Wanaokatakata umeme wajiandae kubeba virago, Aprili 15

Analogia Malenga

Platinum Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,292
Reaction score
10,842
Waziri wa Nishati, Dk Medard Kalemani amesema mameneja wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) ambao hawatawaunganishia umeme wateja waliolipia huduma hiyo hadi Aprili 16 mwaka huu watapoteza ajira zao.

Agizo hilo amelitoa juzi, mara baada ya kutembelea miradi ya umeme katika kata ya Ntyuka jijini Dodoma ambapo alisema Desemba 30, mwaka jana aliagiza kuwa hadi kufikia Aprili 15, mwaka huu waliolipa gharama za kuunganishiwa umeme wawe wamefikishiwa huduma hiyo.

“Tarehe 16 mwezi huu, kama kutakuwa na meneja hajawaunganishia umeme wateja waliolipia kuanzia siku hiyo ajifahamu kuwa hana kazi. Nitakuja na orodha na nitazisoma wazi kwamba huyu hatoshi kuanzia leo hana kazi,” alisema.

Alisema pia mameneja wanaokatakata umeme vibaya katika maeneo mbalimbali wajiandae kubeba virago Aprili 15 mwaka huu.

Waziri Kalemani alisema katika ziara yake hiyo amegundua kuwa Tanesco wanafunga transfoma moja katika maeneo yanayohitaji transfoma zaidi ya moja.

“Maeneo ambayo umeme unakatikakatika sio Dar es Salaam sio Mbeya ziongezwe transfoma ili umeme uache kukatika. Umeme unakatika kwasababu watu wanakuwa wengi transfoma inazidiwa,” alisema.

Mwananchi
 
Hili la umeme limekuwa tatizo sana huku Tukuyu-Mwakaleli-Rwangwa tumekuwa kama desturi kukaa giza na simu kukaa bila chaji,yaani ni shida huku tanesco wakishinda kwenye kijiwe karibu na kyerucu wanakula bata Laxmi bar!
 
Huyu waziri imeweza kazi, Utendaji wake ni daraja la kwanza , ajabu hilo tatizo la transfoma kuzidiwa uwezo na mahitaji analigundua yeye mtaalamu wa sheria wakati tanesco Ina wahandisi hawajagundua.
Inabidi kukagua vyeti vyao kujua kama kuna rushwa ya mitihani au rushwa nyingine
 
Hapa Mwanza mtaa wa Igogo Kusini kila ikifika saa 1 jioni umeme unakata unarudi saa 5 au 6 usiku sijui waga kuna nini tu, sijui huwa wanapitisha magendo yao hata sielewi! Ila mchana unakuepo tu kama kawaida...
 
Hili la umeme limekuwa tatizo sana huku Tukuyu-Mwakaleli-Rwangwa tumekuwa kama desturi kukaa giza na simu kukaa bila chaji,yaani ni shida huku tanesco wakishinda kwenye kijiwe karibu na kyerucu wanakula bata Laxmi bar!
Hapa meneja Tanesco Mbeya pamoja na team yake inabidi a step down akafanye shughuli kwenye wilaya atakazo zimudu au mikoa atakayo imudu na hii nazani ni katavi,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom