Wanandoa na extended family

Wanandoa na extended family

CharmingLady

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2012
Posts
18,304
Reaction score
12,997
Habari za jioni mabibi na mabwana katika jukwaa hili?

Naomba tujadili changamoto zitokanazo na kuishi na ndugu wa mume/mke, watoto wa kambo katika familia.

Hii imekuwa changamoto hasa kwa wanawake tushindwa kuishi na ndugu ama watoto wa mwanaume.

Kuna msemo huu "Ndugu hawana jema, hata uwabebe mgongoni" je msemo huu una ukweli?

Je tatizo ni nini?

Ni jinsi gani ya kukabiliana na changamoto hizo??

Nina mifano hai miwili ambayo wadada wameshindwa kuvumilia kuishi na ndugu. Wanalalamika ndugu wa mume wana masimango, hawaridhiki na chochote wanachofanyiwa...

Karibu kwa mjadala
 
Kuna ukweli kuna ndugu ni visirani balaa asione kaka yake kaja na kimfuko,utasikia"anamdekeza sana mkewe,mwanamke mwenyewe sura kama kiazi kitamu sijui alikua kafumba macho"
na upande wa pili mke/mume anaweza akawa ndiye mbaya.
Changamoto ni kubwa kama kuibuka chuki na maneno ya ugomvi kati ya ndugu na mwanandoa mmojawapo.
 
Nilicho observe siku hizi wanawake tuna roho ya ubinafsi yaana ndugu wa mume akufika tu mtu wamesha mchukulia vibaya.Mama mtu akipiga simu anakuja kutibiwa mkwe anaanza kuwambia mashost maneno nao wanamjaza ujinga.

Japo wapo ndugu wasio na adabu wafikapo katika familia ila mini nime observe wanawake siku hizi ni wa binafsi na hawapendi ndugu wa mume yaani wakija wakala bi dada anavimba kana kwamba wamedraw pesa zakr bank

Siku nyuingine ntakuja na uzi ila kina dada tumezidi kuwatrnganisha waume na ndugu zao.
 
Hahahaa ...Ati sura kama kiazi kitamu!
 
ndugu wa mume %kubwa wana hila sana then wao wako hivyo wao
wao wanataka kaka yao alivyokua anawahudumia kipindi yuko single bas hata baada ya ndoa awe vile
hawajui kwamba asa hv anamzigo mwingine na wao wanajifanya baba wenye nyumba
mi kwangu lakini hawanipi shida mradi tunaelewan shauri yao maana naishi na mashemeji na wale wanaokuja kushangaa mji na kuondoka
mradi kaka yao ndo analeta msosi mi sina habari
 
lakini ndugu zake yeye hawana masimango na wanaridhika!!!...mmh!
 
Katika familia zetu hizi za kiafrika hakuna jinsi unaweza kuacha kuishi na ndugu wa Mme/mke,mwanamke mwenyewe kutambua nafasi yake kama kuwajali na kuwathamini.
Kuhusu maneno ni kukubali kuwa huwezi kumridhisha kila mtu kwa jinnsi anavyotaka yeye ,hata kama umeishi na ndugu hukumtenda baya au akaongea kuhusu maisha yenu binafsi,
 
binafsi nimekulia kwenye extended family, ndugu wa pande zote mbili na watu wengine baki wasiopungua wanne, lakini wote ilikuwa sheria moja, shuleshule, kazikazi, kilizo kijijini kusaidia kulima, wote tulikuwa respect na hakuna muda wa kupiga pelepete zisizo na msingi. kwangu mimi extended family haiepukiki, kikubwa ni misingi tu, hakuna upendelleo wa ndugu wa upande wowote, wote ni sawa, na mwanamke anatakiwa ajue hilo.
 
ndugu wa mume %kubwa wana hila sana then wao wako hivyo wao
wao wanataka kaka yao alivyokua anawahudumia kipindi yuko single bas hata baada ya ndoa awe vile
hawajui kwamba asa hv anamzigo mwingine na wao wanajifanya baba wenye nyumba
mi kwangu lakini hawanipi shida mradi tunaelewan shauri yao maana naishi na mashemeji na wale wanaokuja kushangaa mji na kuondoka
mradi kaka yao ndo analeta msosi mi sina habari

kwa hiyo wewe wasiwasi wako ni msosi tu?!!
 
Mfumo huo wa kijamaa na undugu umeshapitwa na wakati..... Sehemu nyingi duniani hakuna tena kubebana kama vile mtu anakilema!! maLovers wanaishi wawil na vitoto vyao kama wamezaa!!
 
