Wanaoisafisha CCM kwa kitendo cha wabunge wa CHADEMA kumsusa JK hali ngumu


V

Vumbi

Senior Member
Joined
Nov 7, 2010
Messages
191
Likes
8
Points
35
V

Vumbi

Senior Member
Joined Nov 7, 2010
191 8 35
Vipo vyombo ya habari vinajaribu kuishawishi jamii kuwa kitendo cha wabunge wa CHADEMA kususia hutuba ya JK si cha kiungwana. Lakini jamii inamtazamo tofauti kabisa na hawa vibaraka na wa mafisadi CCM. Hebu soma huu waraka uliochapishwa kwenye website ya Globalpublisher then chini yake angalia "comment" kutoka kwa wadau. Nimeweka 10 kati ya nyingi, kweli CHADEMA wameikamata nchi.

Waraka kutoka kwa wanafunzi UDOM
NDUGU WAANDISHI WA HABARI,
NDUGU WANANCHI,.
wali ya yote nawashukuru sana kuhitikia wito wetu wa gfafla kuja kujumika pamoja nasi leo hii, akhsanteni sana.

Sisi vijana wasomi wa vyuo vikuu mbalimbali vilivyoko mkoa wa Dodoma kwa pamoja tunapenda kuweka wazi maoni yetu juu ya kitendo kilichofanywa na Wabunge wa CHADEMA jana 18.11.2010 wakati Mhe. Rais alihutubia Bunge.

Kwanza tumeshtushwa na kitendo hicho na kuweka wazi masikitiko yetu kwa kuwa kilichofanyika ni kinyume na matarajio ya wapiga kura waliowachagua waheshimiwa wabunge hao kuwawakilisha ndani ya chombo hicho kikubwa na chenye heshima kubwa ndani na nje ya nchi.

Bunge ni sehemu ya kuwakilisha wananchi kwa hoja chini ya kanuni zilizopo bila kujali itikadi ya chama chochote cha siasa na kazi kubwa ya mbunge ni kuishauri na kuisimamia Serikali kwa niaba ya wananchi waliomchagua au kuwachagua.

Kwa mantiki hiyo basi kama Wabunge hawamtambui Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania maana yake hawana kazi ya kufanya ndani ya Bunge kwani kazi yao kubwa ni kuishauri na kuisimania Serikali sasa kama hawaitambui Serikali hiyo hawana sababu ya kuendelea kuwepo Bungeni.

Pili Baada ya uchaguzi wa Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda, wabunge hao pia walinukuliwa na vyombo vya habari na ushaidi tunao wakiweka wazi kumkubali kiongozi huyo, na kauli mbiu yake ya ‘Bunge moja’ je, kitendo walichofanya inaashiria utekelezaji wa kauli mbiu ya Bunge moja?

Tatu msimamo wa kutomtambua Rais ni wa CHADEMA kama chama na waliotoka nje ya Bunge ni wabunge sasa ni vema wabune hao watambue na kutafakari upya kama kweli wanawawakilisha Bungeni wananchi au cha na kutekeleza misimamo yao bila kujali maslahi ya waliowachagua na kumpa kura nyingi Rais Kikwete?.

Nne Kwa badhi ya wabunge wa CHADEMA kutomtambua Rais wakati akilihutubia bunge ni wazi kuwa hata sheria zitakzopitishwa na Bunge hawatahusika kwa kuwa mwenye mamlaka ya mwisho kukubali sheria iliyotungwa na Bunge itumike ni Rais ambaye wanadai hawamtutambui.Ni dhahiri kuwa watashindwa kufanya kazi yao ya uwakilishi na usimamizi wa Serikali Bungeni .

Je wanawaonesha watanzania dalili gani kama si kutaka kuleta machafuko nchini na mgawanyiko ndani ya Bunge na kwa Jamii kwa ujumla?.

Wananchi waliowachagua wabunge hao wanapaswa kutafakari upya wawakilishi waliowachagua kama wana uelewa wa kutosha kuhusu bunge, sisi vijana wa vyuo vikuu tunajua na tunatambua kuwa Rais ni Sehemu ya Bunge na Bunge haliwezi kukamilika bila Rais na hii ndio maana kila sheria inayopitishwa na Bunge ni lazima yeye Rais aweke sahihi yake.

