Si kweli!Habari
Mheshimiwa Rais ana nia ya kuwasaidia watanzania hasa wale wa hali ya chini waweze kupata haki zao ambazo tangu uhuru walikua wanazifaidi wachache
Lakini limetokea kundi la watu ambao hawana hata haya eti wanampinga rais katika harakati za kuisafisha nchi na kuifanya nchi ya watu wenye machungu na haki za wengine
Kwa kweli hawa hawana uzalendo kabisa na hawaitakii mema nchi yetu yenye utajiri wa kutupwa lakini watu wachache ndio waliokua wanaufaidi
Mhe Rais ana moyo wa kuwatumikia watanzania kweli kweli mana anaongea mpaka anahisi yale mateso wanayoyapata watu wa hali ya chini ni kama yake, Aanaumia mpaka anataka kulia kwa sababu yauchungu anauhisi. Magu ana moyo wa kipekee kwa kweli
Ila tutafika tu pale Magu anapohitaji kutufikisha. Mwenyezi mungu yu pamoja na wanaonewa
Watu hawapingi utumbuaji Bali njia za utumbuaji!
Magu anaelezwa na watu juu ya matatizo ya mtu X, halafu anamtumbua bila ya kumpa nafasi huyo X ya kueleza kwanini a,b na c vilitokea! Unapomsikiliza mtu wakati mwingine yapo mambo mengi ya kujifunza, maana serikali pia inapaswa ijipime!
Kesi 2 zimenitia shaka juu ya maamuzi yake na nimeona ame-act kama Mwl. wa zamu!
Case1: Ya mkurugenzi wa Dar, pale darajani kigamboni....... Just kaambiwa na Makonda yeye katumbua, angeleta picha tofauti kwa kufanya haya:
- Angesema kuwa baada ya kupata taarifa hizi nilifanya uchunguzi na kujiridhisha, so nimeamua kusimamishwa kazi Mr. Kabwe....! Au
- Naamuru uchunguzi ufanyike juu ya jambo hili na ikithibitika kuwa tuhuma hizi ni za kweli nitamchukulia hatua za kinidhamu!
Case 2:
Kumtumbua Mama Kairuki kwa kutochukua mshahara wake. Barua ya kumsimamisha kazi imetoa sababu hiyo tu bila ya kutoa maelezo mengine!
Hivi Mama Salma Kikwete au Mke wa Magufuli waliendelea kufundisha baada ya waume zao kupata uraisi? Je wao hawajaacha mishahara! Nani anayejua mume wa Kairuki anaingiza kiasi gani? Nani anayejua biashara za huyo Mama? Nani anayejua hazina yake ina kiasi gani cha pesa? Nani anayejua lengo la kuacha pesa hizo ni nini? Hakupokea mshahara, je hicho ndio chanzo pekee cha mapato yake? MF. Majaliwa PM ni mbunge ambaye analipwa posho za vikao, anatumia usafiri wa ofisi na halipii gharama zingine za maisha, je anaulazima gani wa kuutoa mshahara wake wakati mapato mengine nje ya ofisi yanatosha kuendeleza maisha?
Hapa ofisi ya mtumbuaji ilipaswa kuja na taarifa kuwa huyo Mama alikuwa hachukui mshahara lakini ameonekana kujilipa malipo makubwa bila ya sababu za msingi! Au ameonekana kujihusisha na vitendo vya rushwa etc ambavyo labda vita justify matumizi mabaya ya ofisi na kujinufaisha makusudi!
Napenda haki itendeke pale tunapoamua kusafisha ofisi, Ila si vizuri kujitafutia pointi za kisiasa huku ukiumiza familia nyingine!
Hivi unafikiri kwanini hata jambazi lililokamatwa kwa mauaji ktk eneo la ukio hupelekwa mahakamani? Si angefungwa tu straight! Hata Sadam Husein alipelekwa mahakamani kusikilizwa!
Kumshangaa Mama kutochukua pesa na kumfuta kazi ni kituko! Hebu uwashangae basi na wabunge wa ccm wanapata wapi pesa za kampeni wanazogawa wakati wa uchaguzi?
Haki, haki, haki....,...... Hata dhamira ikiwa njema vipi, Ila kama haki ikikosekana, dhamira hiyo itakuwa mbaya na si vema kuichekelea!