Wanaoutaka urais 2015: Yupi anafaa?

CANCER

Member
Feb 21, 2012
36
20
Kwa hali inayoendelea hivi Tanzania inatia shaka bado miaka mitatu kufika uchaguzi mkuu wa uraisi na wabunge 2015, lakini kila kukicha mapya yanajitokeza kwa watu kutaganza nia ya watu kujitangazia kuwa na sifa za kuutaka uraisi, mmoja alisema anasubiri Mungu amuoteshe na kudhihirisha akasema ana maadui 11 ambao 2016 mara baada ya kuoteshwa watakibiria kenya, hiyo inaonyesha dhamira iliyojificha na ulipaji visasi, bado kuna magwinji mengine ambayo yalishaanza harakati zamani kama EL, SS, FS, ambao wanamitandao ndani ya chama chao cha chukua chako mapema.

Ukija kwa upande wa CDM nako mambo yameanza kupamba moto mara nina sifa za kuwa amri jeshi mkuu wa nchi ili hali hata familia hana , mara kiongozi mkuu wa chama anataka, mara mheshimiwa Dr. Slaa, vile vile inetokea wengine wanasema tangu uhuru hatujatoa raisi wakati tuna uwezo, mara tunataka mwislam.

Hizi sio ishara nzuri vile vile kiongozi ambaye nimzuri sio lazima ajipe sifa mwenyewe kuwa anaweza kusema hivyo vyote alivyokuwa anafanya ni unafiki , vile kiongozi kuweza kumpita na kusema ni mwadilifu na mzalendo lazima awe amefanya kazi na kudhibitisha hilo bila shaka na sio kuongea na kukosoa tu, mfano bunge lililopita kilango, mwakembe, ole sendeka, sita tulifikiri ni wazalendo wanatetea watanzania lakini leo hii sio, vile vile zito kasi yake sio ile.

kwa hali hiyo tusidanganyike na porojo za kuwa naweza ili hali ni njaa tu. Kwa hali tuliyonayo na kuangalia ukomavu wa siasa Dr. Magufuli anafaa kuwa raisi ila sio kupitia CCM. Anasifa na amedhihilisha kwa kuwa na misimamo akiwa serikalini , sio mdini, mkanda wala mjenga mitandao.
 
Aanze na wizara yake kwanza, tuone.[/QUOTE
Nafikiri wewe ni shahidi wa anayofanya kwenye wizara yake ana misimamo thabiti hateteleki anafanya kazi bila upendeleo , anapanga miradi bila ubaguzi na hachezi na wafanya kazi wazembe ndo maana miundo mbinu chini ya uongozi wake imekuwa nzur ukilinganisha na wakati wa kawambwa.
 
Magufuli dhaifu sana,hana maamuzi.kama huamini nenda jimboni kwake uone panavyitia hurumaa.
 
ninichojua kiongozi mzuri hapimwi kwa uwezo wake wa kujenga hoja majukwaani...ule utaratibu wa zamani wa usalama wa taifa kufuatilia nyendo za vijana tangu wakiwa mashuleni sijui uliishia wapi?? zamani ilikua ukionekana una mashiko kwa jamii kulikua na watu wana trace background yako toka kijijini kwenu , familia yako, umesoma wapi na mambo kama hayo NDIO KILIKUA KIPIMO KIZURI CHA UONGOZI
 
CANCER Wewe humjui Magufuli hata kidogo. Mimi kwetu ni Biharamulo, kabla ya kutengwa na kuanzishwa jimbo la Chato tulikuwa na jimbo la Biharamulo likijumuisha Chato na Biharamulo na mwaka 1990 Magufuli aligombea akitokea Chato na mpinzani wake alikuwa marehemu Phares Kabuye, Magefuli alishindwa vibaya na Kabuye kwa kupata kura chache sana Biharamulo, ila tangu hapo akajenga chuki na watu wa Biharamulo.

Mwaka 1995 lilianzishwa jimbo la Chato na yeye kufanikiwa kuwa mbunge na baadae Waziri, ila cha kushanganza amefanya vitimbi vikubwa sana vya kuhakikisha kila project inayoihusu Biharamulo ya Miundombinu haifanikiwi. Barabara ya Mwanza-Bukoba ilikuwa inapita Biharamulo ila yeye kaamua kuipitisha Chato kitu ambacho si kibaya ila kibaya ni kuwa kuna 70km za barabara ya vumbi mpk Biharamulo na ni eneo hatarishi kwa majambazi na jamaa ameapa hatoweka rami kwa sababu watu wa Biharamulo walimkataa (inakuchukua zaidi ya masaa mawili distance fupi km hii).

Sasa huyu jamaa akiwa rais akaamua kulipa visasi kwa watu wote wenye anaofikiri walitofautiana nae unadhani itakuwaje? Huyu nae bado kwani sie tunamjua vizuri na ndo maana alipigana Chato ijitenge na mkoa wa Kagera na akawa anataka makao makuu ya mkoa mpya wa Geita yakae Chato ila imeshindikana. Huyu bwana ni mbinafsi.
 
Mgeni akija kwenye hii nchi akasoma magazeti na kuangalia tv atafikiri uchaguzi wa hii nchi ni mwaka huu kumbe tuna miaka mitatu.. Baadhi ya hao wanaotaka urais wanaweza hata wasiwe hai kipindi hicho.. Hawa presidential hopefuls ningewapa more respect kama wangefikiria zaidi maswala ya wananchi kuliko maswala yao binafsi..

Tumewapeleka wabunge bungeni sio kuanza kuongelea nani anafaa kua rais bali mpo huko kututatulia maswala muhimu kama maji umeme huduma za afya elimu bora na vinginevyo sasa hayo mambo yamewashindwa ndo maana bungeni saivi watu ka akina mwigulu wanaongea pumba kwa sababu hakuna cha maana cha kuongelea sioni kwanini mbunge alipwe 200000 kwa siku kazi yake iwe kubeza na kutukana wabunge wenzake
 
Wadau;
Watu wenye dhamira ya dhati kabisa kabisa ya kuifanya nchi hii kuendelea Ki- Viwanda na Ki- Uchumi wamebakia kuwa Madereva taxi na Vinyozi tu, Wengine woote ni wachumia tumbo. Period !
 
Rais Anatoka kwenye system wanamtandao wenyewe wanakwambia sasa sijui ni yupi yetu macho
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom