Wanaompinga Rais kutumbua majibu hamna uzalendo

Wanaompinga Rais kutumbua majibu hamna uzalendo

Magufuli katika safari yake ya kisiasa amekuzwa na kupitia katika mfumo huo huo uliomuweka pale alipo sasa hivi, mfumo uliokumbatia uzembe na ufisadi wa kiwango cha juu.

Kilichoweza kuulinda mfumo huu ni katiba mbovu tuliyokuwa nayo ambayo inampa madaraka makubwa rais na pia kumzuia kufikishwa mahakamani kwa makosa aliyofanya akiwa madarakani hata kama yalikuwa ni ya kifisadi. Rais akiwa fisadi basi hata wasaidizi wake wanakuwa wa fisadi, maana akiuchukia atawakamata na kuwaadhibu mafisadi, hali kadhalika wasaidizi wake wasipokuwa wasipokuwa mafisadi hawatoweza kufanya kazi na Rais fisadi, aidha watajiuzulu au watafutwa kazi.

Kashfa kubwa za ufisadi zilizokumba serikali za CCM za awamu za karibuni Magufuli alikuwa madarakani, EPA, RICHMOND, ESCROW, UDA na nyingine nyingi tu, akiwa kwenye baraza la mawaziri alishiriki kwenye maamuzi ya pamoja.

Hakuachwa mbali na mfumo, kwenye sakata la uuzwaji wa nyumba za serikali utamtenganishaje Magufuli hapo? Wanawake kama Sundi Mulomo aliowapa nyumba akituhumiwa kuwa na uhusiano nao amejiosha vipi hapo? Kivuko cha mv Dar akiwa Waziri mwenye dhamana alichukua hatua gani kuzuia? Au kamuwajibisha nani?

Hii inamuondolea credibility ya kutumbua majipu makubwa ambayo yana direct impact kwenye maisha ya wananchi wa kawaida, tena majipu yanayoonyesha connection na viongozi wakuu waliopita. Angepigania pia katiba itakayompa nguvu yeye na hata wengine watakaokuja kuweza kutumbua majipu hata kwa waliotumia madaraka vibaya kufisidi nchi yetu.

Waliounganisha bomba la mafuta kule bandarini tena ndiyo kuna mabilioni ya pesa za kodi zilizokuwa zinaibiwa na kasababisha serikali kukosa mapato nani kutumbuliwa?

Aliyetoa amri ya kutotumia flow meters pale bandarini na kuikosesha nchi mapato ametumbuliwa lini?

Home shopping centre waliokuwa wanaingiza makontena bila kuyalipia ushuru, zaidi ya PM kwenda na orodha yake akiongozana na wanahabari nini kkmefuata?

IPTL ilivyouzwa kimagumashi wakati ilitakiwa iwe inamilikiwa na serikali baada ya miaka 20 lakini imeuzwa kinyemela na mkataba unaosababisha bei ya umeme iendelee kuwa juu maana wanalipwa capacity charge sh 8b kwa mwezi hata kama hawazalishi umeme, je kuna majipu makubwa kama haya?

Binadamu ni mtumwa wa dhamira yake, na kama dhamira ni kuchukia ufisadi asingeweza kukaa na Muhongo dalali aliyefanikisha dili la kifisadi la kuuza IPTL. Muhongo aliyetia mkono kutoa siri za maamuzi ya baraza la mawaziri kwa kuagiza kwa sms kwa meneja anayehusika na flow meter awashe PM anapenda kukagua.

Kufanya kazi na watu kama akina Chenge watuhumiwa sugu wa ufisadi Tanzania.

UDA inajulikana wazi ufisadi ulivyogubika uuzwaji wake, nini kinachompa kigugumizi? Kuingia kwenye moyo wa majipu yaliyolea ufisadi.

Angalia dana danadana inayopigwa na serikali yake kuhusu LUGUMI, ni kwa sababu inajulikana connection inakoendea hawezi gusa.

January Makamba na dada yake Mwamvita kwenye utapeli wa yule mtaliano? Mtu aliyekuwa anajua magumashi yote ya jinsi alivyoingia na kupata kura kwenye uchaguzi uliopita mbona hazipigwi kelele amtumbue?

Dhamira ya kubadilisha mfumo haipo, sana sana dalili za wazi za kuficha udhaifu wowote utaoweza kuonekana, mfano kuzuia matangazo ya bunge kuonyeshwa live, wakati yeye aonyeshwe live akitumbua majipu. He is attention seeker.

Kwa hiyo si kwamba wanaokosoa si wazalendo, hasha, hatutaki mihemko na hisia zikatawala sababu rais ana madaraka makubwa aliyopewa katiba, kumbuka mwalimu Nyerere aliwahi kusema kuwa katiba hii imempa madaraka makubwa rais kiasi kwamba akitaka kuwa dikteta angeweza, na ikitokea kuwa na Rais anayependa udikteta vyepesi kuitumia katiba hii, je tunataka kutengeneza dikteta?

