Wanaoolewa ni darasa la saba na form 4


dini ipi ?
 
tatizo ndo hilo,na pia ukiwa na mwanamke mwenye challange na challange zake ni kusifia wanaume wengine ungezipokeaje

itategemea sasa anasifia katika sector ipi? kama kwenye suala la mkwanja ndio utafute ili uendane na hao anaowasifia.
 
Ndo maana mimi na degree yangu nilioa housegirl kabsaaa,adabu mwanzo mwisho mpaka leo napewa shkamoo!!
 

dini inasema hivi
mathayo 19:6 6 Hata wamekuwa si wawili
tena, bali mwili mmoja. Basi
aliowaunganisha Mungu,
mwanadamu asiwatenganishe.


je hapo kwenu unajenga akakae nani ? wakati mmeanzisha mji wenu na mumeo.
pia dini inasema mzazi anatakiwa aandae urithi sio mtoto kumsaidia mzazi
 
Kuna jingine kubwa japo haliwekwi hadharani,wenye madegree wengi wameshatumika sana ni kama kununua nguo pale manzese!!! sorry nalog off jioni njema
 
Shda siyo degree lakn anajielewa unaweza ukapata darasa la saba lakn hajitambui kuwa yeye ni mke wa mtu vivyohivyo hata kwa mwenye degree na mkumbuke nyie dada zetu wanaume tunawakwepa kwa sababu ya hzo tabia zenu mnapokuwa chuo tena kama chuo fulan mmmh ni majanga
 

Hiyo dini yako..me dini yangu inanambia niwatunze wazazi wangu na imeniahidi fadhila kubwa kwa kuwatunza....

Pia imenikataza kufanya kazi mpaka pale mume wangu ataporidhia na kuniruhusu nifanye kazi, na kama ataniruhusu dini yangu inanipa uhuru wa matumizi ya pesa zangu na yeye anawajibika kwa kila kitu kwangu....

Tena inanambia hata siku nikitoa pesa yangu kwa ajili ya chakula chake basi inahesabika nimetoa sadaka kama tu vile ningeweza kutoa chakula kulisha masikini....nalipwa thawabu....

So siwajibiki kwa chochote...labda tu nimpe pesa yangu kwa mapenzi.....
 
una level gan ya elimu? uliwahi kuoa level hiyo ya elimu yakakukuta?au umefanya utafiti kwa kuungalia wap?
 

ha ha ha ha ha ha
haya kama ndio hivyo
sisi kwetu hatuna talaka ndio maana tunajihadhari tusikosee kuoa huko kwenye talaka mnaweza mkaoana asubuhi jioni talaka hakuna shida
kwa kwetu hatuoi wanawake wenye degree wengi wao pasua kichwa
 
una level gan ya elimu? uliwahi kuoa level hiyo ya elimu yakakukuta?au umefanya utafiti kwa kuungalia wap?

unaishi Tanzania au jamiiforums ?
usipende kuact maisha humu
 
unaishi Tanzania au jamiiforums ?
usipende kuact maisha humu

jibu hoja mkuu sio unaruka ruka. mmefanyia wapi utafiti wenu? sample yko ilikuwa na ukubwa gani? usije ukawa umefanyia uchunguzi huu kwa mama na dada yako tu halafu unataka tukubaliane na utafiti wako. itakuwa vichekesho sababu tanzania kwa idadi ya wanawake waliosoma na wasiosoma sidhanni kama utafiti wako utakuwa sawa kama umetumia sample ya watu wawili.
 
mkuu unalazimisha watu watoe facts ambazo zipo wazi,haya we tupe kwanza fact kwamba wanawake wasomi si pasua kichwa kwenye ndoa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…