Wanaosema Rais Samia mpaka 2030 wanajua maana ya demokrasia? Je, somo la Awamu ya Tano halikueleweka?

The lost

JF-Expert Member
Jul 3, 2017
2,695
8,209
Wakuu wameanza tena,

Wanasema mama mpaka 2030 na atakayempinga atakiona. Najaribu kuwaza hawa watu tunaposema "Kila amtegemeae mwanadamu amelaaniwa" hawaelewi? Awamu ya Tano walianza hivihivi, wakamtia kibri JPM wakakufuru na mwisho laana ikawa juu yao.

Ameanza Kigwangala, jana tukamsikia tena Mwenyekiti CCM Mara na hawafanyi kwa bahati mbaya! la hasha bali ni kujaribu kuonesha ni kwa namna gani wamepotoka. At the end their regime will be fated to end badly.
 
Kuna watu fulani fulani wanapitishwa kipindi kigumu sana na mama Samia.

Msipokuwa makini mwaka huu mtakunya moto.
 
Akili zao ndogo Maana wanafikiria Kuteuliwa tu, hasa huyo Kigwangala alikuwa bado na ndoto za uwaziri; Wanatumia style ile ya kusifia sifia na kujipendekeza pendekeza aliyowazoesha Boss wao Aliyeendazake bila kuwaaga.

Bado hawajaamini inawapa shinda sana na itaendelea kuwatesa maana akili zao ni za Kujipendekeza pendekeza ili kukumbukwa. Kigwa hafai tena kuwa hata kwenye kamati yoyote ya Kitaifa, yeye aendelee kuwawakilisha wana Nzega huko Bungeni.
 
Kinachosikitisha zaidi ni kama hakutakuwa na wagombea wengine kutoka vyama vingine.

Labda kwa vile wanajua mgombea wa chama chao huwa anashindishwa tu hata kama kura hazitoshi.
 
Wakuu wameanza tena, wanasema mama mpaka 2030 na atakayempinga atakiona. Najaribu kuwaza hawa watu tunaposema "Kila amtegemeae mwanadamu amelaaniwa" hawaelewi? Awamu ya tano walianza hivihivi, wakamtia kibri JPM wakakufuru na mwisho laana ikawa juu yao. Ameanza Kigwangala, jana tukamsikia tena Mwenyekiti CCM MARA na hawafanyi kwa bahati mbaya! la hasha bali ni kujaribu kuonesha ni kwa namna gani wamepotoka. At the end their regime will be fated to end badly.
Watu wanataka fursa
 
Kweli mkuki kwa nguruwe.
Kipindi cha jiwe wewe na MATAGA wenzako mlikuwa mnatupigia kelele kumuonvezea miaka mingine hadi achoke mwenyewe.
 
Kinachosikitisha zaidi ni kama hakutakuwa na wagombea wengine kutoka vyama vingine.

Labda kwa vile wanajua mgombea wa chama chao huwa anashindishwa tu hata kama kura hazitoshi.
CCM ni majambazi wa kura
 
Ni hatari sana nchi kuongozwa na viongozi wa namana hii, viongozi wanafiki wanaofikiri matumbo yao yajae kwanza badala ya kufikiri tujinasuaje kutoka kwenye hili box la umasikini, mtu anafikiria kumpa mama Urais hadi 2030 - Je hii ndiyo agenda ya watanzania kwa sasa?

Hapa ndipo tunasema CCM ishafikia mwisho!
 
Mkuu kwani shida iko wapi?kwani utaratibu wa CCM, mgombea wao lazima atumikie vipindi viwili, na 2025 hakuna atakye ruhusiwa kuchukua fomu tofauti na Mama Samia!!

Kwani ni kanuni walizibadirisha kumpa faida jiwe, basi hazina budi kuendelea tu. Sisi binadamu tuna mipango yetu ila Mungu ndio muamuzi.

Kama wakianza zile kelele zao kuwa, hata baada ya 2030, ni yeye tu hapo sio sahihi! lakini hili la kuendelea na term yake ya pili sioni kama ni shida
 
Back
Top Bottom