Wanaoutaka urais 2015: Yupi anafaa?

Kwa kuwa tumeisifia sana tabia ya rais aliyeko madarakani ya kuomba omba, ina ashiria kuwa kuomba kunainufaisha sana nchi yetu, kwa msingi huo naona kabisa potential candidate anakuwa "MATONYA"

Ni mbunifu katika kuomba!

Ni mstahamilivu anapoomba!

Anaushawishi mkubwa, inakuwa rahisi kumhurumia!

Anajua pa kuomba!!

Tumuunge mkono MATONYA tuachane na kina zito wazito haoooooo.
 
Kwa hali inayoendelea hivi Tanzania inatia shaka bado miaka mitatu kufika uchaguzi mkuu wa uraisi na wabunge 2015 , lakini kila kukicha mapya yanajitokeza kwa watu kutaganza nia ya watu kujitangazia kuwa na sifa za kuutaka uraisi , mmoja alisema anasubiri mungu amuoteshe na kudhihirisha akasema ana maadui 11 ambao 2016 mara baada ya kuoteshwa watakibiria kenya , hiyo inaonyesha dhamira iliyojificha na ulipaji visasi, bado kuna magwinji mengine ambayo yalishaanza harakati zamani kama EL, SS, FS, ambao wanamitandao ndani ya chama chao cha chukua chako mapema.....

Umenigusa sana kaka pamoja kuwa mi ni mpizani ila huyu jamaa anafaa! under employment of comparison with in CCM!
 
Aliuza nyumba za serikali ambazo hakuzijenga,je barabara alizojenga si hatasita kuziuza akiwa Rais?Don't trust a thing!
 
tatizo tunafikiri viongozi wazuri ni wale wanaotembea na waandishi wa habari kuonyesha jinsi wanavoweza
1. kubomoa nyumba za wanyonge walidunduliza miaka 30 kuijenga huku akiwaacha waliojenga kando ya bahari na mahekalu yaliyojengwa maeneo ya wazi
2. kuwakamata na kuwaonyesha kwenye vyombo vya habari wala rushwa wa mizani na kuwaacha mapapa kama wa EPa nk

3. kutuaminisha kuwa matatizo ya nchi hii yanasababishwa na wala rushwa wa mizani, wahandisi wala rushwa kwa makandarasi wadogo, wanaojenga pembezoni, na wla si mafisadi papa

naomba nimnukuu mheshimiwa JACKSOM MWAKWETA WAKATI AKIMJIBU MREMA BUNGENI MWAKA 1986, MH. MREMA KUNA MAMABO MENGI MAZURI YANAYOFANYWA NA BAADHI YA VIONGOZI WA TAIFA HILI BILA KUYASIKIA, WANANCHI HAWAHITAHI PROPAGANDA BALI MAENDELEO YA KWELI.

Watu mnasema pinda siyo waziri mkuu mzuri simply kwa kuwa yeyr haandamani na vyombo vya habari akisema uongo kama akina maghufuliu na lowasa.

mtakuja kukumbuka siku moja "a populist cannot become a good leader, but a dictator"
 
ninichojua kiongozi mzuri hapimwi kwa uwezo wake wa kujenga hoja majukwaani...ule utaratibu wa zamani wa usalama wa taifa kufuatilia nyendo za vijana tangu wakiwa mashuleni sijui uliishia wapi?? zamani ilikua ukionekana una mashiko kwa jamii kulikua na watu wana trace background yako toka kijijini kwenu , familia yako, umesoma wapi na mambo kama hayo NDIO KILIKUA KIPIMO KIZURI CHA UONGOZI
hey hawahwa akina Rama wanaolimboka watu walikuwa wanafanya uchunguzi wa vijana?????????mwe twafwaaa.
 