Tunataka uhuru wa kusikilizwa hata kwa watuhumiwa na vyombo vya serikali vya uchunguzi viimarishwe na kupewa meno tusije kuwa kama North Korea

Let give him time yakutosha yatasafishwa tuu madudu yotee hayo either direct or indirect
 
Rais, kwa nia nzuri kabisa, hawezi kukosea katika huko kutumbua?

Walipokosea wapi? Unaweza kutaja specifics?

Uzalendo ni nini? Raia wanaotekeleza wajibu wao wa uraia wa kukosoa viongozi wanakosa uzalendo?

Kwa nini isiwe kwamba raia wanaoshangikia tu bila kukosoa pale penye la kukosoa ndio wawe wamekosa uzalendo?
 
Tatizo la hawa watu wanamtandao mkubwa mno kwa hiyo akisema asubiri au awashirikishwe kwanza lazima watampiga chenga kwa namna yeyote, its better ata kama mtu atashinda au ataonekana ameonewa hapo baadae kuliko kumwacha mtu mwenye tuhuma kuendelea kuafanya kazi huku watu hawana imani nao. Mana ukipoteza iman kwa watu kuurudisha utatatumia gharama kubwa sana
Bila due process tutajuaje huyu ni mwizi kweli na huyu kasingiziwa?

Ukikataa due process utakubali kubambikiwa kesi na kuhukumiwa bila nafasi ya kujitetea?
 
But kumbuka Magu anafukuza/kuwasimamisha kazi na kuviachia vyombo vya sharia kufanya kazi zake hakuna mahala Magu amemtolea mtu hukumu kwamba huyu mtu afungwe or whatever anachofanya yeye ni kujaribu kuisafisha serikali yake pale anapo ona kuna kupoteza uamnifu kwa watz
Katika ufunguzi wa daraja la Nyerere Magufuli amemtoa kazini Kabwe na kusema watu wa aina hii hawana nafasi katika serikali yake.

Rais anaposema watu wa aina hii hawana nafasi katika serikali yake, baada ya ripoti ya dakika mbili tu ambayo haijampa mtuhumiwa nafasi ya kujitetea, hajahukumu?
 
Rais anavunja sheria makusudi.
Kwa sababu haheshimu utawala wa sheria.

Neither the letter nor the spirit.

Anapenda udikteta.

Ndiyo maana kaapisha wabunge uwaziri kabla hawajaapishwa ubunge, kaliamuru bunge lipeleke fedha za tafrija yake kwenye matumizi ya hospitali against the pronciple of separation of powers, kaingikia mahakama inavyoamua kesi, anaamuru fedha za sikukuu zikizofutwa ziende wizara ya ujenzi bila ya kuwa na nguvu hizo all within the first 100 days.
 
Katika ufunguzi wa daraja la Nyerere Magufuli amemtoa kazini Kabwe na kusema watu wa aina hii hawana nafasi katika serikali yake.

Rais anaposema watu wa aina hii hawana nafasi katika serikali yake, baada ya ripoti ya dakika mbili tu ambayo haijampa mtuhumiwa nafasi ya kujitetea, hajahukumu?

Anahitaji kuisafisha serikali yake kwa namna yeyote ile wapo watakao umia au kuonewa hatukatai lakini mwisho wa siku tutasimama katika line moja. Tunahitaji kusonga mbele kwa namna yeyote ile
 
Tuweke rekodi vizuri. Hakuna mtu anayempinga Rais. Lakini wapo wanaokosoa utekelezaji wa baadhi ya mambo, na hilo ni jambo la kawaida. Kupinga na kukosoa ni mambo mawili tofauti. Lakini nafikiri mleta hoja ni wale yes yes wa chama fulani ambao hawataki kukosolewa., kwa hiyo anataka kutushawishi na sisi wengine tuwe kama yeye. Haiwezekani watanzania milioni zaidi ya 40 wakawa wanakubaliana kwa kila kitu.
 
Anahitaji kuisafisha serikali yake kwa namna yeyote ile wapo watakao umia au kuonewa hatukatai lakini mwisho wa siku tutasimama katika line moja. Tunahitaji kusonga mbele kwa namna yeyote ile
Hapana.

Hahitaji kuisafisha serikali yake kwa namna yoyote ile.

Anahitaji kuisafisha serikali yake kwa namna sahihi inayofuata sheria na maadili.

Tatizo unamuwekea standards ndogo sana wakati yeye ni mtu mwenye kazi kubwa sana.

Tukisema uonewe kwa kupigwa risasi kwa kosa ambalo hujafanya kwa sababu Magufuli anasafisha serikali yake kwa njia ya kidikteta utakubali?
 
Tuweke rekodi vizuri. Hakuna mtu anayempinga Rais. Lakini wapo wanaokosoa utekelezaji wa baadhi ya mambo, na hilo ni jambo la kawaida. Kupinga na kukosoa ni mambo mawili tofauti. Lakini nafikiri mleta hoja ni wale yes yes wa chama fulani ambao hawataki kukosolewa., kwa hiyo anataka kutushawishi na sisi wengine tuwe kama yeye. Haiwezekani watanzania milioni zaidi ya 40 wakawa wanakubaliana kwa kila kitu.
Hakuna maendeleo bila kukosoana.

