Wanaogawa magazeti bure ni akina nani na wanafaidika vipi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanaogawa magazeti bure ni akina nani na wanafaidika vipi?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Ntemi Kazwile, Sep 6, 2010.

 1. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #1
  Sep 6, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Habari za nakala za gazeti la Changamoto, lilokuwa limesheni makala juu ya maisha binafsi ya Dr Slaa, zilinishitua sana kwa sababu siyo kitu cha kawaida, nilishituka zaidi kwa sababu makala kuu ya gazeti hilo ilikuwa inahusu maisha binafsi ya mgombea urais na ilikuwa ikielezea ufusika (kitu ambacho si sifa njema kwa mtu anayetaka kuwa kiongozi wa nchi).

  Baada ya kutafakari kwa kina niligundua kuwa kuna kubwa zaidi lililo nyuma ya ukarimu huo usiokuwa wa kawaida (kugawa gazeit bure). Siku chache baadaye, nilipata majibu ya maswali mengi yaliyokuwa yakinisibu baada ya kuona taarifa ya habari ya Channel Ten ya Jumapili tarehe 5 September 2010.

  Nilijua bila shaka yeyote kuwa aliyekuwa nyuma ya ukarimu wa kugawa Changamoto bure ni Rostam Aziz na mafisadi wenzake wanaoweweseka na nilijua pia kuwa wamefanya hivyo ili kuhakikisha kuwa Dr Slaa anapata doa ili wapiga kura wapata swali la kujiuliza juu ya uadilifu wake.

  Lakini pia nilijua kuwa Rostam na mafisadi wenzake wanajua kuwa Dr Slaa hana doa lolote katika utendaji wake wa kazi na wameshindwa kupata doa lingine isipokuwa kwamba anaishi na mwanamke ambaye alifunga ndoa na mtu mwingine mwaka 2002, wameshindwa kumkosoa katika uadilifu wake wa kutetea wanyonge na kuwachukia mafisadi kwa dhati, Dr Slaa anaamini kuwa kikwazo kikubwa kabisa cha Tanzania kujinasua kutoka kwenye lindi la umasikini ni UFISADI, na ameahidi kuwashughulikia ipasavyo akipata ridhaa ya watanzania kuwa Rais wetu.

  Dr Slaa anaamini kuwa tatizo kubwa la Tanzania ni mikataba ya kinyonyaji (mfano barabara inayotakiwa kujengwa kwa bilion 2 kujengwa kwa bilion 10, ukodishaji wa mitambo tusiyoihitaji kwa gharama kubwa) na ameahidi kuwa akiwa Rais atahakikisha wale wote waliohusika na mikataba mibovu wanawajibika. Rostam ni mtu mmoja ambaye mikataba yote mibovu iko nyuma yake (Kagoda, Richmond, Deep Green FInance,etc) na anauhakika kuwa kama kuna serikali adilifu hawezi kupona kama utafanyika uchunguzi ulio huru na wa haki wa kuwatafuta watu wote walio na wanaolifilisi taifa hili kupitia mikataba na hila za kifisadi.

  Mimi naamini kuwa Tatizo la Tanzania siyo mtu kuoa mwanamke aliyeolewa na akaachana na mmewe wa kwanza, kuna watanzania wangapi wanaishi salama salmini na wake au waume wa aina hii?

  KIKWAZO CHA MAENDELEO YA TANZANIA NI UFISADI --- tunatakiwa tuwaunge mkono watanzania wote wanaoonesha nia ya dhati kupambana na ufisadi. DR SLAA ameonyesha dhamira hiyo na ameahidi kuwa hii ndiyo kero namba moja atakayoishughulikia.

  TUMUUNGE MKONO Dr SLAA ili tuweze kuondoka hapa tulipo tuende kule tunakokutaka.

  Kwa wasiojua Rostam Aziz anamiliki Channel Ten, magazeti ya Mtanzania na Rai na ukiangalia kwa makini utaona yote yanaandika sifa hasi za Jemedari Dr Slaa (doctor wa ukweli)
   
 2. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #2
  Sep 6, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Hawa mafisadi wa mali ya Watanzania watachukua hatua zozote zile ili waendelee kuwa katika madaraka. Vilevile wanahofia hukumu zitakazowafuata baada ya kutoka katika madaraka. Wanajua fika kuwa wamefanya madhambi makubwa na hukumu ya dhambi zao wanazijua. The guilty are always afraid!
   
 3. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #3
  Sep 6, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,635
  Likes Received: 4,744
  Trophy Points: 280
  Wanaogawa magazeti hayo ni wanamtandao wa KIKWETE, hiyo ni staili yao kwa ni hata 2005 walifanya hivyo hivyo. Lakini Kikwete na genge lake wakae wakijua kuwa Watz siyo wajinga kama wanavyofikiri, huu mchezo wao unawajaza watu chuki kwani wanajua kuwa hizo ni fitina za kisiasa. KIKWETE na WAHALIFU WENZAKO kamwe hamtakwepa hasira ya wana wa nchi hii. Yaani nyie ambao ufisadi wenu umewaathiri mamilioni ya watanzania mnamchafua mzalendo wa kweli ambaye yuko tayari hata kuhatarisha maisha yake kwa masilahi y Taifa. Kama Mungu Muumba wa mbingu na nchi aishivyo hamtabaki salama. Tanzania ni kwa Watanzania na si kwa CCM na wateule wake wachache.TUMEONEWA KIASI CHA KUTOSHA, TUMEFISADIWA KIASI CHA KUTOSHA, TUMEDHALILISHWA KIASI CHA KUTOSHA CHINI YA MAKUCHA YA CCM SASA TUNATAKA MAPINDUZI YAKWELI. OLE WAKO KIKWETE NA GENGE LAKO
   
Loading...