CANCER Wewe humjui Magufuli hata kidogo. Mimi kwetu ni Biharamulo, kabla ya kutengwa na kuanzishwa jimbo la Chato tulikuwa na jimbo la Biharamulo likijumuisha Chato na Biharamulo na mwaka 1990 Magufuli aligombea akitokea Chato na mpinzani wake alikuwa marehemu Phares Kabuye, Magefuli alishindwa vibaya na Kabuye kwa kupata kura chache sana Biharamulo, ila tangu hapo akajenga chuki na watu wa Biharamulo.
Mwaka 1995 lilianzishwa jimbo la Chato na yeye kufanikiwa kuwa mbunge na baadae Waziri, ila cha kushanganza amefanya vitimbi vikubwa sana vya kuhakikisha kila project inayoihusu Biharamulo ya Miundombinu haifanikiwi. Barabara ya Mwanza-Bukoba ilikuwa inapita Biharamulo ila yeye kaamua kuipitisha Chato kitu ambacho si kibaya ila kibaya ni kuwa kuna 70km za barabara ya vumbi mpk Biharamulo na ni eneo hatarishi kwa majambazi na jamaa ameapa hatoweka rami kwa sababu watu wa Biharamulo walimkataa (inakuchukua zaidi ya masaa mawili distance fupi km hii).
Sasa huyu jamaa akiwa rais akaamua kulipa visasi kwa watu wote wenye anaofikiri walitofautiana nae unadhani itakuwaje? Huyu nae bado kwani sie tunamjua vizuri na ndo maana alipigana Chato ijitenge na mkoa wa Kagera na akawa anataka makao makuu ya mkoa mpya wa Geita yakae Chato ila imeshindikana. Huyu bwana ni mbinafsi.
Na mnastahili mbaki bila lami hivyo hivyo. Mmewezaje kumwacha mpiganaji kama huyu na kwenda kuchagua watu wasio na uwezo. Huoni kama mmetucheleweshea maendeleo ya Taifa kwa kumchelewesha Magufuli kuja kututumikia..?