Mimi pia nilikutana na kiongozi mmoja wa Chadema ambaye tulikuwa wote mahali nikamuuliza kwa mshangao je, na wewe uko huku? Akanijibu kuwa anaganga njaa kwenye opportunities na kwamba wapo wengi huko...akasema hawezi kumpa kura kibaraka na mpenda ushoga..tehteh
Ahahaha
 
Mleta mada ndio maana huolewi umebaki nungayembe mwongo mkubwa wewe kwa hiyo hizo nguo huwa wanavua mkutanoni na kurudi uchi au?

Wewe kuolewa sio rahisi
 
Mimi pia nilikutana na kiongozi mmoja wa Chadema ambaye tulikuwa wote mahali nikamuuliza kwa mshangao je, na wewe uko huku? Akanijibu kuwa anaganga njaa kwenye opportunities na kwamba wapo wengi huko...akasema hawezi kumpa kura kibaraka na mpenda ushoga..tehteh
Umejaribu kufananisha lakini umekosa akili kuwa CHADEMA hakuna opportunities wala masirahi.Ukiona mtu yuko Chadema ni kwa moyo wake wote maana hata kampeni tunachagia,hatuna pesa za kugawa

Tafuta mfano Mwingine malaya wa kisiasa
 
Back
Top Bottom