Wanaonata baada ya kupata pesa

Wanaonata baada ya kupata pesa

leipzig

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2013
Posts
2,766
Reaction score
1,716
Unakuta mtu anaishi na kuwa mahusiano na watu kama kawaida lakini baada ya kupata nafuu ya ugumu wa maisha kwa kupata fedha kutokana na ajira au biashara basi ghafla anaanza majidai na kunata.

Wengine anadiriki eti kakusahau au anakununia na hata kukuonyesha roho mbaya,hivi hii hali inatokana na nini?
 
kuishi ni mara moja ukificha tabia yako duniani ni wapi watakapoijua ??
 
Inategemeana na hiyo pesa kaipata vipi?

Kwa mfano hawa waliopata ajira unakuta amepata nafasi ya kusaini manunuzi,vile vi 10% unakuta anavipata na mshahara wake uko palepale!
 
Ni kweli, hasa hawa watu ambao wameishi kwa dhiki huwa wanasumbua sana
 
jamaa baada ya kupata pesa alinambia eti i don't fit in his dream! chezeya pesa wewe!
 
Wakati mwingine inaweza ikawa ni kujistukia kwako tu mkuu! Au ulimpiga mzinga akachomoa?
 
Unakuta mtu anaishi na kuwa mahusiano na watu kama kawaida lakini baada ya kupata nafuu ya ugumu wa maisha kwa kupata fedha kutokana na ajira au biashara basi ghafla anaanza majidai na kunata.

Wengine anadiriki eti kakusahau au anakununia na hata kukuonyesha roho mbaya,hivi hii hali inatokana na nini?

Pata pesa tujue tabia yako
 
Ugeni na ulimbukeni unapochanganyika pamoja
 
Ni kweli, hasa hawa watu ambao wameishi kwa dhiki huwa wanasumbua sana

Ni kweli kabisa watu walioishi au kukulia kwenye dhiki, wakija kupata hela mbona utakoma yaani wanajifanya sio wabantu kabisa. Mawasiliano hawataki kabisa yaani wanaishi kama wanaigiza vile. Vijitu vya hivyo vinakera sana.
 
images
 
Wengine wakipata pesa wanakata mawasiliano kwa kuwa wanachoka kuombwa pesa kila wakati. Wabongo mmekuwa omba omba mno ndio maana watu wenye pesa wanawachunia!
 
Ni kujihami self defence. Binadam ni hatar sana hasa wabongo ukupiga hatua maishani ghafla. Sema ni sheria tu lasivyo unachinjwa kweupe. Hakuna ambaye atakupenda kwa dhati ni unafiki tu. Kuwa mkali na leta hofu kwa watu wasikuzoee. Hata ukifa ama ukifiwa wasuse kuja kwenye msiba wako wapotezee. Eti bongo kuuzuria msiba na kugawa Hela na ofa et kipimo una roho nzur. Ni bora umchekee nyani kuliko mbongo mwenzako utavuna hasara na aibu. Chezea muafrika mweus wewe. Nyambaff zetu!!!
 
Hakuna mbongo yeyote atkupenda uwe na hela ama ucwe. Chuki za kulazimisha zinazid bila sababu ukifanikiwa kifedha. Wivu unawajaa watu na hapo wanajishtukizia et unaringa.
 
Unakuta mtu anaishi na kuwa mahusiano na watu kama kawaida lakini baada ya kupata nafuu ya ugumu wa maisha kwa kupata fedha kutokana na ajira au biashara basi ghafla anaanza majidai na kunata.

Wengine anadiriki eti kakusahau au anakununia na hata kukuonyesha roho mbaya,hivi hii hali inatokana na nini?
Mkuu pengine mko wengi mnaotaka kumkopa jamaa, na wewe pata zako halafu mringishie ndo dawa yake.
 
Back
Top Bottom