Tutazunguka katika makosa yaleyale kwa kuogopa kuonekana si wazalendo?

Rais ni mtu tu. Wasaidizi wake pia ni watu. There is such a thing as "the wisdom of crowds" ndiyo maana Waswahili wakasema "penye wengi haliharibiki jambo". Ndiyo maana Wagiriki wakaweka misingi ya utawala wa demokrasia. Demokrasia si kupiga kura tu.That is electocracy, not democracy. Demokrasia inaendelea hata kwenye ushirikishwaji wa umma katika uongozi wa nchi wa kila siku. Rais na viongozi wengine hawawezi kuachwa waongoze kivyao tu. Kuna misingi na taratibu za uingozi. Na hii kama inavunjwa ni lazima wananchi waseme. Hata Nyerere alisema hili. Na yeye alishiriki mpaka kukosoa mambo alipotoka kwenye urais.

Sasa kwa nini wananchi wakishiriki kujadili uendeshwaji wa nchi yao na kukosoa jinsi baadhi ya mambo yanavyomaliziwa- yanavyomaliziwa by the way, nia ni nzuri na ideas ni nzuri ila umaliziaji ndio unakosolewa- kwa nini mwananchi huyo aonekane si mzalendo?
 
tulieni jamani mbona ndo siku imeanza, watapelekwa mahakamani, yeye Magu anachofanya ni kusafisha nyumba. si kwamba hawana makosa, laaha hasha , kikubwa watolewe mambo yaendelee . wakati kikwete yuko madarakani mlisema rais gani mpole anacheka cheka tu, sasa jembe limeingia mnapiga kelele. tulieni tu kitaeleweka na mambo yatakwenda mbele. ROMA haikujengwa kwa siku moja.
Siku imeanza vibaya!
Haki yapaswa itendeke!
Peleka mahakamani au tumia vyombo husika vya uchunguzi na usimamizi wa watumishi!
 
Mleta hoja kuna mahali hujapatendea haki. "Umetuhukumu". Hii ni wrong perception. Ungeanza naye kwa kumkumbusha kuwa: alikuwepo kwenye huu mfumo wa kifisadi kwa miaka ishirini na ushee akiuangalia bila kucomment chochote na hata kujiuzulu kuutumikia huo mfumo ili kutuonyesha jinsi ulivyomkera. Hakufanya lolote labda hakuwa na ndoto ya kuwa rais wa nchi hii siku moja! Na sasa anaelea na kuzama kwenye mfumo huo wa kifisadi ukiomwingiza jumba jeupe. Atawafanyaje watu walewale wenye mindset zilezile ili kuondoa hicho anachotuaminisha? Hakuna njia rahisi zaidi ya hii ya kuuvunja mfumo na kuziacha sheria kufanya yaliyokusudiwa. Namaanisha katiba mpya yenye nguvu na isiyotoa loophole ya namna yoyote. Pia kuwaweka pembeni wasimamizi wa mahakama wenye kwenda kinyume na maadili ya kazi zao. Isitoshe airuhusu takukuru na waendesha mashtaka huru na vyombo vya uchunguzi huru vifanye kazi sambamba na mahakama na dci. Vinginevyo fairness hakuna na haiji kuwepo hadi anamaliza ngwe yake.

Nimewaza kwa sauti tu.

KWA SAUTI, LAKINI KWA KIJINGA

who is he now? wha is he doing? ndio muhimu zaidi kuliko past
 
Hakuna maendeleo bila kukosoana.

Tutazunguka katika makosa yaleyale kwa kuogopa kuinekana si wazalendo?

Rais ni mtu tu. Wasaidizi wake pia ni watu. There is such a thing as "the wisdom of crowds" ndiyo maana Waswahiki wakasema "penye wengi haliharibiki jambo".

Sasa kwa nini wananchi wakishiriki kujadili uendeshwaji wa nchi yao na kukosoa jinsi baadhi ya mambo yanavyomaliziwa- yanavyomaliziwa by the way, nia ni nzuri na ideas ni nzuri ila umaliziaji ndio unakosolewa- kwa nini mwananchi huyo aonekane si mzalendo?
KWA SAUTI, LAKINI KWA KIJINGA

who is he now? wha is he doing? ndio muhimu zaidi kuliko past

kweli mkuu yaliyopita si ndwele tugange yaliyopo na yajayo
 
KWA SAUTI, LAKINI KWA KIJINGA

who is he now? wha is he doing? ndio muhimu zaidi kuliko past
La maana zaidi ya ujinga ulio nao ni who was he before? Au wewe ndio wale mnaoamini kuzeeka kwa shetani hugeuka kuwa malaika? Wrong perception again! Na jibu la swali lako ni kuwa hicho anachokifanya sasa alitakiwa akifanye 20 yrs ago kwa kuonyesha glory spirit na siyo hii one man show.
 
Nashauri wote wanaompinga Magufuli wetu tuwakuze nchini Tanzania wakaombe hifadhi nchi nyingine!
 
Ungecheki wanampnga kwa hoja zipi mkuu, sio kusema hawana uzalendo,
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom