Msonjo
JF-Expert Member
- Oct 13, 2019
- 1,378
- 2,394
Wanaopinga uwepo wa Mungu, ukiwauliza kuhusu asili ya huu ulimwengu na jinsi ulivyo katika mpangilio ambao hauna dosari ndani yake, watakwambia ni nature au coincidence.
Mimi mtu akinambia hivi swali la kwanza linalokuja akilini mwangu, ni je, hiyo nature inaakili(ufahamu)?.
Kinacho mpambanua mwanaadamu, na kumuwezesha kufanya mambo yake kwa mpangilio ni akili yake, hata wanyama nao wanaufahamu hatakama tutasema hawana akili ndio maana na wao kuna mambo wanayafanya kwa mpangilio.
Hivyo jambo/kitu chochote kuwa katika mpangilio kunalazimu uwepo wa kilicho sababisha huo mpangilio, ambapo kwa mambo ya mwanaadamu ni yeye mwenyewe kwa sababu anaakili, na anaevuruga mambo huyo ni chizi(hana akili).
Ndio maana ninauliza je hiyo nature inaakili?
Kwa sababu mpangilio huu wa ulimwengu uliokamilika na usio na dosari, unalazimu uwepo wa akili yenye ujuzi iliyotumika kuweka kila jambo katika mpangilio.
Na kama nature haina akili basi ingelazimu huu ulimwengu kutokuwa katika mpangilio uliokamilika na usio na dosari.
Labda utasema huu mpangilio ni coincidence, ok.
Kwani coincidence ni nini?
Wanasema coincidence of events is the appearance of a meaningful connection when there is none.
Hivyo ni kama kitendo cha kunguru kumnyea mwanaadamu, unaweza ukadhani alikusudia lakini kumbe ni coincidence tu.
Lakini unaonaje mtu akija kukuambia, bwana kila nikipita sehemu fulani kwenda kazini siku fulani, kuna kunguru huja kininyea kichwani.
Kunguru ni yuleyule, sehemu ile ile, Kila akienda kazini, na sehemu anayomnyea ni ile ile.
Asee, atakayekwambia hiyo ni coincidence atakuwa na matatizo ya akili, huyo kunguru ima anaakili ya binadamu au katumwa ndio maana hakosei.
Hivyo coincidence hailazimu kwa huu ulimwengu kuwa na mpangilio uliokamilika na usio na mapungufu yeyote, Bali kama ingekuwa hivyo basi ingetakiwa mambo yawe randomly.
Wote tunafahamu jinsi wanasayansi walivyofanya uvumbuzi wa mambo mbalimbali kuhusu huu ulimwengu, na wametuelimisha jinsi huu ulimwengu ulivyokuwa katika mpangilio usio kuwa na dosari yeyote wala kuingiliana.
The solar system, the internal and external processes of the Earth, na jinsi zinavyofanyika kwa mpangilio.
Na tuache huu mpangilio wa ulimwengu sisi wanaadamu wenyewe tukijiangalia, tunaona jinsi miili yetu ilivyokaa kimpangilio na kufanya kazi kwa mpangilio, na tunajua hatujajiumba wenyewe bali tumeumbwa.
Hivyo kama mtu anasema ni nature basi hiyo nature itakuwa inaakili maana sio kwa kujipangilia huku tuseme ni coincidence.
Wakana Mungu wanasema haya yametokana na nature, basi kama wanasema hivyo itakuwa hiyo nature inaakili na ndio mungu wao, maana wameipa sifa ya uungu, kwa kusema ndio chanzo cha ulimwengu na ndio iliyowaumba, hata kama hawaiabudu au haina dhati.
Maana kwetu sisi waislamu aliyeuumba huu ulimwengu na vilivyomo ndiye tunayemuita Mwenyezimungu (Allah subhaanahu wataa'la) na kumuabudu.
Atakwambia ndio ulimwengu upo katika mpangilio lakini huo sio uthibitisho kwamba mungu yupo............... Umesema kweli kabisa ewe mkana mungu.
Ndio mpangilio wa ulimwengu sio uthibitisho kuwa mungu yupo bali ni alama/ishara ya kwamba kuna aliyeuweka huu mpangilio, na huyo ndiye aliye uumba huu ulimwengu.
Hivyo mwenye akili anakili na kukubali kuwa huu ulimwengu kuna aliyeuweka katika huu mpangilio na anayesema huu ulimwengu umetokea tu basi huyo ni mkaidi tu, na analeta kiburi, ilhali unajua kuwa hiwezekani jambo kama hilo.
Atakuambia thibitisha kama mungu yupo?
Sasa wewe ilikuwaje mpaka ukaconclude kwamba mungu hayupo? halafu hapo hapo hujui ilikuwaje huu ulimwengu upo katika huu mpangilio?
Umezaliwa umeukuta na utakufa utauacha, na ulipozaliwa habari za uwepo wa mungu umezikuta, umeambiwa mungu ndiye aliyeumba huu ulimwengu, ukakanusha ilhali aliye uumba humjui.
Jamani niacheni niendelee kuwaita hawa watu wakaidi.
===
Iliyotangulia soma Wanaopinga uwepo wa Mungu ni wakaidi
Muendelezo soma Wanaopinga uwepo wa mungu ni.....-3