McLaren
JF-Expert Member
- Feb 19, 2025
- 1,135
- 3,632
Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi Mkuu wa LATRA, Dkt. Habib Suluo wakati wa kufunga semina ya siku mbili ya waandishi wa habari iliyofanyika Kibaha, Mkurugenzi Mkuu wa LATRAamesema LATRA itafuta leseni za kampuni za usafirishaji zitakazobainika kusitisha huduma kutokana na kupanda kwa gharama ya mafuta nchini.
Amesema kuwa licha ya kupanda kwa bei ya mafuta, bado hali hiyo haijafikia kiwango cha kusababisha kampuni kushindwa kutoa huduma. Amesema kwa sasa bei ya mafuta inayokadiriwa kuwa kati ya shilingi 3,800 hadi 4,000 haijaathiri kwa kiasi kikubwa uendeshaji wa huduma za usafiri.
Aidha, Dkt. Suluo amezitaka kampuni za usafirishaji zinazodai kupata hasara kufuata taratibu za kisheria, ikiwemo kukata rufaa katika Tume ya Ushindani, ili malalamiko yao yaweze kushughulikiwa ipasavyo.
Pia ameonya vitendo vya baadhi ya watoa huduma, hususan daladala, kugoma kutoa huduma kwa kisingizio cha kupanda kwa bei ya mafuta, akisisitiza kuwa hatua kali zitachukuliwa dhidi ya watakaokiuka sheria.