We Mleta hii hoja hujamsikia Dkt Slaa mchana huu kwenye Thread iliyoanzishwa na 'gamba'kawakataza kujadili huu Upuuzi jengeni chama kuanzia ngazi ya shina badala ya kushinda humu kuanzisha habari za kujipendekeza. Mnakera sana kwa hili nipo pamoja na Babu!
Wewe Songoro kuna wakati unaweka point za maana kwenye hizi thread. Lakini somewhere unajikuta huyo, tayari usharudi kutetea chama chako. Hapa kwa mfano, madai yako kuwa kuna watu wanashindahumu
kuanzisha habari za kujipendekeza. Maudhui ya sentensi hii ni kukatisha watu tamaa kuweka mawazo yao humu kwa hofu watakuwa wanajipendekeza. Hii sentensi yako imekaa kipropaganda sana ujue. Waache watu watoe mawazo yao bila hofu ya kujipendekeza. Kwanza hata wakijipendekeza kuna tatizo gani. Kujipendekeza ni sehemu ya siasa, and its OK.
Wewe mwenyewe hapo ulipo unajipendekeza Makao Maku Madogo Lumumba wakutoe ngazi ya wilaya labda pengine wakupe Mkoa.
Now back to the Issue: CCM ina mtandao mkubwa sana wa matawi, kwa hiyo ni tishio kwa yeyote atayetafuta nafasi ya Urais. Nani atafaa watajua wao. Lakini ukweli utabaki palepale yeyote watayemchagua atakuwa jiwe gumu kwa sababu wana uzoefu katika mambo haya, wana fedha--halali na haramu, wana dola. Hata wakimweka Wasira bado itabidi vyama vya upinzani vijipange vizuri kumkabili.
Kwa upande wa pili, tatizo la CHADEMA halitakuwa kwenye nafasi ya Urais. Watu wamekichoka sana CCM atayewekwa na CHADEMA kwenye nafasi ya Urais hatakuwa na tatizo sana. Kazi kubwa kwa upande wa CHADEMA itakuwa kwenye Ubunge. Huwezi kuunda Serikali bila Wabunge wa kutosha. Kwa hiyo chama hiki cha Ushindani kina kazi kubwa sana kuandaa serikali kwa maana ya kuandaa wabunge.
CCM wameliona hili wanakipunguzia CHADEMA kasi ya kuunda serikali imara 2015 kwa njia ya kukipunguzia kasi vijijini. Kwani kwa kufanya hivyo watakosa wabunge wa kutosha, na hivyo itakuwa vigumu kuunda serikali yenye nguvu.
Tukio la kumpiga bomu mwandishi pale Iringa, kulifungia Mwanahalisi na haya matukio ya Mabwepande na kukataza maandamano vimeleta hofu sana miongoni mwa wananchi. Wanai slow down CHADEMA kupata wabunge 2015 and therefore kushindwa kuunda serikali imara wakati huo.
Songoro, nakuhakikishia wakati huu ni mwafaka kwa CHADEMA kuidhibiti hofu ya polisi, TISS na JW kama wanataka kupata idadi ya kutosha ya wabunge 2015. M4C ni lazime isidumazwe na kitu chochote. Ukumbuke msemo huu: The most fearful enemy of any man or woman is fear itself.
CHADEMA MUST OVERCOME FEAR kuunda serikali 2015.