Wanaonata baada ya kupata pesa

Wanaonata baada ya kupata pesa

kwanza ni kitu gani kinakuambia mtu ana fedha? Gari analoendesha (ambalo lina mkopo anadaiwa hadi kwa mangi bill ya dona), mavazi yake (hahaha mikopo ya blauzi na handbags huko maofisini ni aibu tupu), au dhahabu (mchina katurahisishia wala kama ni feki ama yenyewe mnaweza msijue ).

Yaani mtu anakutembelea siku moja unamfurahisha kwa kukwangua mfuko halafu anataka mgawane hizo bata?
Kwani yeye kinachomfanya asiwe na hela ni nini kwa mfano??
Wakati mwingine mnawasingizia tu wenye fedha. Mtu ukipata fedha lazima ubize uongezeke maana pesa inakutuma. Sasa wewe unataka tuje tukae kijiweni kama nlivyokuwa sina activities? Haiwezekani.
 
kwanza ni kitu gani kinakuambia mtu ana fedha? Gari analoendesha (ambalo lina mkopo anadaiwa hadi kwa mangi bill ya dona), mavazi yake (hahaha mikopo ya blauzi na handbags huko maofisini ni aibu tupu), au dhahabu (mchina katurahisishia wala kama ni feki ama yenyewe mnaweza msijue ).

Yaani mtu anakutembelea siku moja unamfurahisha kwa kukwangua mfuko halafu anataka mgawane hizo bata?
Kwani yeye kinachomfanya asiwe na hela ni nini kwa mfano??

Hatuwa zungumzii hao watu, hao hawana pesa, pole kumbe ukiona mtu anaendesha gari kwako wewe ni anapesa asee
 
Unakuta mtu anaishi na kuwa mahusiano na watu kama kawaida lakini baada ya kupata nafuu ya ugumu wa maisha kwa kupata fedha kutokana na ajira au biashara basi ghafla anaanza majidai na kunata.

Wengine anadiriki eti kakusahau au anakununia na hata kukuonyesha roho mbaya,hivi hii hali inatokana na nini?

tafuta pesa na hutapata muda wa kupika majungu!!
 
Ukipata pesa maisha yanabadilika, kama alikuwa anakula kwa mama ntilie sasa atakula five star hotel na hili litaonekana ni kunata, akaiendelea kula kwa mama ntilie mtamuita bahili na pia pesa ikiongezeka hata marafiki wanabadikika laima aongee na wenye hela kama yeye au zaidi yake ili kupata mchongo mzuri wa kuzungusha hiyo hile, kukusahau itakuwa si kweli ila sema na sie maskini huwa tunajistukia, jamaa kakuzidi na mlikuwa wote kwenye mitikasi ya kuzisaka basi unaanza kumkwepa hata akikutafuta vipi unajinyanyapaa mwenyewe, unaogopa kuonekana unakula hela zake kwa kuwa huwezi kulipa bili viwanja anavyokwenda ukimuona unasepa, mwisho jamaa nae anaona isiwe shida anafunga vioo
 
Tajiri na tajiri mwenzie

masikini na masikini mwenzie.

Ndivyo principle ilivyo.
 
Hehehe mnazungumzia watu wepi? Sema basi tujiongeze na sie.

Mie nikiona mtu anaendesha vitz aka babywalker yaani roho inanitoka manake najua keshayaotea maisha. Unadhani na joto hili na madaladala ya gongo la mboto siogopi tetenus?
Hatuwa zungumzii hao watu, hao hawana pesa, pole kumbe ukiona mtu anaendesha gari kwako wewe ni anapesa asee
 
Back
Top Bottom