Katika mazungumo yake na waandishi wa habari wiki hii Mweneykiti wa CHADEMA MHE. Freeman Mbowe, alinukuliwa na vyombo vya habari akisema wabunge wake na madiwani wanaweza kuendelea kuwakilisha wananchi licha ya kutomtambua Rais.

Sisi tunasema hili si sahihi bali ni upotoshaji mkubwa, kamwe mtoto hawezi kudai kuwa hamtabui Baba yake kisha anaendelea kumwita Baba na kutumia kila kitu kinachotolewa na Baba huyo huyo. Huo ni utovu wa nidhamu au kukosa maadili.

Sisi vijana wa vyuo vikuu Mkoa wa Dodoma tunawaomba Watanzania wote wenye nia njema na Taifa letu kuwapuuza wabunge wa CHADEMA na kutambua kuwa lengo lao ni kutaka kutuhamisha kutoka kwenye ajenda ya msingi ya Maendeleo na kubaki kwenye malumbano ya kisiasa kama tulivyoshuhudia katika nchi jirani.

Kamwe tusikubali kudanganywa na watu wachache.

Mwisho tungependa kuwaomba Wabunge wa CHADEMA wawaombe radhi watanzania kwa kuvuruga tashwira safi ya Bunge letu lisilo na ubaguzi na itikadi za kisiasa vinginevyo wanawadharau watanzania waliowachagua wakidhani kwamba niwaadilifu wa Taifa na si cha chama chao.

Tutambue kuwa kazi kubwa ya CHADEMA na Wabunge wake kwa sasa ni kuwachanganya watanzania ili badala ya kuendelea na shughuli za ujenzi wa taifa wabaki na malumbano ya hapa na pale kwa manufaa yao binafsi.

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Bunge letu na kutuepusha na ubaguzi kama huu uliofanywa na baadhi ya Wabunge wa CHADEMA.

Aksanteni sana.

IMESOMWA NA THOBIAS MWESIGA RICHARD
KWA NIABA YA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU MKOA WA DODOMA

Commet 1
Kwa mtazamo wangu, samahani kama ntakosea ni kuona vijana hasa wanafunzi wa vyuo vikuu wakiangalia hii nchi kwa mapana yake na changamoto zinazoikabili hii nchi. Kwa wanafunzi walio makini na wanaofikiria vizuri wangejiuliza "chuo kilifunguliwa lini? Na sababu gani zilizofanya chuo kuchelewa kufunguliwa mwaka huu. Naomba hao wanafunzi wajifunze! UCHAGUZI MKUU HUU SIO WA KWANZA kufanyika Tanzania. Chaguzi zote zilizopita hayakutokea haya ya mwaka huu. Haya yanatoka wapi ya kuchelewa kufungua vyuo? Nani aliyesababisha haya? Wanafunzi enzi za NDIO MZEE zimepitwa na wakati. Msione ninyi kuchaguliwa na kujiunga na chuo hicho pamoja na kupewa huo mkopo MMEPENDELEWA. NI HAKI YENU. Wanafunzi simameni kudai haki za watanzania.
Tunataka tume iliyo huru na yenye kujenga hoja. Si tume ya NDIO MZEE. Kama ni demokrasia tunaiga, mbona tunakoiga hawafanyi kama sisi? Ikumbukwe Marekani uchaguzi wa kumuingiza Bush junior mhula wa pili matokeo yalichukua takribani mwezi mzima. Vipi tume yetu ya uchaguzi kuambiwa wasimamishe zoezi la utangazaji wa matokeo wawaambie CHADEMA waende mahakamani?

