Wanaoharibu Bunge ni Kina Nani?

Wanaoharibu Bunge ni Kina Nani?

kiwatengu

Platinum Member
Joined
Apr 6, 2012
Posts
19,309
Reaction score
17,845
Kila sehemu sasa, ni mazungumzo ya Bunge na Utovu wa Nidhamu...
Kila mtu anazungumza...

Hata hapa mengi sasa ni kuhusu Bunge..
Wanaoharibu sasa ni kina nani?

A. Spika na Naibu Spika

B. Wabunge wa Upinzani

C. Wabunge wa CCM

D. Wote

Tungepata Poll hapa ingependeza zaidi...

Nchi sasa inalijadili Bunge...

Kwenye media nyingi sasa ni bunge..nidhamu ya bunge..nani wanapaswa kulaumiwa katika hili?
 
A na C wanahuska.SPIKA NA NAIBU WAKE WAMEKUWA KIMYA PINDI MBUNGE ANAPOVUNJA KANUNI,KWA PANDE ZOTE.LAKINI IKITOKEA PANDE MOJA IMEBAINI UKIUKWAJI WA KANUNI MAAMUZI YA KITI HAYAELEWEKI. MARA MKUKI KWA NGURUWE....MARA RULING BAADAE, HUKU WENGINE WANAUMIA!
 
Chadema wanaharibu Bunge.

Mbowe kashindwa kuongoza upinzani.

Wabunge wa chadema wanajiendea tu kama mbuzi wa Vingunguti wasio na mchungaji.

Hamad Rashid aliongoza vizuri zaidi upinzani Bungeni katika Bunge la tisa.
 
Wote wako kimipasho zaidi badala ya kufanya kazi tuliowatuma, kwani Wengi wao ni wanafiki, waoga, wabinafsi na mashabiki.wachache sana wanaelewa na kusema kwa ajiri ya taifa.
 
Wabunge wachache wa chadema wanaotumia bunge kugain political popurality na sympathy ya wananchi huku wakiwa hawajijui kuwa tayari watanzania wameshawachoka kwa singo zao za marudiorudio.
 
Yako ni kwa wabunge wa upinzani....ngoja tuone Watanzania wengine wanaonaje..
 
Kila sehemu sasa, ni mazungumzo ya Bunge na Utovu wa Nidhamu...
Kila mtu anazungumza...

Hata hapa mengi sasa ni kuhusu Bunge..
Wanaoharibu sasa ni kina nani?

A. Spika na Naibu Spika

B. Wabunge wa Upinzani

C. Wabunge wa CCM

D. Wote

Tungepata Poll hapa ingependeza zaidi...

Nchi sasa inalijadili Bunge...

Spika na Naibu wake PLUS Wabunge waMAGAMBA
 
Hapo A na C wanahusika. maana kwa tundu lissu kuomba kutoa taarifa kulikuwa na kosa gani??? Je, si haki ya kila mbunge kuomba mwongozo wa spika au kutoa taarifa. Je, kanuni za bunge zinasema mbunge asimame atoe mwongozo au kuomba kutoa taarifa mara ngapi kwa siku/kikao. Ile mbukwinyi ya kibaigwa anajichanganya mno.
 
Wote wako kimipasho zaidi badala ya kufanya kazi tuliowatuma, kwani Wengi wao ni wanafiki, waoga, wabinafsi na mashabiki.wachache sana wanaelewa na kusema kwa ajiri ya taifa.

Ni kweli mkuu..nilishangazwa sana na Yule mbunge wa viti maalumu...aliyesema yeye ni msomi wa sheria..lakini maelezo yake yote yalikuwa Mipasho tupu..na alishangiliwa sana

Pia yule..Mpina CCM jimbo la Kisesa! alitoa point nyingi sana za maana yeye alipigiwa na upinzani...
 
Wabunge wachache wa chadema wanaotumia bunge kugain political popurality na sympathy ya wananchi huku wakiwa hawajijui kuwa tayari watanzania wameshawachoka kwa singo zao za marudiorudio.

Umeongea point mkuu hawa vijana wanageuza bunge ni sehemu ya kampeni.
 