CANCER Wewe humjui Magufuli hata kidogo. Mimi kwetu ni Biharamulo, kabla ya kutengwa na kuanzishwa jimbo la Chato tulikuwa na jimbo la Biharamulo likijumuisha Chato na Biharamulo na mwaka 1990 Magufuli aligombea akitokea Chato na mpinzani wake alikuwa marehemu Phares Kabuye, Magefuli alishindwa vibaya na Kabuye kwa kupata kura chache sana Biharamulo, ila tangu hapo akajenga chuki na watu wa Biharamulo. Mwaka 1995 lilianzishwa jimbo la Chato na yeye kufanikiwa kuwa mbunge na baadae Waziri, ila cha kushanganza amefanya vitimbi vikubwa sana vya kuhakikisha kila project inayoihusu Biharamulo ya Miundombinu haifanikiwi. Barabara ya Mwanza-Bukoba ilikuwa inapita Biharamulo ila yeye kaamua kuipitisha Chato kitu ambacho si kibaya ila kibaya ni kuwa kuna 70km za barabara ya vumbi mpk Biharamulo na ni eneo hatarishi kwa majambazi na jamaa ameapa hatoweka rami kwa sababu watu wa Biharamulo walimkataa (inakuchukua zaidi ya masaa mawili distance fupi km hii). Sasa huyu jamaa akiwa rais akaamua kulipa visasi kwa watu wote wenye anaofikiri walitofautiana nae unadhani itakuwaje? Huyu nae bado kwani sie tunamjua vizuri na ndo maana alipigana Chato ijitenge na mkoa wa Kagera na akawa anataka makao makuu ya mkoa mpya wa Geita yakae Chato ila imeshindikana. Huyu bwana ni mbinafsi.
Magufuli urais hawezi. Hapatakalika. Anafaa kuwa waziri mkuu. Lazima awepo mtu wa kumfumga speed gavana. Bila speed gavana mkfl ni hatari
 
Last edited by a moderator:
tatizo tunafikiri viongozi wazuri ni wale wanaotembea na waandishi wa habari kuonyesha jinsi wanavoweza ... "a populist cannot become a good leader, but a dictator"
You're perfectly right. Nimekuwa najuiliza mtu kama Zitto ambaye yuko tayari kumtumia au kutumiwa na mtuhumiwa wa kupanga mauaji ya viongozi wenzake wa CDM ( I presuppose that Zitto knew and was part of this satanic plan ) ili tu apate urais, akiupata si atakuwa dictator mbaya kuliko alivyokuwa Hitler?

Magufuli hakujua hata Igunga anatakiwa kukampeni vipi akaishia kumharibia Kafumu. Akipewa uarais itakuwaje?
 
Amekutumu au umejituma? Anayemjua rais ni Mungu maana hakuna binadamu mwenye uwezo wa kujua kitakachotokea hata sekunde moja ijayo. Una uhakika gani kuwa mtu wako atakuwa hai, atakubalika chamani mwake hata kwa wapiga kura na anautaka kama unavyodhani?
 
Mpaka sasa sijaona anayefaa kuwa Rais wetu kwa wote waliojitokeza katika vyama vyote.. Urais siyo ushabiki na uwezo wa kuongea..ni uwezo wa kuchanganua na kuona mbali, tena uwezo wa kufanya maamuzi sahihi na kuyasimamia..bila kuyumbishwa na siasa za chama, dini, ukanda wala kabila lako..
Sasa mnavyokuja kutuambia lazima atoke wapi,sijui nini kamwe hatutaweza kuisogeza Tanzania yetu katika maendeleo kama tutaendelea kuwazia ujinga wa kikoloni vichwani mwetu.
 
Rais anayefaa hadi sasa hayupo kati ya hao waliojitokeza, tunataka rais ambaye:-
1. Analetewa muswada asaini wa kumnyima mfanyakayi asichukue hela yake ya pension yake hadi afe/awe 55yrs, yeye anakataa na kutoa agizo kuwa wafanyakazi waweze kukopa bila riba hela yao inayokatwa na kuwekwa na hii mifukoa
2. Rais ambaye watendaji aliowachagua hawawajibiki ipasavyo ana wawajiaisha rightaway
3. Vipaombele kwake ni maisha ya wananchi wa kawaida si wachache wenye nacho
4. Asiwe muongeaji sana maana atakosa muda wa kufanya kazi
5. Asiwe kiguu na njia
6. Asiwe mbinafsi na mbi'marafiki
 
Amekutumu au umejituma? Anayemjua rais ni Mungu maana hakuna binadamu mwenye uwezo wa kujua kitakachotokea hata sekunde moja ijayo. Una uhakika gani kuwa mtu wako atakuwa hai, atakubalika chamani mwake hata kwa wapiga kura na anautaka kama unavyodhani?
Hajanituna nimejituma kwa kusukumwa na dhamira ya haki kwa kuona utendaji kazi wake usiotetereka
 
Back
Top Bottom