" Uwekezaji nchini Tanzania umekuwa ni tatizo na kwakweli mabadiliko makubwa yanahitaji hapa. Makampuni yanafunga, Wafanyabishara wanashindwa kuendelea huku Uchumi wa Tanzania ukiathirika pakubwa, Ajira nyingi Kutoweka, Mzunguko wa Pesa kuwa Mgumu kupelekea Kilio cha kila Siku kwa Wananchi kuwa Mifuko yao inazidi kuwa mitupu tu "
Tumempenda Rais Samia Suluhu Hassan siyo kwa bahati mbaya tu bali kwa dhamira yake Kuu kwa Watanzania wengi, kuwa ni Mtu aliyejua Kilio Kikubwa cha Watanzania ( cha Ukata mkubwa Mifukoni )
Hatahivyo haongozwi Kimihemko, ila anaenda na Slogan nzuri ya Watu makini ya ' Slow but Sure ' ambayo naamini itamsaidia na atatuongoza vyema tu kabisa.