Wanaomchukia Rais Samia kwasababu ya dini yake, uzanzibari, na kwa kuwa ni mwanamke muache mara moja

Haihitaji hata utafiti wa maprofesa..Jamii inayoamini kwenye ushirikina haiwezi kupima kiongozi Kwa matokeo chanya ndio maana inaamini maji ya upako,uzushi,miujiza na upuuzi kama huo..

Jamii isiyo na elimu huwa inaendeshwa Kwa lazima.Chini ya 2% ya watu hawana degree,chini ya 5% hawana Diploma then unategemea nini?
Unatakataka nyingi sana wewe, kurtwa nzima unajaza uchafu humu jukwaani.
 
Hakuja cha chawa wala nini ila hoja zenu nyingi ni hizo hizo za zinazohusiana na dini,utaifa na jinsia..

Hoja gani yenye mashiko ambayo wewe unampinga Rais Samia?

Kwa mfano mimi sina unasaba na dini ya Rais,kabila lake na Wala anakotokea mimi natokea Njombe na ni mkristo..

Kwa hiyo nachosema namaanisha wengi wenu mumekalia maujinga yenu tuu.
Huwezi kujua chochote kinachozungumziwa kwa sababu ya uchawa wako, wewe kuwa dini na kabila tofauti nae hakusaidii, tatizo akili yako imefunikwa na blanketi la uchawa.

Mpaka utakapotoa hilo blanketi ndio utaamka toka kwenye usingizi wa uchawa uliolala.
 
Huwezi kujua chochote kinachozungumziwa kwa sababu ya uchawa wako, wewe kuwa dini na kabila tofauti nae hakusaidii, tatizo akili yako imefunikwa na blanketi la uchawa.

Mpaka utakapotoa hilo blanketi ndio utaamka toka kwenye usingizi wa uchawa uliolala.
Nitaendelea kuwa Chawa Ili niwakomeshe wenye chuki kama nyie pimbi msio na hoja.
 
Nilichogundua kuna watu baadhi wanamchukia Rais Samia kwasababu ya dini yake na uzanzibari wake

Huyu mama uungwana wake na roho yake nzuri vitamponza sana maskini,sisi wabara tupo wengine tuna roho mbaya sana

Kuna watu wanamchukia Samia kisa ni mwislam, wengine wanamchukia kisa ni mzanzibary wengine wanamchukia kisa ni mwanamke kapewa madaraka makubwa hawakutaka yawe ila kwa uwezo wa mungu yamekua

Wengine wakaenda mbali wanasema Samia ni mdini, hadi sasa sijaona justification ya kumwiita SSH mdini, sijaona chochote kile kafanya cha kuprove ni mdini, nipo tayari kutoa dau la pesa hata ikibidi kwa atakayenionyesha kwamba mama ni mdini

Tatzo tunasahau kwamba teuzi pia anachukua zenji kama pia alivyofanya mtangulizi wake naye alichukua chato

Sasa Zanzibar wengi ni waislam 98% au 99% sasa unatarajia teuzi za kutoka visiwani ziwe za dini gani?

Mbona mwendazake alivyochukua chato ambapo 80% ni Christians maana yake wengi lazima wawe wakristo kuna tatizo hapo?

Mimi hadi sasa ukiniuliza viongozi walowahi kuwa na udini sana hapa tz ni mmoja tu, sio mwingine ni Mkapa, Mwendazake kwa hili tutamsingizia bure japo baraza lake la mawaziri ni kawaida kukuta waislam watatu tu, lakini hatuwezi kusema eti alikua mdini kwasababu teuzi zake zilikua za kwao ambapo wengi ni wakristo

Samia ana mapungufu mengi tu kwenye awamu yake, tumseme,tumkosoe sana na hakuna kumuogopa huyu bi mkubwa, lakini masuala ya udini na uzanzibar wake tafadhali tusiyaingize huko.


Awamu ya Samia mengi ya hovyo yamejitokeza mambo mabaya mabaya na utendaji mbovu ulozidi kiwango, lakini hili la udini, uzanzibar au umama tuyaache kabisa

Kingine tuwe makini sana, na tunavyoyajaji mambo, isije ikawa tunacheza ngoma ya genge lile la kikabila,maana nao hawalali wakikesha kumchafua mheshimiwa ili wao warudi kwenye ukuu, tusisahau miaka 6 ya yule mtu ilivyojaa mateso na dhiki, kwenye kuchagua namna ya kudeal na awamu ya 6 tuwe makini tusije tukawa tunawapa nguvu lile genge maana wale sio watu wazuri, kitendo cha ssh kuwa rais kimewauma sana.

Na hawampendi SSH na wanatamani lolote litokee, hawa sasa hivi nao wameanza kujifanya kutetea demokrasia na haki za binadam wakati miaka 6 ya yule jamaa hawa jamaa (gang) walituambia demokrasia haitakiwi na haki za binadam ni mikakati ya mabeberu

Tuweni makini tukihesabu hatua zetu
Wote wale wale tu, hakuna mwislamu wala mkristo, kuna CCM na mabavu yake dhidi ya maslahi mapana ya wananchi, tabaka fulani likilindwa.
 
Mama kapotea baada ya kurudisha wezi.

Yeye mishahara haja ongeza, afu bando GB 1 lina panda toka 1000 hadi 3000. Hiyo increment ina fidiwa na nini?
 
Mama kapotea baada ya kurudisha wezi.

Yeye mishahara haja ongeza, afu bando GB 1 lina panda toka 1000 hadi 3000. Hiyo increment ina fidiwa na nini?
Mama anajitahidi sana ukizingatia global economy, kidogo karuhusu majadiliano kuliko aliepita. I think kama kusingekuwa na mtikisiko wa kiuchumi post pandemic na vita inayoathiri ulaya now nchi ingekuwa tamu. Hata akiingia mwingine inaweza chukua hata five to ten years kuweka mambo ktk unafuu. Pia usisahau CCM ni CCM tu wanalinda masalahi yao kuliko ya wananchi. Na hizi tunazoandika humu ni kujuzana tu, wala haisaidii kivile.
 
Kama ana dini bila udini wakristo hawawezi kumchukia na huo si utamaduni wetu chunguza.
 
Back
Top Bottom