Wanaotaka kutoka kimaisha, fani ya ufundi bomba ni mkombozi wao

Profesa ntare nkobe

JF-Expert Member
Feb 5, 2018
6,957
8,073
Kwa wale wanaotaka kutoka kimaisha au wana interest na ufundi basi hii fani ya Plumbing ni mkombozi kwao, ina fursa nyingi sana za kujiajiri na kuajiriwa. Kwa utafiti wangu mafundi bomba baadhi yao hawajasomea hii kazi na wanaifanya kwa kubatisha sana, wachache ndio wanaiweza lakini pia fundi bomba aliyesoma anaweza kufanya kazi kwenye gas na mafuta. Soko la ajira ni kubwa sana.

Kama una ndugu mtoto ambaye unapenda akasome ufundi mpeleke kwenye ufundi bomba plumbing vyuo vinavyotoa plumbing sio vingi sana, ni vichache sana baadhi ninavyojua kwa Dar na Pwani ni
Shirika la elimu Kibaha
VETA Mwanza
VETA Iringa.
VETA Kigoma
 
fafanua kwa kina fursa zilizopo Mkuu
Fursa ni kujiajiri hapa kila siku watu wana jenga kuna kufunga vifaa vya usafi namanisha vyoo masinki na mabeseni na kufunga mabomba kuweka choo kimoja kilicho kamilika ni elfu70 vile vile una weza kuajiliwa katika mabomba ya mafuta au gas au kuajiliwa katika idara mbali za serikali na vile vile maji bado ni shida kuna miladi mbali mbali ina anzishwa vijijini na mjini ina itaji mafundi hii fani inalipa sana kumbuka mafundi bomba ni wachache sana na vyuo vinavyo toa plumbing ni vichache sana
 
Back
Top Bottom