Rais Samia katufundisha kuwa na dini tofauti sio sababu ya chuki

zandrano

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
7,148
7,724
Baada ya Rais wetu Samia kukubali mwaliko wa Papa huko Vatican na kuonekana wakia pamoja na Papa wakionekana wakiwa na furaha, kitendo hicho ni funzo kubwa kuwa hakuna haja ya kuchukiana eti kisa huyu ni mwislamu na yule ni mkristu.

Viongozi hawa wawili wametufundisha UPENDO miongoni mwetu bila kujali dini zetu.
Tuachane na chuki binafsi.....eti unamchukia mtu eti kisa dini yake!!!! huo ni ujinga.

Hakuna haja ya kuwa na chuki eti kwa kuwa huyu ni mwislamu ama mkristu sote tupendane na tuheshimiane.
Hakuna haja ya kukashifiana au kudharauliana.

Usimchukie mtu kwasababu ya IMANI yake.
Tupendane kama binaadamu kama watanzania.

Heko kwa Rais Samia amethibitisha kuwa uislamu ni amani sio chuki wala ugomvi. Heko pia kwa Papa ametu thibitishia wakrisu wote kuwa Ukristu sio chuki wala fitina bali ni Upendo miongoni mwetu.

Upendo upendo upendo upendo upendo
 
Samia ni Kiongozi wengine ni wanyapara.

Watu wamekulia kwenye mifugo unadhani watakuwa viongozi wenye utu au wanyapara? 😁😁
 
Back
Top Bottom