Nilicho observe siku hizi wanawake tuna roho ya ubinafsi yaana ndugu wa mume akufika tu mtu wamesha mchukulia vibaya.Mama mtu akipiga simu anakuja kutibiwa mkwe anaanza kuwambia mashost maneno nao wanamjaza ujinga.

Japo wapo ndugu wasio na adabu wafikapo katika familia ila mini nime observe wanawake siku hizi ni wa binafsi na hawapendi ndugu wa mume yaani wakija wakala bi dada anavimba kana kwamba wamedraw pesa zakr bank

Siku nyuingine ntakuja na uzi ila kina dada tumezidi kuwatrnganisha waume na ndugu zao.

heshima kwako!
 
Mfumo huo wa kijamaa na undugu umeshapitwa na wakati..... Sehemu nyingi duniani hakuna tena kubebana kama vile mtu anakilema!! maLovers wanaishi wawil na vitoto vyao kama wamezaa!!

wewe unaongelea "kwingine", tuko hapa ubantuni ongelea mazingira ya hapa. kuna uzi uliwahi kuletwa humu kwamba watu siku hizi hawana shukrani, mtu kasomeshwa na shangazi yake mjomba upande wa bi mdogo lakini toka apate ajira hata kubip ili awajulie hali hakuna, sisi ni waafrika maisha yetu ni ya kuungaunga, tuna jukumu la kuwasuuport walio nyuma yetu kwa chochote kidogo tulichonacho!
 
Kuna ukweli kuna ndugu ni visirani balaa asione kaka yake kaja na kimfuko,utasikia"anamdekeza sana mkewe,mwanamke mwenyewe sura kama kiazi kitamu sijui alikua kafumba macho"
na upande wa pili mke/mume anaweza akawa ndiye mbaya.
Changamoto ni kubwa kama kuibuka chuki na maneno ya ugomvi kati ya ndugu na mwanandoa mmojawapo.

na mara zote ndugu wenye matatizoni wa upande mmoja tu, wa mume! sijaskia mwanamume analalamika shemeji zake wana matatizo, afike mgeni toka kwa mwanamume habari watazipata mpaka wasuka nywele!!
 
kwa hiyo wewe wasiwasi wako ni msosi tu?!!
asikwambie mtu roho mbaya zote unazoziskia kwenye kula
mtu anaekunyima kula muogope kusoma wanasomeshwa na ndgu wengine na ye anachangia pia
binafsi kwangu mimi maneno maneno hayaniumzi na siwezi wafukuza si kwa ndgu yao hata wakijaa maana mi siwezi watesa sijui ntakufa lini
kula ndo kunagombanisha watu mi nakwambia
we fuatlia tu
 
Charminglady;
Sikujua kuwa na weye una inda! Loh! Tabasamu loote hilo kumbe ndani moyo korosho! Weye huna hakika na aliye kuoa? Waliokuja woote wawekee full stop. Pale pale mwanzoni, hata kabla hujafua zile nguo ulizotoka nazo kwenyu. Hakikisha wanaijua mipaka yako na mumeo kwao. Uliolewa na mtu mmoja sio ukoo.
Wa kuja kwenu aje lakini akijua kakayao, kijana wao, au baba mdogo wao, kesha oa. Alimwoa Charminglady. Hajaoa kijiji. Ukiisha kuweka misimamo yako hiyo, sasa wale ambao umewakuta kwake, watoto wa kambo, wapende kwani walikutangulia. Waoneshe kuwa, unawapenda, utawaheshimu nao pia wakuheshimu.
Ukianza kuwa nyanyasa, itakula kwako. Waswahili husema; Nkune nami nkukune! Heshima ni reciprocal!
 
Dah!! My dear charminglady hii mada imefika muda muafaka kwangu kama vile umeniona ninalopitia.Sitapenda kulaumu sana ila kiukweli ni ngumu mwanadamu kumfurahisha kwa kila jambo,chanzo cha yote haya ni inner conflict of interest,Mke hujiona ana haki zaidi na ndugu pia huona wana haki zaidi.

Suluhisho ni nini basi? Mwanamke aliyeko ndoani inabidi aelewe hao watu anaosumbuana nao wana tabia gani,waswahili wanasema mbwa ukimjua jina lake hakusumbui,atambue vitu gani hasa vinavyowafanya wagombane,na wakati mwingine kushuka pia si ujinga,ajikwezae atashushwa na ajishushae atakweza,hekima yahitajika katika kuishi.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom