Wanandoa na vita ya fedha chumbani…..........!

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,806
15,332
Je unadhani kwenye vurugu za kindoa, fedha haina mchango wake? Kama unadhani hivyo, utakuwa umekosea sana. Hebu soma kuhusiana na utafiti huu uliofanyika kule Marekani.

Utafiti uliowahi kufanywa na taasisi ya Harris Interactive (Harris Interactive Poll for Men, Love & Sex) ya nchini Marekani ilibaini kwamba, asilimia 38 ya wanaume na wanawake walioshiriki kura ya Taifa ya maoni kuhusiana na mapenzi nchini humo walisema fedha ndilo tatizo nambari moja linalopelekea kudumaa, kusinyaa ama hata kufikia tamati kwa ndoa.

Mara nyingi matatizo ya fedha hutokana na ukweli kwamba wenza huwa na malengo tofauti ya kifedha na wakati mwingine ni katika mambo ya kawaida tu. Kwa mfano mwanmke anataka Pete ya Dhahabu wakati mume anataka Televisheni ya kioo cha tambarare (Flat Screen TV).

Hii hutokana na kukosekana kwa mawasiliano ya kutosha kuhusiana na malengo hayo na hasa pale ambapo mtu mmoja ndiye anayewajibika za Ankara (bill) nyingi za manunuzi na ikiwa watu hao hawapati muda wa kutosha wa kuzungumzia mambo mengine zaidi ya kupeana madai ya kile kinachotakiwa kupewa kipaumbele.

Tatizo la fedha pia mara nyingi limeonekana kuchangia kwenye kutokea kwa matatizo mengine. Kukiwa na tatizo la fedha tegemea kupewa nafasi chache sana za kufanya tendo la ndoa na mwenzi wako, usitarajie kutayarishiwa chakula kizuri na chochote kile unachotarajia kupata kwa mwenza wako.

Najua mtauliza chanzo, bofya hapa:
How Money Ruins Relationshipshttp://www.articledashboard.com/Article/How-Money-Ruins-Relationships/982316
 

sinafungu

JF-Expert Member
Feb 13, 2010
1,520
859
mkuu uko sahihi. jamaa yangu mmoja miaka ya nyuma mke alimkimbia kisa fedha, pamaoja na kuwa jamaa alikuwa anajitahidi mno kuiangalia familia yake , wakafika hadi kuazisha biashara ambayo mwanamke ndiye aliyekuwa akiisimamia, bali huko ktk biashara mwanamke akakutana na wenye pesa zaidi na (waongo) wakamlaghai hadi kuvujika kwa ndoa yao, hadi leo mwanamke yukoyuko tu na jamaa aliendelea baada ya mtikisiko wa kuvunjika kwa ndoa yao.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom