Mpaka Kieleweke
JF-Expert Member
- Feb 27, 2007
- 4,132
- 1,571
Hivi hawa wapambanaji mbona majimboni mwao wanakumbana na aibu?
Ni kuwa wananchi hawawaelewi ama?
Je? wanaonekana kuwa wasanii?
Je?wamesahau kuhudumia wananchi wao wakijificha kwenye kichaka cha kupambana na mafisadi?
Mbunge Aloyce Kimaro azomewa mkutanoni jimboni kwake
Daniel Mjema na Rehema Matowo,Moshi
Â
MBUNGE wa Vunjo, Aloyce Kimaro jana alikuwa na wakati mgumu baada ya kuzomewa na kundi la wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika mji mdogo wa Himo ulio kwenye jimbo la Vunjo, Moshi Vijijini.
Kimaro ni mmoja wa wabunge ambao wanaonekana kujitoa mhanga katika vita ya ufisadi, lakini jana alijikuta kwenye hali ngumu wakati akihutubia mkutano wa hadhara.
Kundi la watu takribani 100 wanaodhaniwa kuwa ni wafuasi wa chama pinzani cha TLP ambacho ndicho chenye nguvu eneo hilo, lilipiga kelele likisema "hatukutaki" wakati Kimaro alipokuwa akihutubia mkutano huo.
Â
Kadhia hiyo ilianza wakati Mbunge Kimaro alipozungumza na kuelezea kuwa yuko katika hatua za mwisho za kutatua kero ya muda mrefu ya maji katika eneo hilo lenye uhaba mkubwa wa huduma hiyo.
Baada ya kugusia tu suala hilo, Kimaro alishtukia sauti zikitoka kwenye kundi hilo zikidai kwa kelele kuwa mbunge huyo ni mwongo na kwamba hawamtaki, lakini Kimaro akaendelea kusisitiza kuwa kero ya maji itakuwa historia muda mfupi ujao.
Kelele za wananchi hao zilizidi baada ya viongozi wanne waliojitoa TLP kusimamishwa jukwaani kuwahutubia, wakielezewa kuwa wameamua kujiunga na CCM.
Wananchi walidai kuwa viongozi hao ni wasaliti na kuwatuhumu kupokea Sh500,000 kila mmoja ili waisaliti TLP. Lakini walipopata nafasi ya kuzungumza jukwaani, wenyeviti hao walikanusha tuhuma hizo.
Â
Hali hiyo ilimlazimisha katibu mwenezi wa CCM wilayani Moshi Vijijini,Jamal Hussein kuchukua kipaza sauti na kuwakemea wananchi hao waliokuwa wakizomea, akidai kuwa anawafahamu kwa majina.
Hussein alisema kwa kuwa CCM ni chama cha watu makini na wastaarabu hawana sababu ya kulipiza kisasi kuvuruga mkutano wowote wa kambi ya upinzani kama lilivyofanya kundi hilo.
Â
Tishio hilo lilisaidia kupunguza kelele za sauti hizo na mkutano huo ukaendelea kama kawaida kwa Kimaro kuwaelezea wananchi kampeni yake mpya ya âSafishaâ yenye lengo la kuondoa viongozi wabovu.
Naye mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango Malecela alizungumza kwenye mkutano huo na kuwataka viongozi wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) kuwaunga mkono wanawake wanaojitokeza kuchuana na wanaume katika chaguzi, akisema utafiti unaonyesha wanawake ni waadilifu zaidi kuliko wanaume.
Kilango aliwahamasisha wanawake nchini kugombea nafasi mbalimbali za uongozi nchini ikiwamo urais mwaka 2015.
Alisema wanawake wanatakiwa kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi za uongozi katika jamii kwa kuwa waliachwa nyuma muda mrefu na kudharauliwa na sasa ni wakati wao.
"Wanawake sasa ni wakati wetu; tuliachwa nyuma na kudharaulika muda mwingi, sasa ni wakati wetu," alisema Kilango.
Hata hivyo, alipotakiwa baadaye kueleza endapo atakuwa mmoja wa wanawake watakaochukua fomu za kuwania urais mwaka 2015, Kilango alisema: "Aaaaa! ni mapema mno kuzungumzia hili. Mimi nilikuwa nawahamasisha tu... suala la nani atasimama ni juu yao,".
"Isitoshe kusema sasa kwamba kwamba nina mpango wa kugombea urais mwaka 2015 sio sahihi kwa kuwa wakati huo nitakuwa mzee. Hili nawaachia wanawake watakaokuwa vijana wakati huo."
Kilango pia alihutubia mkutano wa hadhara juzi kwenye jimbo la Moshi Mjini ambako alitangaza kupiga kambi hadi mwaka 2010 ili kuhakikisha kuwa CCM inanyakua jimbo hilo, uamuzi ambao unamuingiza kwenye vita kali na mbunge wa sasa, Philemon Ndesamburo.
Katika kuonyesha kuwa Ndesamburo hana nguvu kwenye jimbo hilo, Kilango aliwaambia wanachama na viongozi wa CCM kuwa mbunge huyo kutoka Chadema ameshinda mara mbili mfululizo kutokana na matatizo ya WanaCCM wenyewe na kuwataka wajisafishe.
Lakini jana Ndesamburo alijibu mapigo ya mbunge huyo na kueleza kuwa hatishwi na kitendo chake cha kupiga kambi jimboni humo akisema mpango huo ni sawa na kutikisa kibiriti kilichojaa.
Ndesamburo aliiambia Mwananchi jana kuwa hatishiki na mkakati huo wa Kilango na akakanusha madai ya mke huyo wa makamu mwenyekiti wa zamani wa CCM, John Malecela, akisema hajawahi kumwambia kuwa wengi wanaompigia kura ni WanaCCM.
Â
âMimi sitishiki... yeye afanye kampeni anavyotaka,â alisema Ndesamburo ambaye anamalizia kipindi cha pili cha ubunge wake tangu alipoingia mwaka 2000 akiwa amelichukua kutoka kwa mbunge wa NCCR Mageuzi, Joseph Mtui ambaye alikuwa mbunge kuanzia mwaka 1995.
Ndesamburo, ambaye liibuka na ushindi wa kura 32,035 katika uchaguzi wa mwaka 2005 akimuacha mbali mgombea wa CCM, Elizabeth Minde (23,773), aliongeza kusema: âSijawahi kumwambia hata kidogo kuwa wanaonifanya nishinde ni wafuasi wa CCM⦠WanaCCM hawazidi 5,000, mimi nilipigiwa kura na wananchi 30,000.â
Â
Mbunge huyo wa Moshi Mjini alimwonya Kilango kuwa asijaribu kutingisha kibiriti kilichojaa na kusisitiza kuwa kwa mujibu wa takwimu, wanaompigia kura si CCM pekee, bali wengi ni wale wasio na chama.
Â
âHapa Moshi Mjini Chadema tuko kama 2,000. Hivi hawajiulizi hizo kura za ziada zilitoka wapi kama sio wananchi ambao hawayumbishwi na propaganda chafu,â alihoji Ndesamburo.
Â
Ndesamburo, ambaye pia ni mwenyekiti wa mkoa wa Chadema, alimtaka Kilango kuimarisha kwanza jimbo jirani la Same Magharibi ambako alikuelezea kuwa si shwari. Jimbo hilo linaloshikiliwa na Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Dk David Mathayo na Ndesamburo alidai kuwa linapwaya hivyo Kilango hana budi kuweka kambi huko ili kulinusuru lisichukuliwe na wapinzani.
Alipoulizwa kuhusu madai hayo ya Ndesamburo, Dk.Mathayo alisema kauli hiyo ni ya kisiasa na kwamba kati ya majimbo yote ya mkoa wa Kilimanjaro, jimbo lake ndilo salama kwa asilimia 100.
âMambo niliyofanya Jimboni hayajawahi kufanywa na mbunge yoyote tangu uhuru na wewe kama mwandishi unaweza kwenda mwenyewe ukafanya utafiti,â alitamba Dk. Mathayo. Â Dk. Mathayo alisema katika kipindi kifupi ametoa mifuko ya saruji kwa ajili ya kujenga vyumba vinne vya madarasa katika kila kata, kutoa darubini nane kwa zahanati nane na kujenga soko la kimataifa.