Wanaodai Pride Tanzania kulipwa Julai 2023

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,903
945

WANAODAI KAMPUNI YA PRIDE TANZANIA KULIPWA JULAI 2023

Serikali itaanza kuwalipa Watanzania wanaoidai Kampuni ya Pride Tanzania Julai mwaka huu baada ya taratibu za ufilisi kukamilika. Pride ilianzishwa Mei 5, 1993 chini ya Sheria ya Kampuni (CAP 212) kwa lengo la kutoa mikopo midogomidogo kwa wajasiriamali.

Akiuliza swali la nyongeza Ijumaa, Juni 9, 2023 la Mbunge wa Iringa Mjini (CCM), Mhe. Jesca Msambatavangu alihoji kuwa kama Serikali ina mpango gani wa kuwalipa wanaodai mkoani Mtwara na nchi nzima.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Hamad Hassan Chande amesema tathimini ilifanyika nchi nzima hivyo wote wanaodai watalipwa Julai mwaka huu baada ya taratibu za ufilisi zitakapokamilika.

Katika swali la msingi, Mbunge wa Mtwara Mjini (CCM), Mhe. Hassan Mtenga amehoji ni lini Serikali itawasaidia wakazi wa Mtwara Mjini waliojiunga na Kampuni ya Pride kurejeshewa fedha zao.

Akijibu swali hilo, Mhe. Chande amesema Serikali ilifanya tathmini ya hali ya kampuni ya Pride na kufuatiwa na ukaguzi maalum uliofanywa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuhusu kutambua mali na madeni ya kampuni hiyo.

Amesema kufuatia tathmini hiyo, Serikali inaendelea na taratibu za kisheria za kuifilisi Pride na kwamba madeni yatalipwa kwa kuzingatia sheria na taratibu za ufilisi na yanatarajiwa kukamilishwa Julai 2023.

Aidha, Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Naghenjwa Kaboyoka amehoji Serikali ina mpango gani kumaliza tatizo la mikopo ya kausha damu, komandoo na mingine inayoumiza wananchi.

Akijibu swali hilo, Chande amesema kuwa taasisi zinazotoa mikopo midogo zinatakiwa kufuata sheria na kujisajili.
 

Attachments

  • pride-pic.jpg
    pride-pic.jpg
    62.7 KB · Views: 5
  • WhatsApp-Image-2023-04-06-at-02.33.13.jpeg
    WhatsApp-Image-2023-04-06-at-02.33.13.jpeg
    40.2 KB · Views: 5
  • mqdefaultmkjui.jpg
    mqdefaultmkjui.jpg
    10.5 KB · Views: 4
  • sddefaultaqw.jpg
    sddefaultaqw.jpg
    27.6 KB · Views: 5
Back
Top Bottom