Naomba niwakumbushe wanafunzi kuwa wabunge ni wawakilishi wa wananchi. Mawazo ya wabunge bila kujali itikadi zao ni mawazo ya watanzania. Kama kuna mambo hayaendi sawa, chukua hatua kwa kusema. Ikishindikana, onesha kwa vitendo (DEMONSTRATION) ambacho CHADEMA wamefanya. Kwa hiyo, wanafunzi hawa wamekurupuka kwa hili. Think critically kabla ya kutoa tamko.
Comment 2
TANZANIA NI NCHI YA AMANI TOKA ENZI ZA UKOLONI KWANINI CCM KILA MARA INASEMA IMELETA AMANI SISI WAZEE LEO MIAKA 50 SIJASIKIA TANZANIA ILIWA KUWA NA MATATIZO YA AMANI MUNGU IBARIKI TANZANIA NA PENYE HAKI WATU WAELEZE HUU NDIO USALAMA. USALAMA SIYO KUWANYIMA WATU HAKI ZAO, KUWANYIMA WATU HAKI ZAO NDIO MATATIZO HIVYO KATIBA YA NCHI NI MUHIMU SANA KUBADIRISHWA ILI KULETA AMANI NCHINI JAMANI
Comment 3
wakati nasoma darasa la mkoloni sikuwa na mawazo mpauko kama haya ya vivuli vya wasomi. sishangai haya yote ni matokeo ya shule za kata,ndo upinzani wamekuwa wakipigia kelele sasa ona wasomi wetu na fikra zao. KUNA TAIFA LA BAADAE HAPO? UWIIIIIIIIIIIIIIIIII Comment4
Nilidhani vijana wasomo wangefikilia kwa undani zaid na uchunguzi wa kutosha kuhusu jambo hili kumbe ni kaz bure,elimu inawakomboa vp kifira nasikitika sana haya ndo mawazo ya viongozi wa kesho kweli? La hashaaa! fungukeni kifikira na kuwa na tabia ya kufanya uchunguzi wa kutosha kuhusu jambo fulani kisha ndo unasupport hoja au kupinga ,ni hayo wasomi wenzangu!!!!
comment5
Hamna wanafunzi hapo, wasomi wa hivi? Labda wanadhani wasipo support CCM watafukuzwa chuo.
UDOM hakuna somo la DS siku hizi mbona siwaelewi

comment 6
kama kweli wasome basi wangalipinga mambo mengi yanayoenda dhidi ya taifa ufisadi, majambazi, wafanyya wa east afrika kutolipwa mishahara yao tangu afrika mashariki ivunjike wakati kenya na uganda wamelipwa na pia albino kuua.

hawa sidhani kama wanastahili hata kuitwa wasomi hawajui wamekula nini jana no bora kuwapuuza, wanglikuwa wanajua haki basi wangalizungumzia kikamilifu na siyo kudanganya watu.

mtu akizungumza ukweli eti analeta hatari nchini hamjua kama dulma ndio huleta hatari katika nchi. kwanza tanzania ni nchi ya aman tangu historia yake enzi za wakoloni hapajatokea matatizo ila viongozi wanatumia hili usalama la kupitishia mambo yao.
MUNGU IBARIKI AMANI YA TANZANIA LAKINI KWENYE UOVU UFICHULIWE MAANA NDIO HATARI KATIKA AMANI YA NCHI LEO HATA KUKU UKIMBANA ATAKURUKIA NA KUKUKWARUZA NA MAKUCHA. AMANI SIKO ZOTE INADUMU INAPOKUWEPO HAKI MUNGU IBARKI HAKI AMEN comment7Nyie mtakua mmetumwa si mawazo yenu maana mnaonyesha pamoja na shule yenu mliyonayo bado uwezo wenu mdogo kihoja,fanyeni utafiti kwanza na mpate sababu ya msingi ya kwanini CHADEMA wabunge waliamua kutoka nje wakati Raisi anautubia bunge alafu pitia kanuni za bunge muone kama zinaruhusu au haziruhusu kufanya hivyo.Me nafikiri nyie mgekuwa watu wenye mtizamo mzuri zaidi kumbe nanyie bado.Maisha na Siasa za Ndiyo Mzee zimepitwa na wakati watu wanajenga hoja na wanazisimamia na kuzitetea.Lengo CHADEMA si kuleta vulugu nchini kama mnavyosema no ni kutetea DEMO ya ukweli si uongo kama tulioyaona wakati wa uchaguzi,waache watanzania wachague viongozi wanaowahitaji wao na si kuwachagulia viongozi.comment 8Bila kukukosoa Egla, unayejisema msomi. Unaposema Chadema watoe elimu bure na afya kwa majimbo waliyoshinda una maana gani? Au unafikiri vyama vinachapisha pesa. Kwa kukuelimisha kidogo iyo si kazi ya Chadema iyo ni kazi yaserikali. Chadema hawana serikali, hwana madaraka ya kukusanya kodi na kuzigawia. Rais na serikali yao ndo kazi zao. Nadhani huna usomi wowote, na kama kweli upo Chuo umeingia kwa milango ya nyuma, na ni aibu kwa taifa kuona mwanafunzi wa chuo hajui kuwa chama cha upinzani hakina uwezo wa kusimamia kodi ila kuikosoa serikali. Taifa lina kazi comment 9..kama wasomi wetu ndio hawa nchi yetu inakwenda kubaya sana, nilitegemea wasomi ndiyo wangeelewa mantiki ya kile kilichofanywa na Chadema.
Kweli sasa hata elimu yetu ya vyuo vikuu imechakachuliwa!
nadhani vile vile, hawa "wasomi" wamesahahu kuwa ni kinyume cha sheria kujihusisha na siasa wakiwa vyuoni.....ni agizo la serikali yao ya CCM!!!
Acheni kujipendekeza kwa serikali, kilichofanywa na wabunge wa chadema ni sehemu ya mchakato wa kuidai katiba mpya, si kwa maslahi yao ni kwa maslahi ya taifa! comment 10Acheni kulipuka na nyie...kabla ya kurukia kwenye majukwaa ni lazima muwe na uhakika na mnachotaka kukisema, hata huo usomi mnaojifanya mnao ni wa mashaka kwani hakuna msomi anaeweza kufanya jambo bila kufanya critical analysis! Acheni kua vibaraka....nyie mmetumwa...
 
Azimio Jipya

Azimio Jipya

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2007
Messages
3,370
Likes
17
Points
135
Azimio Jipya

Azimio Jipya

JF-Expert Member
Joined Nov 27, 2007
3,370 17 135
Nimesema tena; Sisiem wana akili nyingi na ufahamu kidogo sana kama wa sisimizi..na hii ni hatari

Wako kwenye kiza.. Kwa mikono yao .. Taratibu wanajifuta kwenye uso wa dunia ... !

Na kwa ufahamu walio nao...hatachukua ushari wowote..hadi wajimalize kabisa..!
 
N

nkomelo

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2010
Messages
212
Likes
4
Points
35
N

nkomelo

JF-Expert Member
Joined Jan 25, 2010
212 4 35
kwa kweli wanazuoni wenzangu tujitafakari kabla ya kujitokeza kwa wanajamii wanaoamini sana hoja wa wasomi.fasili halisi ya msomi ni kueleza mambo kwa uwazi na kufanya tafiti,kwa hili tujitafakari tena
 
G

Gurtu

JF-Expert Member
Joined
May 15, 2010
Messages
1,210
Likes
10
Points
135
G

Gurtu

JF-Expert Member
Joined May 15, 2010
1,210 10 135
CCM wanawanunua watu kama wasomi ili neno likisikika kwamba limetoka kwa wasomi basi litaonekana la maana. Hata mtu asiyeenda shule anatambua kuwa waliojiita wasomi ni wapumbavu.

Ni msomi gani asiyehoji vitu vya msingi kama; kwanini Tume inatangaza matokeo ya kura kule Dar huku matokeo ya Geita kule kura zilikopigwa zinatofautiana na matokeo ya Tume? Wanachosoma kinawasaidia kuwa watu wa aina gani? Mtu mwenye akili anatambua kuwa hao wanaojiita wasomi wanayasema mambo ambayo wameambiwa na mafisadi wayaseme.
 

Forum statistics

Threads 1,236,918
Members 475,327
Posts 29,272,681