Mimi nadhani katika multiple choice yako jibu ni "B" yaani wabunge wa upinzani baaasi!! nitaishia hapo. Lakini ukitaka nifafanue zaidi ni kwamba Kabla hatujaingia kwenye Siasa za vyama vingi bunge letu lilikuwa halina mgongano wowote kila kitu kilikuwa kinapita kwa 100% na tulizoea kelele zozote bungeni zilikuwa ni za kupongezana na kugonga meza. Lakini baada ya kuingia Siasa za vyama vingi hasa kipindi hiki ambacho wamepatikana watu wanaozijua sheria na wajibu wao kama wabunge mfano watu kama Tundu Lisu, Mnyika, Machali na Mkosamali wamekuwa wakiisumbua sana Meza ya Spika.

Kutokana na Kiti cha Spika kutokuzoea hizi changamoto za kuhojiwa hojiwa hivyo kimeamua kutumia nguvu ili kukilinda chama tawala dhidi ya fedheha kwa wananchi inayopelekea wapinzani pia kupatwa na hasira kutokana na ukandamizaji huu hivyo kusababisha haya yanayotokea Bungeni kutokukiheshimu tena kiti cha Spika. Hebu chukulia mfano Hasira za Ndugai kumtoa nje Tundu Lisu kwasababu tu anasimama mara nyingi kuomba muongozo na kuitafsiri kama ni fujo je sheria zinasemaje kuhusu mtu kuomba mwongozo? zimeweka kikomo? Kwahiyo wanao lihalibu Bunge to me ni Wabunge wa Upinzani Watanzania hatukuzoea watu CRITICAL.
 
Hapo A na C wanahusika. maana kwa tundu lissu kuomba kutoa taarifa kulikuwa na kosa gani??? Je, si haki ya kila mbunge kuomba mwongozo wa spika au kutoa taarifa. Je, kanuni za bunge zinasema mbunge asimame atoe mwongozo au kuomba kutoa taarifa mara ngapi kwa siku/kikao. Ile mbukwinyi ya kibaigwa anajichanganya mno.

ha ha ha..
 
mkuu ccm wakubali yanayosemwa yana ukweli. Sana ila wanajifanya hawajui. Time will tell

Chadema wanaharibu Bunge.

Mbowe kashindwa kuongoza upinzani.

Wabunge wa chadema wanajiendea tu kama mbuzi wa Vingunguti wasio na mchungaji.

Hamad Rashid aliongoza vizuri zaidi upinzani Bungeni katika Bunge la tisa.
 
Spika na Naibu wake kwani wao ndio wenye mamlaka. Kama wanasikiliza ya pembeni badala ya terms of reference ya ajira yao kazi itawashinda. Haki .... haki daima. Yeyote anaeenda kinyume na kanuni anapashwa kuchukuliwa hatua stahili!
 
Naibu spika haenei kwenye kiti chake kwa hiyo as a defensive mechanism anaamua kutoa maamuzi ya kipumbavu yanayotokea kwenye kichwa chake ambacho pia nahisi ni kibovu badala ya kufwata kanuni. Wabunge wa CCM wanatia hasira sana kwa mtu yoyote mwenyeakili timamu kutokana na yale wanayoyafanya bungeni, hasa kwa kukubali mambo ya kipuuuz kupita, suala kama la kutenga 1 Bilion kwa ajili ya kumzika Lukuvi badala ya kuielekeza fedha hiyo kwenye kuwasaidia wananchi waliohai.

Baada ya kusema hayo A na C ndio wanaotuharibia Bunge. Ikumbukwe kuwa kazi za wabunge ni kuisimamia Serikali na sio kuilinda serikali na kuwa ndio wasemaji wa serikali. Na Pia ni kuwakilisha mawazo na interests za wapigakura wao Bungeni, kwa wanayoyafanya wabunge wa ccm cdhani kama yanalenga kumfaidishwa mwanakijiji wa songambele au Msanga!!
 
'A' yaweza kuwa sahihi zaidi.

Naona wachangiaji wengine wanajibu zaidi ya jawabu moja hivyo nami naongezea, hii attachment pia ndio inafanya wale wa 'class A' na 'wafuga mbwa' kushindwa kuainisha kilichomo ndani ya mafuvu yao.
edu v intel.jpg
 
Back
Top Bottom